Kwanini Watanzania hamjiungi na ALIBABA small business website

Kwanini Watanzania hamjiungi na ALIBABA small business website

uliza swali ujibiwe mkuu, hapa hakuna mtu anayeuza ujuzi, na hakunamtu mwenye maslahi na alibaba!

Hv mkuu kuna uhusiano wowote kati ya Alibaba na Aliexpress?au ni kama Ebay na Amazon?
 
Hv mkuu kuna uhusiano wowote kati ya Alibaba na Aliexpress?au ni kama Ebay na Amazon?

zote ziko chini ya kampuni moja, alibaba kule wamejazana manufacturer, wholesalers, na traders wanaouza mzigo jumla, japo wapo wanaouza rejareja pia, aliexpress kule unapata vitu vingi vya retail.
 
hapo hakuna shaka mkuu zaidi nyie ndo wenye maujuzi hivyo ni vema ukatabainisha vizuri mkuu

tunabadilishana uzoefu tu mkuu, ukikwama sehem unauliza "jamani nyie ikitokea hivi mnafanyaje", maisha yanakwenda namna hiyo mkuu!
 
zote ziko chini ya kampuni moja, alibaba kule wamejazana manufacturer, wholesalers, na traders wanaouza mzigo jumla, japo wapo wanaouza rejareja pia, aliexpress kule unapata vitu vingi vya retail.

Ahsante sana mkuu,je na hawa Aliexpress umewahi kufanya nao biashara?
 
ndiyo mkuu, wako vuzuri tu.

Asante sana mkuu!naona jamaha wako vizuri hawa jamaha wa Aliexpress,though means zao za shipping naona ziko juu sana,maana naona wengi ni DHL na sio Postal service!
 
Real Businesmen should take risks, hata wao wachine wanatake risk kukutumia. What if uka-claim hujapata mzigo?? si wao wanarefund??

Kama umeliwa ni uzembe wako, ila wengine tunapiga biashara kama kawaida
 
We unasemea sample ya laptop?!!!!..we jamaa! naona unaongelea biashara ya rejareja, kwa taarifa yako ya bure tu binafsi nilishapokea sample nyingi sana kuanzia clone za honda motorbikes, box za spare za pikipiki, motor, generator za umeme, matairi ya pikipiki, alibaba imenikutanisha na watu wengi sana, wewe unataka kununua laptop mbili unataka utumiwe sample, wewe si mwizi tu!!!! sikatai kuna matapeli, hakuna market place inayokosa matapeli, kuidiscredit alibaba kwa sababu ya experience yako mbovu na watu fulani ni utovu wa nidhamu tu, ni sawa na mimi nisema "wamarekani hawafai kitu wale, nimenunua cover ya kindle tu mwezi mzima sasa sijaipata"!!! alibaba Watanzania wanauza na kununua kule, watu wanauza asali, vitunguu, ufuta, karanga, msiwakatishe tamaa watu wasiojua mnawatia uwoga usio na msingi. Alibaba ipo na inazidi kukua siku hadi siku, ingekuwa imejaa matapeli kwa jinsi unavoiweka ingekuwa inakufa, badala yake inakua!
SCARED MONEY DON'T MAKE MONEY!

Huna lolote wewe.
We utawadanganya watz kuwa ulipewa sampla ya Vitu hivyo bure?

Hebu tuwekee ushahidi hapa km huyo jamaa hapo nyuma wa Waybill yako ya hizo sample.

Hivi wewe na bichwa lako unategemea watz wajinga eti!

Nasema tena, Alibaba WIZI ni wengi kuliko waungwana.
Sasa km umepewa kamisheni kuja kuibia watu humu, hupati mtu.

Mwenye biashara kubwa anakesha Jf akipiga bla bla..?

Huna llt wewe.
 
Nimenunua vitu vingi sana mitandaoni sijawahi kutapeliwa...ni MEMBER wa kudumu EBAY, ALIEXPRESS, GOODLUCKBUY,ALIBABA na kote nimenunua kwa kweli taarifa zinazoenezwa kuwa wale jamaa ni wezi ni upuuzi mtupu usiona na ukweli...

japo nimewahi kuagiza device Ebay ikaibiwa posta dar es salaam...wakati ule wa vuguvugu la madawa ya kulevya la Mwakyembe walikuwa wanakagua kila kitu, waliuona ni kitu kizuri ndani yake na wakaiba....

anaetaka maujuzi na uzoefu...ani PM

kiongozi, mimi sitaku PM kwa manufaa ya wadau wengine.. naomba uniambie mchakato mzima mpaka mzigo unakufikia bongo.. in short, shipment options..? mzigo ukifika unaupokelea wapi?
 
kwangu nilichojifunza mkuu ni kudhindwa kuchsnganua michanganuo ya hawa waungwana kiasi kwamba inafikia pahala hawatoi suluhu kuwa tufanye nini . tuanzie wapi nk zaidi ya ubababe wa kudhinda

Wewe unaogopa nini??
 
