Kwanini Watanzania hawapendi kusafiri?

Wasomali vipi? Hawana njaa?
Mkuu, labda niseme miongoni mwa mambo yanayomchochea mtu kusafiri ni pamoja na:
1. Shida
Hapo utakuta watu wanaotafuta ajira na makazi, mfano raia wa Somalia, Ethiopia, Libya, Sudan, n.k.

2. Mafanikio.
Hapo, watu wanaosafiri si kwa sababu ya hali ngumu, bali kipato kinawaruhusu.

Sababu za safari zinaweza kuwa masomo, utalii, biashara, n.k.
Nchi zinazoongoza duniani kwa raia wake kusafiri ni hizi hapa
1. Finland
2. USA
3. Sweden
4. Denmark
5. Norway
6. Hong Kong
7. New Zealand
8. Canada
9. Australia
10. France

πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Wazungu wamejipendelea? Mbona hakuna hata nchi moja ya Afrika?
 
Hakuna nchi ina gawa hati ya kusafiria kama njugu, utaratibu ufatwe

 
Tupo comfortable nyumbani, Tuzurure tupate nini?
Inaonekana una kazi nzuri, mahali pazuri pa kuishi na kila kitu ni uhakika.

Wengine ramani hazisomi na hawana matumaini wanajaribu kutafuta maisha kwingineko duniani. Na sio jambo baya, dunia ni yetu na tumeamrishwa tuizunguke tuone maajabu na uumbaji wa mungu wetu muumba.

Kama umefunguliwa na umejaaliwa na mungu wako mshkuru sana!
 
Ila watanzania wako sehemu kubwa dunia kuna nchi unaweza kwenda utashanga unakutana na mbongo

Ova
 
Kusafiri ni anasa kwa mwananchi ambaye hajui kesho asubuhi atakula nini huku anadaiwa kodi ya nyumba, kurejesha kikoba, ada za watoto na gharama za matibabu ya shangazi aliyemeza panga
Hapo sasa.
 
Hayo umesema wewe, ila mie nimekupa sababu why watanzania hatoki nje.
Japo nimeisema katika mtindo wa masihara.
Ila ni kuwa watanzania wapo comfortable na Nchi yao ukilinganisha na mataifa mengine.
Pia ukiwa mtanzania huwezi kupata ata ile hadhi ya Ukimbizi sababu kuna Amani.
 
USHAMBA

Hata watu wenye pesa hapa Tanzania wengi hawapendi Adventure au kupata Exposure hata ya kujua tamaduni za watu tofauti tofauti

Wanachojua wakishatajirika basi ni kununua magari na nyumba kisha kula pombe na Wanaaake kila siku
 
USHAMBA

Hata watu wenye pesa hapa Tanzania wengi hawapendi Adventure au kupata Exposure hata ya kujua tamaduni za watu tofauti tofauti

Wanachojua wakishatajirika basi ni kununua magari na nyumba kisha kula pombe na Wanaaake kila siku
Umenikumbusha habari niliyoisikia hivi karibuni!

Kwamba kule Arusha maeneo ya Loliondo, kuna Mmasai alimkopesha mfanyabiashara mwenye sheli za mafuta shilingi milioni mia mbili. Halafu mtu mwenyewe alikuwa akiishi kwenye nyumba ya nyasi.

Hata alipojenga nyumba ya kisasa baada ya kushawishiwa na marafiki zake, alirudi kwenye nyumba yake ya nyasi baada ya siku chache kwa madai kuwa nyumba ya bati siyo nzuri.

Sasa huyo mwenye uwezo wa kukopesha milioni mia mbili kwa mkupuo angeshindwa kutembelea alau nchi moja kwa mwaka?

Ni kweli kuwa ushamba ni sababu mojawapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…