Kwanini Waswahili hatuwezi kwenda na muda?

Sio kwamba hatuheshimu muda,tunacheleweshwa na factors mbalimbali.
Inawezekanaje tumepanga kukutana watu 15, wote mcheleweshwe na factors mbalimbali, yaani hakuna hata mmoja alieweza kufika on time
 
Ni uzembe tu..
Tuna vijana wana ufanisi mkubwa kwenye baadhi ya taaluma..lakin hawajui kwenda na muda...siku za kazi mara zote wanakuja kwa kuchelewa...anatakiwa akamilishe kazi baada ya siku 3..anamaliza week.

Halafu ni uzembe mkubwa sana tunao, kuna kupata dharura..lakin unakuta mtu hatoi taarifa anakaa kimya,anakuja kwa kuchelewa na hata kazi mshamaliza ndio anaanza kukulete blah, blah zake..

Hii time management imenikoseshana na watu wengi sana...mtu anakwambia baada ya nusu saa nitakua hapo,anza kutoka kabisa.bhasi unakula ka ugali kako mbio mbio afu ukute ka moto yani unakapuliza uli hata kwa raha,unafika mapema unakaa hata saa zima mtu hatokei,ukipiga anapokea anamkwambia nafika sasa hivi..nusu saa ingine..

Siku hizi nasubiri dk 10 usipotokea nasepa.

Inakwaza ndio mana naona fursa nyingi zinakuja kamatwa na wageni.

Sent from my SM-G975U using JamiiForums mobile app
Inakera sana waafrika inabidi tubadilike. Watu wasomi, wana masimu na masaa makubwa mikononi wamevaa ila kufika mahali kwa wakati hawawezi!
 
Hata discussion za chuoni mnazokaa hostel watu wanachelewa hahahah, kwenye ibada za jumuia watu wanachelewa,
Kwenye vikao vya shule ya msingi wanachelewa,

Hivyo vyote usafiri ni wew tu kuchanganya matako vizuri 😂😂😂
Wengi hawana usafiri bongo, miundo mbinu mibovu, maeneo wanayokaa wabongo wengi ni chokoromageni hayo ni baadhi ya matatizo makubwa mengine watajazia... halafu mtoa mada acha ushamba na uzumbukuku utafikiri ulizaliwa ulaya.. kwani ulizaliwa ndani ya muda?
 
Kikubwa tubadilike muda ni Mali.
 
Tunakubaliana kabisa, jamani eeh kesho tukutane saa tatu kamili asubuhi. Watu wote wanaitikia "Sawa, saa tatu imekaa vizuri kabisa!"

Wewe unawahi saa tatu kasoro dakika 5 unafika eneo la tukio unakuta hakuna mtu hata mmoja. Unaanza kusubiri... saa tatu kamili, saa tatu na dakika 10, saa tatu na nusu.... saa nne!

Ndio watu wanaanza kujitokeza mmoja mmoja huku ikijichekesha chekesha "Ooh unajua bana mambo mengi asubuhi..." Sasa si mngesema tukutane saa nane?

Hivi kweli Waafrika tutaweza mambo serious kama swala la muda tu linatushinda!
Hilo swala linaanzia kwenye malezi. Haya mengine ni sababu tu
 
Tunakubaliana kabisa, jamani eeh kesho tukutane saa tatu kamili asubuhi. Watu wote wanaitikia "Sawa, saa tatu imekaa vizuri kabisa!"

Wewe unawahi saa tatu kasoro dakika 5 unafika eneo la tukio unakuta hakuna mtu hata mmoja. Unaanza kusubiri... saa tatu kamili, saa tatu na dakika 10, saa tatu na nusu.... saa nne!

Ndio watu wanaanza kujitokeza mmoja mmoja huku ikijichekesha chekesha "Ooh unajua bana mambo mengi asubuhi..." Sasa si mngesema tukutane saa nane?

