sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,474
- 6,195
Serikali yafukuza kazi walimu wote waliogoma - CWT yafanya majadiliano na serikali kuwaonea huruma walimu hao - Serikali yafuta nia yake ya kuwafukuza kazi : Hapo sasa ndio mfano wa majadiliano, chama chenye wanachama wengi kimezungumza kwa niaba ya walimu wote hata wasio wanachama, hapo kitaomba ada ya uwakala.Sababu inayotumika siku zote ni moja, na ipo kwenye sheria.
"Ikitokea katika eneo lako la kazi at least Nusu ya wafanyakazi ni wanachama wa chama Cha wafanyakazi, then Chama kinazungumza na Mwajiri kwaajili ya kukata hiyo ADA YA UWAKALA"
Note: Mwajiri=Chama Cha wafanyakazi ni YALE YALE.
Hayo majadiliano anafanya NANI na NANI?
Unamshtaki Mwajiri wapi huko unakohisi utatendewa HAKI ???
Iwe CMA au PSC HAKUNA Cha maana utapata. Nimekuwekea taarifa ya hukumu ya walimu 347 kutoka CMA umeona??
Kitu pekee unachoweza kufanya labda mchongo tu, uongee na Afisa Utumishi binafsi akutoe.
Lakini as long as Sheria ya Ajira itabaki kuwa Kama ilivyo HAKUNA pa kutokea.
Hakuna mjadala unaofanyika zaidi ya viongozi wa CWT kupinduana na kushtakiana mahakamani, wanaanzaje kukata ada ya uwakala.
Hukumu ya CMA kigoma ilisema kitu ambacho ndio hiki tunachokisema kuwa walimu wale sio wanachama wa CWT lakini watakatwa ada ya uwakala (pale itapohitajika), sio kuwa watakatwa kila mwezi.
Huwezi kukata tamaa kuwa mwajiri hawezi kushtakiwa kwa kuwa atapendelewa, unaangalia zama na nyakati. Zitto alifungua kesi dhidi ya Rais kwa kumuondoa CAG pasipo kufuata taratibu, akaona JPM anaikontroo mahakama, akaiondoa kesi yeye mwenyewe Zitto na akairudisha tena baada ya Samia kuwa Rais na ameshinda kesi hiyo. Kwa hiyo wewe peleka tu huko PSC kajenge hoja yajo wakikataa wataeleza ni kwa nini wamekataa, usiogope kuchukua hatua.