Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uko sahihi.Iko hivi ukiangalia wazungu wengi ni watu ambao wanafanya sana saving hata wenye vipato vya kawaida.
Wanaweza saving kwakuwa kwanza kiwango cha utegemezi kwao ni kidogo sana. Yani utakuta baba na mama wana mtoto mmoja au hawana na hamna mtu anaewaomba hela.
Hakuna sijui michango ya ukoo, sijui mtoto wa mjomba ada shule, mara rafiki anaoa, mara bibi anaumwa n.k
Birth control imesaidia wenzetu sana. Sisi huku mtu ana ndugu zaidi ya laki na akipata tu ka ajira ka kulipwa laki saba basi kila mtu anamtolea macho, vizinga visivyoisha.
Huyo mtu ata save sangapi ili aweze kutembelea nchi mbalimbali?
Kingine kwa wenzetu wa nje huko wengi wanakula generational wealth. Yani mtu anazaliwa anakuta familia iko well-off kuanzia vizazi kadhaa vilivyopita. So yeye anaendeleza kutengeneza hela tu na future ya kizazi chake so mambo kama kusafiri ni kawaida tu.
Chamwisho ni nchi yetu hii ina mifumo ya ajabu sana. Mtu kumiliki passport tu inaonekana kama vile ni jambo la ajabu sana. Ukienda uhamiaji kutaka passport inakuwa ni mchakato mgumu utadhani unataka kwenda mbinguni.
Nchi za wenzetu kuwa na passport ni kawaida na kila raia anayo kama document muhimu. Hapa kwetu passport inachukuliwa tofauti sijui kwanini CCM hawataki raia wamiliki passport?
Acha uongo bana, mtu atasafiri na njaa?Nchi ya asali na maziwa, why uondoke unaenda kufuata nini huko nje?
matunduiziTanzania ni nchi bora sana duniani. Ukisafiri mikoani inatosha kupata kile ambacho ungekipata duniani kote.
Mkuu umefikiri nini apo?
Tanzania nchi ya amani ambapo ukiweka jitihada kidogo tu maisha yanakunyookea. Sababu kuu ni watu kuridhika na nchi yao na kutokuwa na sababu ya kuhangaika. Hao wakenya, Rwanda na Burundi wana dhiki kali kwenye nchi zao hivyo hawasafiri kwa kupenda.Ukizilinganisha nchi za Afrika Mashariki, hasa Kenya, Uganda, na Rwanda, Watanzania ndiyo wanaoongoza kwa kutokusafiri kwenda nchi zingine. Kwa nini hivyo?
Bwana we, kubali tu uhalisia.Sio lazima tufanane. Kila watu na taratibu zao, ziheshimiwe.
HakikaSasa mzee unapata 20k kwa siku, una mke na watoto wawili, ulipe kodi ya nyumba, kula, umeme, maji, nauli kwenda mzigoni bado hapo hapo hajaumwa mtu, wazazi wanakutizama wewe, unapataje mpunga wa kwenda kwa kusafiri nje ya nchi.
Standard ya maisha yetu ni mbovu.
Poor youTanzania nchi ya amani ambapo ukiweka jitihada kidogo tu maisha yanakunyookea. Sababu kuu ni watu kuridhika na nchi yao na kutokuwa na sababu ya kuhangaika. Hao wakenya, Rwanda na Burundi wana dhiki kali kwenye nchi zao hivyo hawasafiri kwa kupenda.
Wengi wa wanaosafiri si kwa ajili ya kutafuta pesa, bali kwa sababu wana hela.Tanzania nchi ya amani ambapo ukiweka jitihada kidogo tu maisha yanakunyookea. Sababu kuu ni watu kuridhika na nchi yao na kutokuwa na sababu ya kuhangaika. Hao wakenya, Rwanda na Burundi wana dhiki kali kwenye nchi zao hivyo hawasafiri kwa kupenda.
Tupo comfortable nyumbani, Tuzurure tupate nini?😂 Kweli au unajipaka na kuwapaka wabongo wenzako mafuta kwa mgongo wa chupa na kuwadhihaki?! 😂
Umeelezea kama Mwalimu 🙏🙏🙏Ukiachilia mbali pesa yetu kutokua na nguvu duniani.
Hawa wenzetu passport zao zina nguvu sana wanaweza kwenda nchi nyingi bila ya kuomba visa.
kwa mfano huyu mwanadada ni mmarekani, ambapo ukiwa na passport ya marekani unaweza kwenda nchi 143 bila kua na visa hili lina wapa unafuu mkubwa sana tofauti na passport zetu.
Na pia katika baadhi ya nchi zitakazo hitaji awe na visa ili kuingia hazisumbui sana kwasababu ina fahamika akishakua raia wa marekani bila shaka yupo vizuri ki'uchumi na inakua rahisi kupewa visa kuliko sisi wa nchi nyengine.
Kusafiri kimataifa kuna changamoto nyingi sana na nchi nyingi zina zingatia passport yako na hali ya nchi yenu ki'uchumi.
NB: kwa wasio jua maana ya visa ni kibali unachopewa na nchi unayotaka kwenda baada ya kujiridhisha wao kwa masharti waliojiwekea, na huwa kina weza bandikwa ndani ya passport kama stika au kuwekwa muhuri wa stamp.
Unaambiwa tuma hela ya matibabu haraka[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] shangazi aliyemeza panga...
6. MajukumuMwanamke aitwaye Cassandra de Pecol kutoka Connecticut, alifanikisha ndoto yake ya kutembelea nchi zote duniani, 193,
akiwa na umri wa miaka ishirini na saba.
Mpaka anafikisha miaka 18, Canada ndiyo nchi pekee aliyokuwa amefika, tena, ni kwa vile mama yake anatokea huko. Sababu kubwa iliyomfanya asisafiri akiwa mdogo ni uwezo mdogo wa kifedha.
Kufanikiwa kwake kuzitembelea nchi 193 ni jitihada zake binafsi. Anavyoonekana si tajiri, ila anapenda kusafiri. Lakini kuna Watanzania ambao pengine wana uwezo mkubwa kifedha kumzidi yeye lakini bado hawasafiri.
Ukizilinganisha nchi za Afrika Mashariki, hasa Kenya, Uganda, na Rwanda, Watanzania ndiyo wanaoongoza kwa kutokusafiri kwenda nchi zingine. Kwa nini hivyo?
1. Umaskini?
2. Lugha?
3. Ugumu wa upatikanaji wa passport?
4. Ushamba?
5. Utamaduni?
Sababu ni nini?
😃😃😃Vyote ukiviweka pamoja ukiongeza na utapeli uongo uongo nda unapata mtanzania halisi.