Kwanini Wasichana wengi wanaona wana haki ya kupewa Salamu na sio kutoa?

Kwanini Wasichana wengi wanaona wana haki ya kupewa Salamu na sio kutoa?

Ilo kweli boss maana wamama wanatoa salamu hatari😀😀ila masister aka slay queens duh

Iko hivyo, hata wanawake wenyewe wakimuona binti anaringa utasikia wakisema subiri apate mimba mbona nyodo zitaisha😊😊
 
Ivi Kwanini? Wasichana Wengi Uwa Wanajiona Wana Haki ya Kupewa Salamu na Sio Kutoa?


Habarini wanajamii Forums nimekuwa na kitu kinanishangaza sana tangu utoto hadi sasa kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu , imekuwa kawaida kwa jamii ya kiafrica mvulana kumshobokea mtoto wa kike yaani kuanza kumpa salamu ata kama kakukuta sehemu , maana navyojua mtu anapokukuta sehemu yeye ndo anatakiwa kukupa salamu na sio yeye afike na kukaa kimya kisha wewe ndo umpe salamu

Hii kitu nimeishuhudia mara kwa mara tangu nizaliwe hadi sasa , hii kitu imekuwa ikinikuta mara kwa mara labda nipo kwenye bus naenda mkoa fulani nimekaa zangu kwenye seat anakuja msichana seat ya pembeni yangu anafika na kukaa bila ata salamu aisee uwa nashindwa kumuanza kumsalimia au kwa kumuonea aibu nampa hi halafu nakausha, hii ishu pia kwenye usafiri wa umma uwa inatokea unakuta nimewahi nimekaa zangu ndani ya gari mara anaingia sister duh anakuja anakaa pembeni yangu kimya kimya ata asalimii uwa sijui namuonaje kuna muda uwa napiga kimya hadi safari napoishia maana uwa naona kumshobokea mtu kumsalimia aliyekukuta ni kuuaibisha ukoo wangu na mimi pia.

Sijui kwa wengine kama hii hali wanaishuhudia ila nimekuwa naishuhudia ata mitaani na vyuoni ni ivyo ivyo binti anaweza kuwakuta mmekaa na asiwasalimie au akasalimia kwa majina kadhaa na sio wote [emoji3][emoji3]sijui uwa ni kitu gani kinawasumbua, ila kwa mimi nachoamini iyo ni tabia iliyojengeka kwao kutokana na wavulana tunavyowatreat wasichana tunajishusha sana mbele ya wasichana hadi wanatudharau na wanaona wana haki ya kila kitu kutoka kwetu hadi salamu [emoji3][emoji3]

Ningependa kusikia maoni ya wasichana na wanaume kuhusu ili suala ...
Sina tabia hiyo, awe mwanamke, awe mrembo, awe mmama au mzee akinikuta asipo salimia nampotezea wala simsemeshi wala kumsalimia
 
Leo npo kwny mwendokasi, nmekaa. Kaja pisi kali kakaa seat ya pemben bila kunisalimia akadhan ntamshobokea. Ihiiiiiiiii ndo kwanza nkageukia pembeni.

Mimi hata nkiwa barabaran hua sisalimii madem hata sku moja mana wanajiona cake

Kuna dem humu nshawai mfata PM namwomba namba, akawa hajibu message, akidhan ntambembeleza,, Ihiiiiiiiiiii ndo kwaaaaanza nkafuta hlo wazo la kutaka namba zake
 
kwa kawaida wasichana walio wengi wanajisikia, na ndio sababu pia utaona hata walioko kwenye sehemu za kutoa huduma wana "customer care" mbaya! ila muda ndio kila kitu, wanafanya yote hayo na kuolewa hawaolewi siku hizi kwasababu pia wanapishana na wanaume wenye hekima.
 
Wakulungwa mkipewa salamu huwa haiishi, mnaelekea kwenye namba😃😃.

Hata hivyo hii kawaida tumeitengeneza sisi wanaume, ile kushoboka sana na pisi.

Binafsi mwanamke akianza yeye kunipa salam huwa nampa heko sana, namuana ni shupavu na anajiamini , anajitambua pia.
 
Wakaka weupe ndo kiboko ya madem utasikia "ooh siwapendi wakaka weupe wanajishaua" [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] wanataka kutumudu wanaume wote ila weupe wamegoma.
 
Sipendi watu wanaopenda penda salamu utadhani chakula khaa hadi kwenye daldala napo unataka usalimiwe,utasalimiwa na wangapi sasa na utasalimia wangapi maana wanaingia na kutoka. Tafuteni pesa wakuu muache kujali vitu vidogo vidogo
Huko umeenda mbali.

Mantiki ya mtoa mada anamaanisha wanawake mnajichukulia haki ya kuanza kusalimiwa kuwa ni yenu tu.

Hata mkikutana na mwanaume mkawa wawili tu, wewe unajithamanisha na kujipandisha wadhifa, mpaka jamaa akuanze wewe.

Ndiyo hiyo sababu ya kujithamanisha kwenu inatafutwa.
 
Dah nilikuwa nadhani ni mimi tu ndo yananisibu na hivi vitoto vya chuo kwa hii sura yangu ya kazi! Ngoja nianze kuvilia bati sasa
 
Ninapokaa mimi niko na mambo yangu kuna wadada wamepanga basi huwa siwasalimii nikitoka niko na mishe zangu siku hyo natoka nje kuna kama kakona nikajibanza nikasikia wananisema huyu kaka hata hasalimii


Nikarudi niliwaashia moto nikawaambia salamu hailazimishwi wakawa kimya kama maji kwenye mtungi
 
Huwa sisalimii maslay queen kabisa hasa njiani,,

Leo nimeingia ofisi fulani nimekuta wasichana wengi wanaogopa kuingia Kwenye ofisi ninayoenda mimi nikapita katikati yao nikaingia ofisini nilivotoka wakanisalimia wenyewe kwa heshima na kuomba utaratibu bila hiyana nikaelekeza nikapita zangu.
Mkuu ulikosoa ungemchagua mmoja wapo mzuri uchukue No yake unitumie mimi ndugu yako
 
Wasichana/wanawake wanaofanya kazi taasisi za kifedha, hasa benki wanaweza kuwa wanaongoza kwa kiburi cha kutosalimia.......... Wengi wanajiona wameyapatia maisha..... they are so stupid!
I rest my case! Nimetupa jiwe gizani. Nasubiri atakayegugumia kwa maumivu, ili nimjue niliyemtungua.......
Unakuta mshahara wao hauzidi 1million kwa Mwenzi anasumbua sana
Bank nyingi zina viyoyozi vinawafanya wanakuwa soft sana
 
Back
Top Bottom