Kwanini wanyama huwa wanakula watoto wao wadhaifu mara baada ya kuzaa?

Kwanini wanyama huwa wanakula watoto wao wadhaifu mara baada ya kuzaa?

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Habari wanajukwaa!

Ningependa kujua kwa nini baadhi ya wanyama, hasa mamalia na wengine, hula watoto wao dhaifu au waliokufa mara tu baada ya kuzaliwa. Mara nyingi huwa ni tabia ambayo ipo kwa paka, mbwa, fisi pamoja na wanyama wengine, kwani ni vigumu sana kuona amezaa na kukuta vitoto vyake vikiwa hoi taabani au vimepoteza maisha?
images - 2025-03-06T205752.996.jpeg


Je, ni tabia ya kiasili au kuna sababu nyingine za kisayansi zinapolekea kutokea kwa jambo hili?
images - 2025-03-06T205827.915.jpeg


Binafsi nimepata kuwa na mbwa katika makazi yangu kwa vipindi tofauti, na mara kadhaa sijawahi kukutana na kitoto cha mbwa kikiwa dhaifu ama kimekufa na mama yao hajawatafuna.
images - 2025-03-06T205716.179.jpeg


Natamani sana kufahamu kwanini huwa wanawapiga menu, huwa ni njaa tu ama kuna jambo jingine nyuma ya pazia?
 
Logic ipo hapa..
kwanin wanyama wanaokula nyasi ukimtoa nguruwe hawali watoto wao?!

Hapo nadhani utakuwa umenielewa.
 
Logic ipo hapa..
kwanin wanyama wanaokula nyasi ukimtoa nguruwe hawali watoto wao?!

Hapo nadhani utakuwa umenielewa.
Kiufupi TU, kiumbe chochote kinachokula nyama hutakiwa kutoa matunzo ya mwanzo ya mtoto na huchukua muda mrefu mpaka mtoto aweze kujitegemea hivyo idadi inapokuwa kubwa huongeza mzigo Kwa waleaji hapo nature inatake place Kwa mama kupunguza idadi,
Mfano hata ndege anaekula nyama(mara nyingi atricial) hawatagi mayai zaidi ya 3 kwasababu ya kero ya kulea anatotoa mtoto haoni, shingo haijakaza, yupo naked.
Pili mnyama anapotoka kujifungua husikia njaa sana, mara nyingi kukiwa na chakula Huwa Hali mtoto
 
Back
Top Bottom