Afadhali sana Clouds, lakini Efm na Wasafi ndio hovyo kabisa. Na ishu sio kuwa ni mashabiki wa Simba au yanga. Tatizo waliopo kwenye hivyo vipindi ni wahuni, wanaletra stori za vijiweni. Vipindi havina mpangilio yaani watu wanazungumza habari za vijiwe vya bia mara nimetumiwa sms sijui huyu kafanya hiki. Yaani vipindi haviandaliwi. Watu wanakuja studio na vikaptula tu na kuanza kuongea utumbo. Na vilevile hutumiwa na hivi vilabu viwili ili kuvurugana kisaikolojia. Na hiyo mbinu ndio wanaitumia sana yanga sasa hivi. Inawalipa hawa waganga njaa na kuanza kuposti na kuongelea habari za kuwaongelea vibaya Simba ili kuwachanganya. Kuendelea kuumia kichwa kwa habari wanazoongea hawa wajinga, ni kujitesa tu.