Kwanini Watanzania hawapendi kusafiri?

mwaka huu naenda Ruanda
 
Nilishawahi kuleta uzi kama huu,inashangaza sana,achilia mbali kusafiri nchi za nje,kuna watu mpaka wanazeeka hawajawahi kwenda hata bagamoyo,kaole na wamezaliwa hapo dar tu
 
Nilishawahi kuleta uzi kama huu,inashangaza sana,achilia mbali kusafiri nchi za nje,kuna watu mpaka wanazeeka hawajawahi kwenda hata bagamoyo,kaole na wamezaliwa hapo dar tu
Hivi vitu vinaendana na level ya maisha. Ukichora ile graph ya mahitaji ya binadamu ndiyo utaelewa zaidi. Kwanza binadamu anapigania basic needs kama chakula, mavazi na malazi. Kipato chako kikitosheleza haya na ziada ndiyo unakwenda level nyingine na kadiri kipato kinavyoongezeka ndiyo mambo ya anasa na yasiyo na uhitaji yanavyoongezeka. Ukienda nchi zilizoendelea mtu wa kipato cha kati ana nyumba ya kuishi, nyumba ya kuishi pembeni ya mji kipindi cha summer, magari, boti ya ku-enjoy baharini wakati wa summer, holiday ya kila mwaka kutembelea sehemu mbali mabli duniani nk. Huku kwetu gari linaonekana kama ndiyo level ya ufahari.
 
Kusafiri ni anasa kwa mwananchi ambaye hajui kesho asubuhi atakula nini huku anadaiwa kodi ya nyumba, kurejesha kikoba, ada za watoto na gharama za matibabu ya shangazi aliyemeza panga
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] shangazi aliyemeza panga...
 
πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„Et bora ubanwe kende ila ni kweli mkuu life la bongo ni tight.

Kila kitu bongo kupata ni tabu.
Sasa mzee unapata 20k kwa siku, una mke na watoto wawili, ulipe kodi ya nyumba, kula, umeme, maji, nauli kwenda mzigoni bado hapo hapo hajaumwa mtu, wazazi wanakutizama wewe, unapataje mpunga wa kwenda kwa kusafiri nje ya nchi.

Standard ya maisha yetu ni mbovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…