tamsana
JF-Expert Member
- Jan 13, 2012
- 3,739
- 8,044
Sawa mkuu.Sadaka wanatoa, nimewahi kusali kwao ila wako well organized, ukitoa hata 100 unapewa risiti.
Huo ndio utaratibu wao, sasa kanisani tuko zaidi ya 1500 tuanze kupeana risiti za nini kwenye sadaka.
Ambacho kinafanyika ninapoabudu mimi ni kuwa michango yote pamoja na zaka ndio ukitoa unapata risiti yako.
Kwenye sadaka kibinafsi ukifahamu maana ya utoaji wala hautakuwa na hila moyoni mwako. Hata biblia inatufundisha kutoa kwa moyo wa kupenda.
Zama za sasa hatutoi kwa moyo wa kupenda kwa sababu hatuamini tunamtolea nani.
Nadhani kila dhehebu liwekeka utaratibu wake ambao wameona unawafaa. Hivyo si busara kuwahukumu wengine kwa kutoweka utaratibu sawa na ule unaofanyika sehemu unakoabudu.