steveson manumbu
JF-Expert Member
- Apr 1, 2014
- 887
- 178
uliza swali ujibiwe mkuu, hapa hakuna mtu anayeuza ujuzi, na hakunamtu mwenye maslahi na alibaba!
uliza swali ujibiwe mkuu, hapa hakuna mtu anayeuza ujuzi, na hakunamtu mwenye maslahi na alibaba!
Hv mkuu kuna uhusiano wowote kati ya Alibaba na Aliexpress?au ni kama Ebay na Amazon?
hapo hakuna shaka mkuu zaidi nyie ndo wenye maujuzi hivyo ni vema ukatabainisha vizuri mkuu
zote ziko chini ya kampuni moja, alibaba kule wamejazana manufacturer, wholesalers, na traders wanaouza mzigo jumla, japo wapo wanaouza rejareja pia, aliexpress kule unapata vitu vingi vya retail.
Ahsante sana mkuu,je na hawa Aliexpress umewahi kufanya nao biashara?
ndiyo mkuu, wako vuzuri tu.
We unasemea sample ya laptop?!!!!..we jamaa! naona unaongelea biashara ya rejareja, kwa taarifa yako ya bure tu binafsi nilishapokea sample nyingi sana kuanzia clone za honda motorbikes, box za spare za pikipiki, motor, generator za umeme, matairi ya pikipiki, alibaba imenikutanisha na watu wengi sana, wewe unataka kununua laptop mbili unataka utumiwe sample, wewe si mwizi tu!!!! sikatai kuna matapeli, hakuna market place inayokosa matapeli, kuidiscredit alibaba kwa sababu ya experience yako mbovu na watu fulani ni utovu wa nidhamu tu, ni sawa na mimi nisema "wamarekani hawafai kitu wale, nimenunua cover ya kindle tu mwezi mzima sasa sijaipata"!!! alibaba Watanzania wanauza na kununua kule, watu wanauza asali, vitunguu, ufuta, karanga, msiwakatishe tamaa watu wasiojua mnawatia uwoga usio na msingi. Alibaba ipo na inazidi kukua siku hadi siku, ingekuwa imejaa matapeli kwa jinsi unavoiweka ingekuwa inakufa, badala yake inakua!
SCARED MONEY DON'T MAKE MONEY!
Nimenunua vitu vingi sana mitandaoni sijawahi kutapeliwa...ni MEMBER wa kudumu EBAY, ALIEXPRESS, GOODLUCKBUY,ALIBABA na kote nimenunua kwa kweli taarifa zinazoenezwa kuwa wale jamaa ni wezi ni upuuzi mtupu usiona na ukweli...
japo nimewahi kuagiza device Ebay ikaibiwa posta dar es salaam...wakati ule wa vuguvugu la madawa ya kulevya la Mwakyembe walikuwa wanakagua kila kitu, waliuona ni kitu kizuri ndani yake na wakaiba....
anaetaka maujuzi na uzoefu...ani PM
kwangu nilichojifunza mkuu ni kudhindwa kuchsnganua michanganuo ya hawa waungwana kiasi kwamba inafikia pahala hawatoi suluhu kuwa tufanye nini . tuanzie wapi nk zaidi ya ubababe wa kudhinda
weka link
kiongozi, mimi sitaku PM kwa manufaa ya wadau wengine.. naomba uniambie mchakato mzima mpaka mzigo unakufikia bongo.. in short, shipment options..? mzigo ukifika unaupokelea wapi?
Mkuu hilo ulisemalo sio kweli kabisa.
Usije ukawaponza waTz hapa.
ALIBABA.COM Hawatoi Guarantee yyt kwa Washiriki waliomo humo na makampuni mengi yaliomo humo ALIBABA.COM hayakubali PAYPAL as a source of payments.
Kwa sababu PAYPAL inakuhakikishua Usalama wa Pesa zako.
Wengi wao wanataka utume pesa kwa Moneygram au Western Union.
Na njia hizi zote HAKUNA USALAMA WAPESA ZAKO.
Ukiwaambia utume kwa (LOC) kupitia benki yako ASILIMIA 90% ya makampuni hayo WANAKATAA.
WIZI WENGI MNO kupita WAAMINIFU.
Mwenye kutaka bidhaa CHINA ni bora mara milioni upoteze hio NAULI uende mwenyewe.
Huna lolote wewe.
We utawadanganya watz kuwa ulipewa sampla ya Vitu hivyo bure?
Hebu tuwekee ushahidi hapa km huyo jamaa hapo nyuma wa Waybill yako ya hizo sample.
Hivi wewe na bichwa lako unategemea watz wajinga eti!
Nasema tena, Alibaba WIZI ni wengi kuliko waungwana.
Sasa km umepewa kamisheni kuja kuibia watu humu, hupati mtu.
Mwenye biashara kubwa anakesha Jf akipiga bla bla..?
Huna llt wewe.
Nimeshanunua incubator 8 tokea january 2013 toka kwa Alibaba na sijawahi kukumbana na utapeli wala ubabaishaji wowote,hofu yangu kubwa mwanzoni ilikua ni kwenye ubora,lakini nikaja kugundua hata bidhaa zao ni bora tofauti na porojo tunazopeana Watanzania tusiojua reality!na tukumbuke Alibaba ni among the biggest online commerce company in the world,biashara zao kubwa wanafanya America,Europe na Asia,hapa Tanzania ni kama hakuna watu wenye uelewa juu ya Alibaba(kwa maana ya wachache sana) na tukumbuke kua mwezi june Soko la hisa la New York,waliwashinda Nasdaq katika kuwashawishi Alibaba wawe listed kwenye soko lao la hisa,so utaona ni jinsi gani wenzetu wanavyojua u giant wa Alibaba na u serious wao katika biashara..hizo nyingine za WIZI mkubwa,sijui hv na vile,ni porojo tu za Watanzania tulio wengi tunaopendaga kujiona tunajua mambo kumbe hakuna lolote,kwa mtu alie serious na mwenye uelewa kidogo tu,anaweza google na akaona jinsi Alibaba walivyo serious na wanavyoheshimika kimataifa..tuachene porojo Watanzania,kama jambo ujuhi kaa kimya ujifunze kwa wenzako
Kweli ndg, kuna mambo yanashangaza hapo Alibaba mfano mtu anakwambia Tv Lg org 72 nch atakuuzia kwa usd 110, jamani huu kama si uongo nini? Mimi nimejiunga na huwa nachat nao lakini sina imani nao. Na hawakubali malipo nusu. Waaminifu wapo sema jinsi ya kuwabaini.
Hayo ndio nayasema mkuu.
Wezi wengi kuliko waungwana.
Hebu soma comments za watu kwenye hio Alibaba express uone watu wanavyolalamika.
Halafu wanakuja watu hapa na kukupa Guarantee.
Hawa jamaa ni wa kuwachunga sana.
Na kama ukifanikiwa kutumiwa hio bidhaa ulionunu basi km ni Mobile phones watakupakilia Viatu vya watoto. Au toys za kuchezea.