Mkuu hizi mamlaka husika na serikali ndio wanawafanya Watanzania watafute mbinu za kukwepa kodi na waichukie kodi!mfano TRA wao kodi uwa wanakadiria tu,mimi niliwahi leta mzigo wa $520 walivyo wehu wakakadiria kwa $950 nilibishana nao na nilipoteza siku nane na nika incur cost ambazo sio necessary mwisho wa siku ndio yakaja kukubaliana na gharama ile halisi,ukija kwa Serikali,wao usiku na mchana ni kuwahimiza watu walipe kodi,na kuwapandishia kodi kila budget,lakini mwisho wa siku nchi nchi inaendeshwa kwa misaada inayotugharimu Watanzania,na hata budget kuu ukiangalia,karibu nusu ya budget inaenda kwenye matumizi yao ya kawaida(yasio na tija) na nyingine ndio upelekwa kwenye mambo ya maendeleo,sasa kwa mwendo huu kweli kuna Mtanzania atakaependa kulipa kodi wakati anajua wanao nufaika kwa kiasi kikubwa ni wao wachache?