Hivi kweli Waafrika tutaweza mambo serious kama swala la muda tu linatushinda!
Hatutaweza na hatujawahi kuwa serious, sio viongozi wala wanaoongozwa

Watu weusi ni Wapuuzaji wa vitu vya muhimu
 
Tunakubaliana kabisa, jamani eeh kesho tukutane saa tatu kamili asubuhi. Watu wote wanaitikia "Sawa, saa tatu imekaa vizuri kabisa!"

Wewe unawahi saa tatu kasoro dakika 5 unafika eneo la tukio unakuta hakuna mtu hata mmoja. Unaanza kusubiri... saa tatu kamili, saa tatu na dakika 10, saa tatu na nusu.... saa nne!

Ndio watu wanaanza kujitokeza mmoja mmoja huku ikijichekesha chekesha "Ooh unajua bana mambo mengi asubuhi..." Sasa si mngesema tukutane saa nane?

Hivi kweli Waafrika tutaweza mambo serious kama swala la muda tu linatushinda!
Wewe mbona pia hujaenda na muda, mmekubaliana saa 3 unaenda saa 2 na dakika 50 huko?
 
Tunakubaliana kabisa, jamani eeh kesho tukutane saa tatu kamili asubuhi. Watu wote wanaitikia "Sawa, saa tatu imekaa vizuri kabisa!"

Wewe unawahi saa tatu kasoro dakika 5 unafika eneo la tukio unakuta hakuna mtu hata mmoja. Unaanza kusubiri... saa tatu kamili, saa tatu na dakika 10, saa tatu na nusu.... saa nne!

Ndio watu wanaanza kujitokeza mmoja mmoja huku ikijichekesha chekesha "Ooh unajua bana mambo mengi asubuhi..." Sasa si mngesema tukutane saa nane?

Hivi kweli Waafrika tutaweza mambo serious kama swala la muda tu linatushinda!
kitendo cha kuzaliwa bongo tayari umechelewa
 
Inawezekanaje tumepanga kukutana watu 15, wote mcheleweshwe na factors mbalimbali, yaani hakuna hata mmoja alieweza kufika on time
Mkuu ndo ishakuwa tamaduni, watu watatafuta sababu za kuhalalisha tu lakini kiukweli kabsaaa hakuna sababu zaidi ya mazoea na udhembe na Mimi nikijiweka japo najitahidi 😁

Hakuna mtu ambaye hajui anaishi mbali au kuna jams muda flani, ila ni makusudi kabsaa kujichelewesha ili kuepuka kusubiri wenzio kama utafika on time. Ni tabia mbovu ila tumeikubali
 
Sasa mbona unawalaumu wenzako hali ya kuwa wote hamkuwa ndani ya muda??

Jaribu kufikiri kuna sehemu mnatakiwa kufika ndani ya muda fulani kwa pamoja ,wewe ukajitia kihere here kuwahi ina maanisha hapo umewachoma wenzako hata kama kungekuwa na adui angeweza kukudhuru kiurahisi maana muda huo utakuwa upo peke yako.
 
Mimi mwenyewe nimeanza kujitahidi kujichelewesha ili nisikasirike lakini bado hata nikijichelewesha najikuta nimewahi kuliko wenzangu na nalazimika kukasirika.
 
Mimi nawalaumu kwa kuchelewa, wao pia wanaruhusiwa kunilaumu kwa kuwahi.
 
Mimi mwenyewe nimeanza kujitahidi kujichelewesha ili nisikasirike lakini bado hata nikijichelewesha najikuta nimewahi kuliko wenzangu na nalazimika kukasirika.
Mkuu ukiwa hivyo utapata stress, ichukulie kama tamaduni ya watu, fika mapema tulia, do you mkuu lakini usitaraji wengine wawe kama wewe

Mimi kiukweli nilikuwa concious na muda sana lakini baadae nikajua kuitaraji hiyo iwe the same kwa watu wengine ni kujiumiza akili buree, kwa hiyo huwa najitahidi kuwajua watu kitabia lakini pia kupima umuhimu wa meeting yenyewe ili nibaki kwa safe side
 
Muda wenyewe umekaa kizungu
07: 45 am mnasema saa mbili kasorobo
 
Back
Top Bottom