Ni vizuri kununua vitu kwenye alibaba.com kama una mkaguzi China ambaye anaweza cheki vitu vyako kabla havijatumwa au uwe unasafiri mwenyewe kuja China.
Kama huna mtu wakukagua vitu vyako hapa China au kuja china mwenyewe binafsi utapata matatizo tu, maana wachina mara nyingi wanapenda kureduce production costs kwahiyo kuna uwezekana mkubwa wakakupa mzigo wenye ubora wa Chini zaidi yani under specifications.Kitu kibaya zaidi vikashatumwa na ukavipokea haviwezi rudishwa China!vitu vikisha toka nje ya China huwezi virudisha maana sheria zao ni ngumu.
Ushauri wangu, kama wewe ni mfanyabiashara inabidi utumie sourcing agent wa kitanzania ambaye yuko China awe anakusaidia kucheki na kuakiki bidhaa zako na kuakikisha mambo uliyo ongea na supplier wako yanatendeka vizuri.Maana huwezi kuwa unasafiri kuja China kila wakati ni gharama sana na pia huwezi zungumza Kichina, maana lugha pia upelekea kutokuelewana hawa wachina.
Kitu kingine, on alibaba.com suppliers wengi hukataa order ndogo maana hizi order ndogo inakuwaga vingumu kusafirisha na pia unakutaka mara nyingi hawana products in stock mpaka kuwe na order kubwa ndiyo wanafanya production.Wanapenda kupokea order kubwa kwasababu inakuwa lahisi kusafirisha kwa kutumia maji.
Traders Easy Way-We Supply According to your Budget - Featured Electronics