Kwanini Watanzania hamjiungi na ALIBABA small business website

Mm pia nilinunua, semaTRA walinibambika kodi ya kuua, kitu cha $80 nikalipia kodi TZS 176k , namna gani ya kukabiliana na customs , kidogo nizire kchukua ile item

Mkuu mimi niliagiza HTC ONE X na Huawei Ascend P7 toka kwa sellers wawili tofauti wa Aliexpress na mizigo ilifika tena ikiwa salama na katika good condition?nachojua ni kua,aliexpress unapolipia,pesa yako inakua pending mpaka pale unapopata mzigo wako ndio muuzaji upatiwa pesa,na pia ninachofanya najaribu sana kuangalia huyo seller bidhaa zake alizouza awali ziko rated kiasi gani na prev buyers,buyer protection ambayo ina option za full refund if u dont receive ur order,refund ok keep item as not described!kusema ukweli mimi sijawahi kumbana na tatizo lolote kuanzia,amazon,ebay,alibaba na hata aliexpress,microcentre etc na mimi ni mnunuaji mzuri sana wa mitandaoni
 
Ni kweli mkuu,TRA wana urasimu sana tu,sijui ni kutojua au kukomoana tu,sometime naonaga kama kuna option ya kodi kulipiwa kule na wewe kufika hapa ni kusign na kuchukua mzigo tu,uwa ni nzuri zaidi
 
Wanaoleta ushabiki wa kutoiamini alibaba wakati hawajawahi kuagiza au kununua kitu ndiyo wanaowakosesha fursa watanzania wenzao

Nimejiunga na alibaba kabla hawajawa na Aliexpress year 2002 na tokea halo nimenunua bidhaa na kuunganishwa na biashara nyingi bila usumbufu, utapeli, kadhia na pia kupata bidhaa zenye viwango vizuri pamoja na unafuu wa bei
 
Mkuu mimi niliagiza HTC ONE X na Huawei Ascend P7 toka kwa sellers wawili tofauti wa Aliexpress na mizigo ilifika tena ikiwa salama na katika good condition?nachojua ni kua,aliexpress unapolipia,pesa yako inakua pending mpaka pale unapopata mzigo wako ndio muuzaji upatiwa pesa,na pia ninachofanya najaribu sana kuangalia huyo seller bidhaa zake alizouza awali ziko rated kiasi gani na prev buyers,buyer protection ambayo ina option za full refund if u dont receive ur order,refund ok keep item as not described!kusema ukweli mimi sijawahi kumbana na tatizo lolote kuanzia,amazon,ebay,alibaba na hata aliexpress,microcentre etc na mimi ni mnunuaji mzuri sana wa mitandaoni

Hilo mkuu sijalikataa.
NA Ebay, pamoja na Amazon Wanatoa Guarantee kwa wateja wote kuhusu hao Suppliers kwenye ile policy ya Money back if there is dispute between buyer and seller.

Na kwa hao ALIBABA nadhani items zilizo chini ya $50 kwa retail na ukichungunza excellent rated sellers nadhani nafasi ya kutapeliwa utakuwa umeiPunguza sana.

Lkn mzigo mkubwa ambao unaanzia $5000-$30,000 na kwenda juu. Unatakiwa uwe makini sana sana.

Hakuna Guarantee wanatoa hao admin wa ALIBABA. ispokuwa lzm upitie ESCROW na Hao ni wasumbufu mwisho wa maneno.

Haya yamenikuta mimi binafsi na sina ninachopata kwa kuwatisha watu km sio kweli.

Wachina Asilimia kubwa ni MATAPELI.! na hilo muulize mfanyabiashara yyt yule.

Mtu unakwenda mpaka China mwenyewe na km hauko makini UNATAPELIWA je! Humu kwenye biashara za mitandao Utajihakiki mara zote?

Nadhani watu wanatakiwa kujichunga zaidi kuliko kuamini tu kwa sababu mtu kutoka JF kasema.

Watz ni wahangaikaji wazuri tu, kuwadanganya watu kuwa ALIBABA NI 100% waungwana ni kutaka kuwaponza watu humu na kuwaharibia maisha yao.
 
Hapo nimeipata point yako mkuu,na kwa kweli upo sahihi,kinachotakiwa kwenye hizi biashara za mitandaoni UMAKINI unahitajika sana,kuna vitu muhimu vya kuangalia before haujafanya biashara,mimi feedback za seller toka kwa buyers mara nyingi ndio uwa na consider sana juu ya ubora wa bidhaa ya muuzaji!yote kwa yote biashara ya online ni nzuri sana kama ukiwa MAKINI..tuendelee kuelimishana wakuu bila kua na jazba wala kebehi,sisi wote ni Watanzania na lengo letu wote ni maendeleo yetu binafsi na ya jamii zetu kwa ujumla
 
Kwanza lazima uwe na physical adress ya posta.....(P.o.Box) inayofanya kazi...Jisajili mitandao yote...

