Kwanini waraka wa kisheria unaomkataza mwajiri kuingiza makato ya vyama viwili vya wafanyakazi kwa mpigo bila ridhaa ya mtumishi,hauheshimiwi?

Serikali yafukuza kazi walimu wote waliogoma - CWT yafanya majadiliano na serikali kuwaonea huruma walimu hao - Serikali yafuta nia yake ya kuwafukuza kazi : Hapo sasa ndio mfano wa majadiliano, chama chenye wanachama wengi kimezungumza kwa niaba ya walimu wote hata wasio wanachama, hapo kitaomba ada ya uwakala.

Hakuna mjadala unaofanyika zaidi ya viongozi wa CWT kupinduana na kushtakiana mahakamani, wanaanzaje kukata ada ya uwakala.

Hukumu ya CMA kigoma ilisema kitu ambacho ndio hiki tunachokisema kuwa walimu wale sio wanachama wa CWT lakini watakatwa ada ya uwakala (pale itapohitajika), sio kuwa watakatwa kila mwezi.

Huwezi kukata tamaa kuwa mwajiri hawezi kushtakiwa kwa kuwa atapendelewa, unaangalia zama na nyakati. Zitto alifungua kesi dhidi ya Rais kwa kumuondoa CAG pasipo kufuata taratibu, akaona JPM anaikontroo mahakama, akaiondoa kesi yeye mwenyewe Zitto na akairudisha tena baada ya Samia kuwa Rais na ameshinda kesi hiyo. Kwa hiyo wewe peleka tu huko PSC kajenge hoja yajo wakikataa wataeleza ni kwa nini wamekataa, usiogope kuchukua hatua.
 
Nadhani hicho unachokisema kitawezekana Kama Watumishi watakuwa na umoja tofauti nje ya TUCTA.

Na Hilo la hukumu ya Zitto ni siasa tu zimepigwa, HAKUNA Cha maana hapo.
 
Nadhani hicho unachokisema kitawezekana Kama Watumishi watakuwa na umoja tofauti nje ya TUCTA.

Na Hilo la hukumu ya Zitto ni siasa tu zimepigwa, HAKUNA Cha maana hapo.
Kwenye mambo ya ajira hatufanyi kwa kushirikiana - unachukua hatua wewe mwenyewe bila kujali wengine wanasema nini
 
Kwenye mambo ya ajira hatufanyi kwa kushirikiana - unachukua hatua wewe mwenyewe bila kujali wengine wanasema nini
Mtu mmoja ni ngumu kufanikiwa kulingana na system ilivyo, unless uwe huna Cha kupoteza.

Njia rahisi na less risk Kama ninwewe mwenyewe, ni kuhonga tu Afisa Utumishi akuondoe kwenye Makato. Basi
 
Ni hiari Kujiunga na chama Cha wafanyakazi ila ni LAZIMA kukatwa mshahara kwenda kwa chama Cha wafanyakazi.

Loophole hiyo ipo kwenye Sheria ya Ajira na mahusiano kazini, 2004.
Weka kifungu mkuu,naona Kuna mfanyakazi alikataa mshahara wake kukatwa na hakatwi.Hiyo ya lazima tunaomba kifungu ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…