Kwanini wapinzani wanapenda kutumia media za nje kuzungumzia mambo yetu ‘ya ndani’?

Kwanini wapinzani wanapenda kutumia media za nje kuzungumzia mambo yetu ‘ya ndani’?

Sasa imekuwa kama imehalalishwa vile kwa viongozi wa upinzani kuvikacha vyombo vya habari vya ndani na kukimbilia media za nje na za washindani wetu wa kiuchumi.

Alianza Zitto na zile fedha za kusaidia elimu ya watoto wa kike lakini kwa bahati nzuri WB wakamshushua na kumpuuza. Zitto aliitumia BBC badala ya media za ndani.

Sasa Tundu Lisu naye anayarudia makosa yaleyale, hivi kwanini mnakwepa media zetu?

Inakera sana.

Maendeleo hayana vyama!
Ukiona hivyo ujue wewe una hitilafu ambayo hutaki kuikubali.
 
Wewe utakuwa. MNYARWANDA ndo maana umeposti huu UHARO. Ni mgeni kiasi kwamba you know nothing about most of TANZANIAN mass media. KANYE V.I.MA haraka 😂😂🤣🤣
Mbona jana ACT wazalendo walikuwa mubashara ITV?
 
Hu
Watakuwaje wajinga wakati elimu ni bure.
Fanya kazi achana na mambo yakwenda kwa wazungu kujidhalilisha
Huwezi kuzuia wazungu kukutawala.hata apo ulipo mpaka chupi ya mkeo ni made in britain.chungulia uioine
 
Media za ndani haziko huru kurusha mambo ya wapinzani isipokuwa kwa mambo ya kusifu na kuabudu mambo ya CCM na mkuu wao.
 
Mexicana, siku hizi kila ndege ikitoka kwa Wazungu na kutua KIA, mh. Waziri wetu wa utalii anatupa taarifa ya idadi ya wazungu!! Wazungu ni wazuri kuliko ‘WAJUMBE’!
Wazungu wale wanajua Kiswahili kuliko wenyeji wao mpaka mtangazaji wa media mashughuri nchini aliyekuwa kwenye mapokezi akajiuliza kwa sauti kama ni Wachaga. Kunani kila ndege kutoka kwa mabeberu ikitua KIA viongozi wetu na Media wanakuwepo kuwapokea wasafiri kwa mbwembwe?
 
johnthebaptist,

Kwani CCM yako imezuiliwa na Mtu yoyote Kuvitumia vyombo vya Habari hivyo hivyo vya nje (Kimataifa) katika Kujitangaza na Kujiimarisha pia?
 
johnthebaptist,

Pengine ndiko wanakopewa platform ya kuongea. Lakini kusikika nje ya mipaka ni pendezo la pande zote

Mungu Ibariki Tz - MITz
 
Back
Top Bottom