Nimeshanunua incubator 8 tokea january 2013 toka kwa Alibaba na sijawahi kukumbana na utapeli wala ubabaishaji wowote,hofu yangu kubwa mwanzoni ilikua ni kwenye ubora,lakini nikaja kugundua hata bidhaa zao ni bora tofauti na porojo tunazopeana Watanzania tusiojua reality!na tukumbuke Alibaba ni among the biggest online commerce company in the world,biashara zao kubwa wanafanya America,Europe na Asia,hapa Tanzania ni kama hakuna watu wenye uelewa juu ya Alibaba(kwa maana ya wachache sana) na tukumbuke kua mwezi june Soko la hisa la New York,waliwashinda Nasdaq katika kuwashawishi Alibaba wawe listed kwenye soko lao la hisa,so utaona ni jinsi gani wenzetu wanavyojua u giant wa Alibaba na u serious wao katika biashara..hizo nyingine za WIZI mkubwa,sijui hv na vile,ni porojo tu za Watanzania tulio wengi tunaopendaga kujiona tunajua mambo kumbe hakuna lolote,kwa mtu alie serious na mwenye uelewa kidogo tu,anaweza google na akaona jinsi Alibaba walivyo serious na wanavyoheshimika kimataifa..tuachene porojo Watanzania,kama jambo ujuhi kaa kimya ujifunze kwa wenzako
 
kiongozi, mimi sitaku PM kwa manufaa ya wadau wengine.. naomba uniambie mchakato mzima mpaka mzigo unakufikia bongo.. in short, shipment options..? mzigo ukifika unaupokelea wapi?

Kwanza lazima uwe na physical adress ya posta.....(P.o.Box) inayofanya kazi...Jisajili mitandao yote...

Ebay Huwezi kununua mzigo mpaka uwe umejiunga PAYPAL na iwe imrunganishwa na bank yako (hapa benki yako lazima iwe na Mastercards na Visacards) iwe ina support internet Transactions...Ukishajisaliji...Unaweza kununua....

Mitandao km Alibaba,Ali express si lazima uwe PAYPAL unachotakiwa uwe na Mastercard na Visa...unajisajili mtandao wao...then unakuwa secured na Escrow pesa yako haipotei...kamwe...

Goodluck buy
 
Mkuu hilo ulisemalo sio kweli kabisa.
Usije ukawaponza waTz hapa.

ALIBABA.COM Hawatoi Guarantee yyt kwa Washiriki waliomo humo na makampuni mengi yaliomo humo ALIBABA.COM hayakubali PAYPAL as a source of payments.
Kwa sababu PAYPAL inakuhakikishua Usalama wa Pesa zako.
Wengi wao wanataka utume pesa kwa Moneygram au Western Union.

Na njia hizi zote HAKUNA USALAMA WAPESA ZAKO.

Ukiwaambia utume kwa (LOC) kupitia benki yako ASILIMIA 90% ya makampuni hayo WANAKATAA.

WIZI WENGI MNO kupita WAAMINIFU.
Mwenye kutaka bidhaa CHINA ni bora mara milioni upoteze hio NAULI uende mwenyewe.

Kweli ndg, kuna mambo yanashangaza hapo Alibaba mfano mtu anakwambia Tv Lg org 72 nch atakuuzia kwa usd 110, jamani huu kama si uongo nini? Mimi nimejiunga na huwa nachat nao lakini sina imani nao. Na hawakubali malipo nusu. Waaminifu wapo sema jinsi ya kuwabaini.
 
Huna lolote wewe.
We utawadanganya watz kuwa ulipewa sampla ya Vitu hivyo bure?

Hebu tuwekee ushahidi hapa km huyo jamaa hapo nyuma wa Waybill yako ya hizo sample.

Hivi wewe na bichwa lako unategemea watz wajinga eti!

