Kwanini Watanzania hawapendi kusafiri?

All of the above ikiwemo hali ya kiuchumi.
 
Sio kwamba hatupendi kusafiri ni kwamba nauli ndio changamoto wenzetu wametatua swala la nauli ndio maana wanafanikiwa ukijifungia ndani fursa pia unazifungia kutoka Mkoa au Nchi nyingine ni kufungua fursa huko...
 
Nitajibu Kulingana na Title. UMEWAPA HIZO HELA ZA KUSAFIRIA
1. Kwanza Unatakiwa kujua Pato la Mtanzania Mmoja Mmoja Ni Lipi

2. Mtu anawaza Madeni huo Muda wa Kusafiri Anautoa Wapi.?
 
Asilimia kubwa wanaoishi Ulaya hawawazi kesho watakula nini watavaa nini, hiyo hatua wameshaivuka miaka mingi Sana ndio maana unaona wanawaza kwenda anga za juu kuishi.. kubuni mambo mengii sasa utakuwa mbunifu wa aina gani Kama muda wote unawaza utakula nini? Njaa inakuuma. Stress ?



Sasa wewe mtanzania wa makambako bado unawaza kesho utakula nini, utavaa nguo gani? Kama pesa ya mama mwenye nyumba inakusumbua kuipata hiyo nauli utatoa wapi!.? Ya kwenda nchi za nje? Kwanza kitengo tu cha kwenda kuomba kibali wahusika wanakushangaa wanaanza kukupa ushauri usiende. 😁 wanakuambia ukienda tunajua hautarudi.. utang'ang'ania huko huko.

ndugu zangu watanzania. Pesa ni muhimu Sana hasa kwa sisi wanaume pesa ni muhimu sana. Hakuna mtu asiependa kuishi maisha mazuri hayupo
 
Napenda kuchangia. Binafsi nimesafiri Dubai na Guangzhou kama mkalimani. Njia nyingine unaweza kujifunza lugha za kimataifa kuanzia 5 na kuendelea, uwe competent kweli, then safari za nje utazizoea.
 
Tuna mambo mengi kichwani ndo maana hatuwezi kusafiri, hata ukiangalia nchi za wenzetu wanafocus na ushoga kwa sababu hawana shida ya maji, umeme, umasikini na afya. Akili zao zinaanza kutafuta shida nyingine maana binadamu tumeumbwa kusolve shida na matatizo. Ndo maana hata wabongo tukishinda vijiweni hatuwezi kujikalia tu tutaanza kuchunguza watu na kufuatilia watu that is our human nature.
 
Ugali mtamu😄

Kauli hiyo waliitoa walipotakiwa waandamane kipindi kile mkuu wa polisi aliposema wakiandamana watapigwa kipigo cha mbwa koko. Sijui ni ile UKUTA ya chadema?

Kwa asili ni waoga. Lakini kwasababu kuna chakula, watabanana hapo tu maisha yaendelee.

Hata kuku anapata mauchafu ya kula hawezi kuwa na juhudi za kuruka juu kama ndege wengine wala hajishghulishi.
 
Sio kwamba hatupendi kusafiri ni kwamba nauli ndio changamoto wenzetu wametatua swala la nauli ndio maana wanafanikiwa ukijifungia ndani fursa pia unazifungia kutoka Mkoa au Nchi nyingine ni kufungua fursa huko...
Wazungu wana save hela kwa ajili ya vacations pia
Je sisi wabongo tunafanyaga hivyo

Ova
 
Hapo kwenye kupata paspoti uhamiaji nimekuelewa sana
 
Vyote ukiviweka pamoja ukiongeza na utapeli uongo uongo nda unapata mtanzania halisi.
Mkuu, si kila Mtanzania ni muongo!
Si kila Mtanzania ni tapeli!

Na hata kama kuna waongo na matapeli, hawawafikii Wanigeria, ingawa si wote pia wako hivyo.

Mbona Wanigeria wanasafiri sana kuwazidi Watanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…