Ebay Huwezi kununua mzigo mpaka uwe umejiunga PAYPAL na iwe imrunganishwa na bank yako (hapa benki yako lazima iwe na Mastercards na Visacards) iwe ina support internet Transactions...Ukishajisaliji...Unaweza kununua....

Mitandao km Alibaba,Ali express si lazima uwe PAYPAL unachotakiwa uwe na Mastercard na Visa...unajisajili mtandao wao...then unakuwa secured na Escrow pesa yako haipotei...kamwe...

Goodluck buy

sawa sawa kiongozi.. sasa mzigo unafikafika vipi bongo na unaupokelea wapi?
 
mzigo unaupokea kupitia hilo sanduku lako la posta...kinachotokea posta mzigo ukifika wanaweka notification memo kwenye box we ukiwa umeipata unaenda na ID u nachukua chako...kumbuka mizigo mingi unaweweza kuitrack kuanzia kule unakonunua..yaani kuna option ya ku track mzigo wako movement zake na hii ni "recommended" kuanzia siku uliponunua mpaka unakufikia unaona kila kitu

au unaweza kununua bila kupewa track number...we mwenyewe tu chaguo lako

pia unaweza kuingia - Electronic digital products and spare parts accessories wholesale goodluckbuy.com humo kuna bidhaa nyingi za kielectronic kwa bei chee ila lazima uwe member wa PAYPAL

la msingi hasikutishe mtu kuwa unaibiwa...mitandao hii kwa mimi binafsi nimenunua bidhaa nyingi sana...na ukitaka kukwepa kodi mathalani item uliyonunua ni expensive unaweza kunegotiate na muuzaji akaandika bei kidogo kwenye Invoice...kitu ulichonunua $100 unaweza kuandika $15...:A S wink:

so buy with confidence....
 
jambo lingine jitahidi kuangalia unanunua kwa seller gani? maana kuna wale wanaitwa ''TOP RATED SELLERS" hao ni bora zaidi na kwa sababu wameuza bidhaa nyingi na wana positive feedback kutoka kwa wateja wao...

na kabla hujanunua hakikisha unachotaka kununua ni kitu sahihi...ikiwa mtumaji ametuma kitu with wrong descriptions unaweza kumfungulia kesi humo humo na akarejesha pesa yako...

JIACHIEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.....chukua fursa
 
Mm pia nilinunua, semaTRA walinibambika kodi ya kuua, kitu cha $80 nikalipia kodi TZS 176k , namna gani ya kukabiliana na customs , kidogo nizire kchukua ile item

ngoja nikupe maujanja ...kabla hujanunua ongea na seller kwenye "contact a seller" muombe aandike bei kidogo kwenye invoice ya item...mathalan....kitu chako cha $80 unaweza kuandika $10...:cool2: hasa mitandao ya china au EBAY ukinunua kitu kutoka Hongkong, singapore, korea au China...

usiende kichwa kichwa...una bergain bei ya invoice ipunguzwe akikubali unanunua....nimefanya hayo maujanja kitambo sana....ukijifanya unanunua nunua bila kuomba adanganye kwenye INVOICE...TRA watakuua..
 
mzigo unaupokea kupitia hilo sanduku lako la posta...kinachotokea posta mzigo ukifika wanaweka notification memo kwenye box we ukiwa umeipata unaenda na ID u nachukua chako...kumbuka mizigo mingi unaweweza kuitrack kuanzia kule unakonunua..yaani kuna option ya ku track mzigo wako movement zake na hii ni "recommended" kuanzia siku uliponunua mpaka unakufikia unaona kila kitu

au unaweza kununua bila kupewa track number...we mwenyewe tu chaguo lako

pia unaweza kuingia - Electronic digital products and spare parts accessories wholesale goodluckbuy.com humo kuna bidhaa nyingi za kielectronic kwa bei chee ila lazima uwe member wa PAYPAL

la msingi hasikutishe mtu kuwa unaibiwa...mitandao hii kwa mimi binafsi nimenunua bidhaa nyingi sana...na ukitaka kukwepa kodi mathalani item uliyonunua ni expensive unaweza kunegotiate na muuzaji akaandika bei kidogo kwenye Invoice...kitu ulichonunua $100 unaweza kuandika $15...:A S wink:

so buy with confidence....

asante sana kiongozi
 
Mbona walikataa kutumia hata bei ya invoice wakaja na bei yao ya $200 wakati mm nililipa $80 tu! nikapeleka hadi bank statement km proof but wapi, was very frustrating indeed
ngoja nikupe maujanja ...kabla hujanunua ongea na seller kwenye "contact a seller" muombe aandike bei kidogo kwenye invoice ya item...mathalan....kitu chako cha $80 unaweza kuandika $10...:cool2: hasa mitandao ya china au EBAY ukinunua maujanja kitambo sana....a..
 
