Kwanini wapinzani wanapenda kutumia media za nje kuzungumzia mambo yetu ‘ya ndani’?

Kwanini wapinzani wanapenda kutumia media za nje kuzungumzia mambo yetu ‘ya ndani’?

johnthebaptist,

Media gani ya ndani itaweza ruhusu?! Unataka wafungiwe!? JANA TU HAPA ALIPOANZA KUONGEA LISU WENGINE WAKATOA SAUTI! Yanayoendelea juu ya vyombo vya habari vya ndani ndo yanafanya wapinzani waende nje.

Na nikurekebishe kidogo hiyo sentensi yako ya mwisho!! MAENDELEO YANA VYAMA.. SI UMESIKIA ALICHOONGEA JPM KULE KILWA KUHUSU BWEGE!? Si aliwaambia wabaki na Bwege wao!?
 
Katika ulimwengu huu tuliopo wa kiteknolojia, hakuna sababu ya msingi ya kumkosoa mtu kwa kutumia media za nje kuzungumzia mambo ya "ndani" ya nchi yake unless nchi hiyo haina uhuru unaopasa wa vyombo vya habari.

Kama Twitter tu ni media ya nje kwa nchi mbalimbali lakini viongozi mbalimbali ulimwenguni wamekuwa wakiitumia kuzungumzia mambo mengi tu ya nchi zao tena hata hayo ya "ndani" unayoyasema.
 
johnthebaptist,

Mbatizaji hujaangalia ITV jana wakati ‘Nelson Mandela’ akitoa maneno machache ya salamu kule ACT-Wazalendo?! Pia, kisumbusi chako hakina Chanel za njee?!! Mwisho; Kenya ni wenzetu, John, acha ubaguzi!!
 
Umeshawahi kuona tbc mali ya uma wakirusha matangazo ya elimu ya uraia angalau kuonyesha vyama vya upinzani vilipotoka mpaka vilipo sasa? Je TBC wamewahi kuzungumzia mijadala ya tume huru ili kulinda Amani yetu? Je uliwahi kuona mijadala ya wazi namna ya elimu yetu ilivo duni?
 
Umeamua kupost hii ili kutusanifu au unamaanisha kweli??

Media gani Mkubwa ya ndani iliyo na guts za kumwendea Tundu Lissu na kufanya naye mahojiano kuelezea SERA na MIPANGO yake kama akiwa Rais?

Ni mwandishi gani wa "Tanzania ya Kidikteta ya Magufuli " wa TV ama Redio anaweza kuwa "hajipendi" amuulize Tundu Lissu maswali kama aliyoulizwa na KTN na Majibu take kisha chombo chake na yeye mwenyewe visiweze kula "ban" kwa "uchochezi??"
KTN sio solution kisiasa kalikoroga kacheza wrong pass at a wrong time.
 
Haya mapinzani ya hoovyo kabisa,
Mwl. Nyerere alituachia legacy ya uzalendo kwanza.

Haya mapinzani yametanguliza pesa kuliko utu wetu

Uzalendo wa kubana sehemu moja? Nyerere aliheshimu kushindana kwa hoja, sio mashindano ya kutumia dola kukandamiza wengine
 
johnthebaptist,

Media za ndani zinatakiwa kumsifia "MWANAKIJIJI" ambaye kwa miaka mingi alikosa sifa kwa kuwa hakuwa na mamlaka. Sasa anayo, watamjuaje anayo Mamlaka kama media zikitumiwa kumkosoa!!?
 
Kwani kuna media yoyote ya ndani inayoweza kumpa mtu coverage kama mtu huyo hazungumzi maneno ya kumsifu Rais?

Media zote za ndani ama kwa woga au unagiki, hawataki kuripoti chochote cha vyama vya upinzani. Wanaalikwa kwenye mikutano, hata kwenda tu wanaogopa! Halafu utegemee waongee na wapinzani?

Hakuna awamu ambayo imeua haki za maoni ya watu kama hii. Nadhani itabakia kwenye kumbukumbu za Taifa kwa miaka mingi. Awamu hii imejaribu sana kutaka kuendesha nchi kidikteta. Cha kushukuru ni uwepo wa jamii ya kimataifa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
johnthebaptist,

Mkuu nilikuwa nakuona ni mmoja ya wanajamii magreat thinker. Sasa ulitaka watumie vyombo vya habari vya wakati vimebanwa na serikali hili swali lako hata ukimuuliza mtoto wa form one anakujibu
 
Tunajenga nchi moja lazima tuwe wamoja,
Wakizuka wasaliti na wahuni wachache kuwashughulikia hakuepukiki.
Uzalendo wa kubana sehemu moja? Nyerere aliheshimu kushindana kwa hoja, sio mashindano ya kutumia dola kukandamiza wengine
 
Mbatizaji hujaangalia ITV jana wakati ‘Nelson Mandela’ akitoa maneno machache ya salamu kule ACT-Wazalendo?! Pia, kisumbusi chako hakina Chanel za njee?!! Mwisho; Kenya ni wenzetu, John, acha ubaguzi!!
Nimekuelewa bwashee!
 
Mkuu nilikuwa nakuona ni mmoja ya wanajamii magreat theanger kumbe ni kilaza sijapata kuona sasa ulitaka watumie vyombo vya habari vya wakati vimebanwa na serikali hili swali lako hata ukimuuliza mtoto wa form one anakujibu
Vyombo gani vimebana.....Lisu na Zitto jana walikuwa mubashara ITV au unazungumzia vyombo gani bwashee?
 
johnthebaptist,

Kenya kwasasa nadhani wanataka kuingilia uchaguzi wetu na ikijulikana hivyo sisi tusiogope kuwarudishia fadhila 2022.
 
Back
Top Bottom