Nasema tena, Alibaba WIZI ni wengi kuliko waungwana.
Sasa km umepewa kamisheni kuja kuibia watu humu, hupati mtu.

Mwenye biashara kubwa anakesha Jf akipiga bla bla..?

Huna llt wewe.

sina hata biashara kubwa ndugu yangu wala usiogope mi maskini tu, na sina muda wa kubishana na watu virtual kwa sababu sina ninachogain wala kupoteza, wanaonifahamu wapo humuhumu na hawana haja ya kuja kukuhakikishia wewe kwa faida ya kwako wewe, mimi siyo ghost kama wewe, maisha yangu ya online yana uhusiano wa moja kwa moja na real life, humu nina ndugu na marafiki wa duniani, sina shida ya kumfurahisha mzimu wa mtandaoni nisiyemfahamu, nachofanya ni kubadilishana uzoefu wangu mdogo tu na watu wanaouhitaji, sina maslahi yoyote wala silipwi na alibaba kwa hiyo sina shida yoyote ya kukaa nakomaa na mtu anayeponda alibaba, hauipendi licha ya kuwa haujawahi kununua hata chupi alibaba achana nayo kimyakimya, kelele za kanga wa porini toka lini zikamwathiri mwewe?!!!
 
Nimeshanunua incubator 8 tokea january 2013 toka kwa Alibaba na sijawahi kukumbana na utapeli wala ubabaishaji wowote,hofu yangu kubwa mwanzoni ilikua ni kwenye ubora,lakini nikaja kugundua hata bidhaa zao ni bora tofauti na porojo tunazopeana Watanzania tusiojua reality!na tukumbuke Alibaba ni among the biggest online commerce company in the world,biashara zao kubwa wanafanya America,Europe na Asia,hapa Tanzania ni kama hakuna watu wenye uelewa juu ya Alibaba(kwa maana ya wachache sana) na tukumbuke kua mwezi june Soko la hisa la New York,waliwashinda Nasdaq katika kuwashawishi Alibaba wawe listed kwenye soko lao la hisa,so utaona ni jinsi gani wenzetu wanavyojua u giant wa Alibaba na u serious wao katika biashara..hizo nyingine za WIZI mkubwa,sijui hv na vile,ni porojo tu za Watanzania tulio wengi tunaopendaga kujiona tunajua mambo kumbe hakuna lolote,kwa mtu alie serious na mwenye uelewa kidogo tu,anaweza google na akaona jinsi Alibaba walivyo serious na wanavyoheshimika kimataifa..tuachene porojo Watanzania,kama jambo ujuhi kaa kimya ujifunze kwa wenzako

kaa kimya ndugu yangu utaambiwa unalipwa commission na alibaba, sijui commission kwa mauzo yapi...lol!
 
Kweli ndg, kuna mambo yanashangaza hapo Alibaba mfano mtu anakwambia Tv Lg org 72 nch atakuuzia kwa usd 110, jamani huu kama si uongo nini? Mimi nimejiunga na huwa nachat nao lakini sina imani nao. Na hawakubali malipo nusu. Waaminifu wapo sema jinsi ya kuwabaini.

Hayo ndio nayasema mkuu.
Wezi wengi kuliko waungwana.

Hebu soma comments za watu kwenye hio Alibaba express uone watu wanavyolalamika.

Halafu wanakuja watu hapa na kukupa Guarantee.

Hawa jamaa ni wa kuwachunga sana.

Na kama ukifanikiwa kutumiwa hio bidhaa ulionunu basi km ni Mobile phones watakupakilia Viatu vya watoto. Au toys za kuchezea.
 
Mkuu mimi niliagiza HTC ONE X na Huawei Ascend P7 toka kwa sellers wawili tofauti wa Aliexpress na mizigo ilifika tena ikiwa salama na katika good condition?nachojua ni kua,aliexpress unapolipia,pesa yako inakua pending mpaka pale unapopata mzigo wako ndio muuzaji upatiwa pesa,na pia ninachofanya najaribu sana kuangalia huyo seller bidhaa zake alizouza awali ziko rated kiasi gani na prev buyers,buyer protection ambayo ina option za full refund if u dont receive ur order,refund ok keep item as not described!kusema ukweli mimi sijawahi kumbana na tatizo lolote kuanzia,amazon,ebay,alibaba na hata aliexpress,microcentre etc na mimi ni mnunuaji mzuri sana wa mitandaoni
 
Back
Top Bottom