Kwanini Wapalestina waliisaliti Tanzania na kumuunga mkono nduli Idd Amin kupigana?

Dah! Wee jamaa banha umeachanisha sana maneno afu hujajibu swali uliloulizwa au Mimi ndo sinakuelewa?

Alafu kama idd amini alimpindua mwenzake Sasa yeye alikuwa na hualali Gani, Raia waliyakubali mapinduzi yake, Mimi naona wafuasi wa Obbote nao walikuwa sawa tu kwenda kumuwinda huyo Dada Idd Amini Fred
 
Kama hoja ni dini, mbona ALGERIA taifa la kiislamu liliiunga mkono Tanzania na kutoa msaada muhimu kabisa ?​
'
Kuna Sheikh wa Naijeria kapewa Uraia wa Marekani kwasababu ali-harbor kundi la wakristo wasiuliwe na ISWAP lakini tukio ili aliondoi ukweli kuwa Christian communities in Nigeria have been under unreported siege by Muslims.
Juzi 190 wakristo wamekwenda na maji.
So, hata kama Algeria ilifanya kinyume na PLO hiyo haiondoi ukweli kuwa PLO kumsaidia Amini ilikuwasukumwa na Dini zaidi.
 
Tanzania imeunda mahusiano na PLO hata kabla Iddi Amin hajawa Raisi wa Uganda. Swali linakuja, kwanini mbali na kuwaunga mkono na kuwasemea huko duniani, waliamua kuishambulia Tanzania ?​
Hao PLO walishawahi kupewa hifadhi nchi fulani ya kiarabu.
Wakaishia kuanzisha vita ya kumpindua Rais wa Nchi hiyo.
 
Hao PLO walishawahi kupewa hifadhi nchi fulani ya kiarabu.
Wakaishia kuanzisha vita ya kumpindua Rais wa Nchi hiyo.
Ilikuwa ni Jordan mwaka 1970, PLO walijikusanya na kutaka kumpindua King Hussein ambaye aliwapa hifadhi. Tukio linaitwa The Black September. Inaonesha hii ndiyo tabia yao, sasa nini kitawazuia wao kufanya jambo kama hili tena ?​
 
Watu na Taifa ni tofauti. Watu tunaongozwa kwa hisia na utashi, Taifa huongozwa kwa sera na maslahi. Hadi taifa likaamua kujiingiza kwenye vita ina maana hilo swala limeangaliwa kitaalamu na kwa mapana. Hivyo PLO, Libya na wengine kumuunga mkono Amin haikuwa ni suala la dini peke yake. Kuna kitu hatukifahamu...​
 
PLO haikumuunga mkono Idi Amin.
Algeria nchi ya kiarabu jirani na Libya ndio ilikua nchi ya kwa kutangaza bila kupepesa macho kuwa inaunga Tanzania mkono katika vita na Uganda. Algeria walituma zana nyingi sababu walikua na vifaa vya kurusi ambavyo Tanzania pia ilikua navyo.
Mzayuni angepewa Uganda ndio ungejua matatizo yao sababu hao wamagharibi wangekuwa nae akimega mkoa mmoja hadi mwingine.
 
Haya mambo mnafundishwa Sunday school. Mnatiwa sumu dhidi ya waislam na uislam. Mkija humu mnaandika utumbo usiokichwa waala miguu
Kaka naongelea from my experience, miaka yangu yote ya kwenda kanisani hata siku moja sijawahi kusikia wanaongelea uislamu kanisani. Mimi ni mkatoliki.
 
Hapo nimetaja maslahi na dini, Algeria anaweza kuwa alikuja kimaslahi au kwa good cause.

Uislamu kwenye ile vita unakuja kwa Iddi Amin, sio kwa Tanzania wala Uganda ambazo sio nchi za Kiislamu.
 
Likini kwanini nchi ya kiislamu na kiarabu, ALGERIA iliiunga mkono Tanzania ?​
Na kuweka kumbukumbu Sawa kuna meli ilitoka Algeria na kutia Nanga bandari Salama ambayo inasadikiwa kuwa na siraha ambazo zilisaidia katika mapinduzi ya Zanzibar na ilipokelewa na Oscar Kambona.

NB:Hili ni nje na mada nimeandika baada ya kuona uhusiano wa karibu Kati ya Tanzania na Algeria.
 
Makai makuu ya PLO yalikuwa wapi Dar es salaam- Sinza Palestina,??
 
Anhaa kwahiyo Iddi Amini kuwasaidia wapalestina, ndiyo iwe chanzo cha PLO kuwasaidia kuishambulia Tanzania ?
Awali Amin alikuwa na urafiki na Israel na walikiwa wanampa silaha.Lakini kuna kipindi wakataaa kumpa silaha.Amin akasirika akaanza kuwaunga mkono wapalestina ila kumkomoa Israel
 
Awali Amin alikuwa na urafiki na Israel na walikiwa wanampa silaha.Lakini kuna kipindi wakataaa kumpa silaha.Amin akasirika akaanza kuwaunga mkono wapalestina ila kumkomoa Israel
Siyo tu kumpa silaha, Israel ndiyo walimpa pia mafunzo ya kijeshi Bwana Idd Amin hadi akawa askari wa mwamvuli (Paratrooper). Tatizo ni kwamba mwaka 1971-1972, alipotaka kuvamia Tanzania, akaomba silaha nchini Israel, Wayahudi kwasababu walikuwa na mahusiano mazuri na Tanzania wakakataa. Idd Amin akachukia akageukia kwa wakina Muammar Ghaddafi ambao walimuahidi silaha za kutosha.

Jambo ambalo linashangaza ni kwamba, Israel walikataa kumpa Idd Amin silaha kwasababu walikuwa na mahusiano mazuri na Tanzania. Lakini PLO walikubali kumsaidia Idd Amin mbali na kwamba Tanzania alikuwa ni mshirika wao mzuri. Yaani WAZAYUNI waliwashinda kabisa PLO kwenye suala zima la diplomasia na uungwana.​
 
Kwanini walipinduliwa kama unafikiri hao walikuwa sahihi
 
Ni kweli kabisa, Idd Amin na yeye pia alikuwa mtetezi mkubwa wa Palestina, yaweza kua ndio sababu
Iddi Amin alikuwa ni rafiki wa wayahudi, hadi elimu yake ya kijeshi walimpa wao ila baadaye wakagombana.
Iddi Amin alikuwa ni kibaraka wa Waingereza, hadi vita ya Mau-Mau alikuwa yuko upande wa Waingereza, KAR.
Huo utetezi wa Iddi Amini kwa wapalestina ni kuteka ndege ya iliyojaa raia wasio na hatia ili kuwasaidia PLO ?​
 
Israel walikuwa na mahusiano mazuri vip na Tz wakati Nyerere alikuwa akiwapinga? Hata mahusiano ya kibalozi kati ya Tz na Israel kulikuwa hakuna?
 
Israel walikuwa na mahusiano mazuri vip na Tz wakati Nyerere alikuwa akiwapinga? Hata mahusiano ya kibalozi kati ya Tz na Israel kulikuwa hakuna?
Tanzania na Israel mahusiano yamevunjika mwaka 1973 baada ya vita vya Yom Kippur, kabla ya hapo tulikuwa tunashirikiana vizuri tu. Israel ndiyo waliisaidia Tanzania kuanzisha, The National Service a.k.a JKT, pamoja na kufundisha maafisa wengi wa jeshi la Tanzania.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…