Mbona walikataa kutumia hata bei ya invoice wakaja na bei yao ya $200 wakati mm nililipa $80 tu! nikapeleka hadi bank statement km proof but wapi, was very frustrating indeed

ulinunua wapi? ikiwa seller amekataa...usimg'ang'anie jaribu several sellers hata mtandao mwingine kabisa...kuna sellers wakaksi kinoma...wengine wanajua biashara sana...hata ukitaka akuandikie $1 anaandika....:A S 109:
 
ngoja nikupe maujanja ...kabla hujanunua ongea na seller kwenye "contact a seller" muombe aandike bei kidogo kwenye invoice ya item...mathalan....kitu chako cha $80 unaweza kuandika $10...:cool2: hasa mitandao ya china au EBAY ukinunua kitu kutoka Hongkong, singapore, korea au China...

usiende kichwa kichwa...una bergain bei ya invoice ipunguzwe akikubali unanunua....nimefanya hayo maujanja kitambo sana....ukijifanya unanunua nunua bila kuomba adanganye kwenye INVOICE...TRA watakuua..

Huu ndio upuuzi tusioutaka humu.

Sasa we wizi unauita "kaujanja"!

Halafu kwa akili zako zilivyo nyingi unadhani TRA wanajali bei ya hio invoice yako?
Ingekuwa raha basi.

Manake unanunua TV Sonny 75 inches km pc 10 hivi halafu unaandika kila moja $15 tu! Ili ulipe chini.

Halafu we huoni kuwa hata huyo Supplier unamfajamisha kuwa wewe ni MWIZI!

Hebu Watanzania jaribuni kubadilika msome japo kidogo!

Dah!
 
huo upuuzi usioutaka humu... we kama nani :majani7:? hakuna biashara inayoendelea bila ujanja ujanja...kabla ya kuanza kushusha hizo bei TRA washanipiga sana...nikaona inatosha

endelea kulipa kodi kadiri uwezavyo mzee
 
Najaribu kuchangia kadri ninavyoweza lkn kufundisha ummah namna ya KUIIBIA SERIKALI YAKO tena Mbele ya Hadhara namna hii sidhani km ni jambo la maana sana.

Hakuna Mfanya biashara akawasifu TRA lkn ziko namna nzuri tu za kupata mapungufu ya KODI.

Uliza wataalam wakusaidie.
Kupunguza kwako bei kwenye invoice kulikuwa kunasaidia wakati wa NYERERE!
Hio imepitwa na wakati.
 
mkuu mi imenisaidia sana...na sio kama kodi sili[pi kabisa..ikiwa wewe umenyoosha mikono wakutandike poa tu...

kuna siku nimeagiza vitu nikagongwa 18% VAT+17% Excess Duties kwenye bei na shipping costs...niliumia sana nikaona dunia chungu...sasa mwendo ndio huo kucheza nao tu...akili yako kichwani ndugu ikiwa unaona sio issue unapotezea tu au siyo? ila this is what we do...

alafu hakuna mtu hasiyependa nchi yake hapa..hata CCM ukiwauliza watakwambia wanaipenda
 
ngoja nikupe maujanja ...kabla hujanunua ongea na seller kwenye "contact a seller" muombe aandike bei kidogo kwenye invoice ya item...mathalan....kitu chako cha $80 unaweza kuandika $10...:cool2: hasa mitandao ya china au EBAY ukinunua kitu kutoka Hongkong, singapore, korea au China...

usiende kichwa kichwa...una bergain bei ya invoice ipunguzwe akikubali unanunua....nimefanya hayo maujanja kitambo sana....ukijifanya unanunua nunua bila kuomba adanganye kwenye INVOICE...TRA watakuua..

Mkuu maelezo yako yamenipa nguvu sana Na Ninajiona naweza kusonga mbele
ila mkuu mbali na TRA nasikia pale bandari kuna mzunguko wa malipo mengi , Ni kweli?
 
Hapo nimeipata point yako mkuu,na kwa kweli upo sahihi,kinachotakiwa kwenye hizi biashara za mitandaoni UMAKINI unahitajika sana,kuna vitu muhimu vya kuangalia before haujafanya biashara,mimi feedback za seller toka kwa buyers mara nyingi ndio uwa na consider sana juu ya ubora wa bidhaa ya muuzaji!yote kwa yote biashara ya online ni nzuri sana kama ukiwa MAKINI..tuendelee kuelimishana wakuu bila kua na jazba wala kebehi,sisi wote ni Watanzania na lengo letu wote ni maendeleo yetu binafsi na ya jamii zetu kwa ujumla

Kununua online kutoka kwa supplier yeyote duniani inahitaji uangalifu na kila mnunuaji ni lazima achukue tahari yeye mwenyewe mapema kabla ya kuingia mzima mzima.Alibaba imeorodheshwa ktk soko la hisa la Hongzkong ktk bara la asia ndiye mshindani mkubwa wa ebay na amazon na sasa wapo ktk IPO ya soko la hisa New York. Km pangekuwa na kashfa yeyote kubwa wasingaliruhusiwa kuwa Public Company nchini America kwani utapeli wowote utachafua soko la hisa na kuleta nyufa ktk barabara ya uchumi. Tuwe na amani na tuchukue tahadhari mapema
 
Back
Top Bottom