Kwanini Wasabato Wanatengwa kwenye Shughuli za Kitaifa?

Kwanini Wasabato Wanatengwa kwenye Shughuli za Kitaifa?

Boss la DP World

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
2,318
Reaction score
8,464
Nijuavyo mimi, katika nchi hii wapo watu ambao huabudu siku za Ijumaa, wengine Jumamosi na wengine Jumapili.

Ukifuatilia mikutano mingi ya kisiasa utagundua wanaopewa kipaumbele ni Wanaoswali siku ya Ijumaa na wanaosali siku ya Jumapili. Wanaosali jumamosi nimewahi kuona kama mara 2 hivi kipindi cha JPM waliwahi kupata nafasi ya kutoa sala.

Napenda kujua, ni kwanini?

Maana hata kwenye televisheni ya taifa ni mwaka jana ndiyo walianza kutoa airtime ya nusu saa kwa wanaoabudu siku ya Jumamosi kama inavyotoa kwa madehebu mengine siku ya Jumapili na kwa Wengine Ijumaa.

Wajuzi wa mambo nijuzeni kuhusu hili.
 
Napenda kujua ni kwanini?
Maana hata kwenye televisheni ya taifa ni mwaka jana ndiyo walianza kutoa airtime ya nusu saa kwa wanaoabudu siku ya Jumamosi kama inavyotoa kwa madehebu mengine siku ya Jumapili na kwa Wengine Ijumaa.

Wajuzi wa mambo nijuzeni kuhusu hili.
Kila dhehebu likitaka hivi itakuwa tafrani.
 
Hawana unafiki wao nyeupe ni nyeupe

Wengine wasaka tonge tu
Dini na siasa wapi na wapi kama sio kujipendekeza?
Hayo ni mawazo yangu maana naona wengi wanasifia mpaka wanasahau kuomba Mungu wanamtukuza Rais au kiongozi mkubwa
 
Hao wanashirikishwa wamenufaika ama wamesaidia nini?
 
Wasabato ni dhehebu la watu makini sana sio wapiga vizinga wala makanisa yao hayanaga michango ya hovyo hovyo kama hayo madhehebu ya watenda miuniza mi nawakubali sana sana
Na waumini wake ni akina Mzee wetu Wasira et al, yani watu makini kabisa. Hakuna kutoa sadaka kabisa, sijui kanisa linaendeshwa kwa fund gani
 
Na waumini wake ni akina Mzee wetu Wasira et al, yani watu makini kabisa. Hakuna kutoa sadaka kabisa, sijui kanisa linaendeshwa kwa fund gani
Sadaka wanatoa, nimewahi kusali kwao ila wako well organized, ukitoa hata 100 unapewa risiti.
 
Kuna dini nyingi zinabaguliwa kwenye shughuli za kiserikali, Anza na dini za jadi ambazo waumini wake ni wengi. Ubaguzi huu unaenda pia kwenye preferential treatment kwenye ulipaji wa Kodi. Nafikiri hii siyo sawa. Jamii ibadilike
 
Back
Top Bottom