Kwanini Watanzania hawapendi kusafiri?

Kwanini Watanzania hawapendi kusafiri?

Mwanamke aitwaye Cassandra de Pecol kutoka Connecticut, alifanikisha ndoto yake ya kutembelea nchi zote duniani, 193,
akiwa na umri wa miaka ishirini na saba.

Mpaka anafikisha miaka 18, Canada ndiyo nchi pekee aliyokuwa amefika, tena, ni kwa vile mama yake anatokea huko. Sababu kubwa iliyomfanya asisafiri akiwa mdogo ni uwezo mdogo wa kifedha.

Kufanikiwa kwake kuzitembelea nchi 193 ni jitihada zake binafsi. Anavyoonekana si tajiri, ila anapenda kusafiri. Lakini kuna Watanzania ambao pengine wana uwezo mkubwa kifedha kumzidi yeye lakini bado hawasafiri.

Ukizilinganisha nchi za Afrika Mashariki, hasa Kenya, Uganda, na Rwanda, Watanzania ndiyo wanaoongoza kwa kutokusafiri kwenda nchi zingine. Kwa nini hivyo?

1. Umaskini?

2. Lugha?

3. Ugumu wa upatikanaji wa passport?

4. Ushamba?

5. Utamaduni?

Sababu ni nini?
Yaani mfano wa huyo mtu mmoja ndo unatuletea watanzania 60+m?
Kwanini hujawauliZa mataifa mengine? Swali la kitoto sana.
 
Unaongea ukiwa choo kipi Cha shule au stand
Nenda wizara ya mawasiliano na uchukuzi kaombe taarifa za idadi ya watz waliosafiri nje ya nchi kisha uje uandike upya
 
Mtu anazaliwa hadi kuzeeka hajawahi hata kutembea mikoa minane ya nchi yake ndiyo atavuka border!
 
Yaani mfano wa huyo mtu mmoja ndo unatuletea watanzania 60+m?
Kwanini hujawauliZa mataifa mengine? Swali la kitoto sana.
Kwani hujui kuwa mtu mmoja anaweza kuwabadilisha mamilioni ya watu?

~ Nyerere alikuwa ni mtu mmoja, lakini aliingiza nchi nzima kwenye ujamaa na mpaka sasa athari zake zingalipo. Mojawapo ni ya Watanzania(japo si wote) kuogopa kusafiri.

~ Adolf Hitler alikuwa mtu mmoja, na unafahamu alikoifikisha Ujerumani.

~ Carl Max alikuwa ni mtu mmoja! Unajua falsafa yake ilivyoathiri ulimwengu?

Hakuna anajua kila kitu, na hakuna asiyejua kitu maadam ana akili timamu.

Unapong'amua chochote kizuri kwa mwenzako, kama una mtazamo wa kijasiriamali, kidake haraka na kuitumia kwa manufaa kabla haijawa too late!

Kwa hiyo, ni sahihi kuutumia mfano wa huyo mwanamke mmoja kuwahamasisha Watanzania wenzangu kusafiri.

Hata akihamasika mmoja tu, itakuwa ni hatua kubwa sana.
 
Mwanamke aitwaye Cassandra de Pecol kutoka Connecticut, alifanikisha ndoto yake ya kutembelea nchi zote duniani, 193,
akiwa na umri wa miaka ishirini na saba.

Mpaka anafikisha miaka 18, Canada ndiyo nchi pekee aliyokuwa amefika, tena, ni kwa vile mama yake anatokea huko. Sababu kubwa iliyomfanya asisafiri akiwa mdogo ni uwezo mdogo wa kifedha.

Kufanikiwa kwake kuzitembelea nchi 193 ni jitihada zake binafsi. Anavyoonekana si tajiri, ila anapenda kusafiri. Lakini kuna Watanzania ambao pengine wana uwezo mkubwa kifedha kumzidi yeye lakini bado hawasafiri.

Ukizilinganisha nchi za Afrika Mashariki, hasa Kenya, Uganda, na Rwanda, Watanzania ndiyo wanaoongoza kwa kutokusafiri kwenda nchi zingine. Kwa nini hivyo?

1. Umaskini?

2. Lugha?

3. Ugumu wa upatikanaji wa passport?

4. Ushamba?

5. Utamaduni?

Sababu ni nini?
Kila mtu na vipao mbele vyake. Kwa life ya kuungaunga usafiri nchi zote duniani..? Kwanza kwenda kufanya nini. Afu nauli sasa nk mtaji mkubwa tosha huo kibongo bongo
 
Si lazima kusafiri nchi zote, lakini kwenda alau nchi kadhaa ni vizuri kwa afya ya fikra. Inasaidia kuondokana na fikra mgando!
 
Mwanamke aitwaye Cassandra de Pecol kutoka Connecticut, alifanikisha ndoto yake ya kutembelea nchi zote duniani, 193,
akiwa na umri wa miaka ishirini na saba.

Mpaka anafikisha miaka 18, Canada ndiyo nchi pekee aliyokuwa amefika, tena, ni kwa vile mama yake anatokea huko. Sababu kubwa iliyomfanya asisafiri akiwa mdogo ni uwezo mdogo wa kifedha.

Kufanikiwa kwake kuzitembelea nchi 193 ni jitihada zake binafsi. Anavyoonekana si tajiri, ila anapenda kusafiri. Lakini kuna Watanzania ambao pengine wana uwezo mkubwa kifedha kumzidi yeye lakini bado hawasafiri.

Ukizilinganisha nchi za Afrika Mashariki, hasa Kenya, Uganda, na Rwanda, Watanzania ndiyo wanaoongoza kwa kutokusafiri kwenda nchi zingine. Kwa nini hivyo?

1. Umaskini?

2. Lugha?

3. Ugumu wa upatikanaji wa passport?

4. Ushamba?

5. Utamaduni?

Sababu ni nini?
Mkuu unajua bei za vyakula hotelini yanakosimama mabasi watu wachimbe dawa?
Chips vipande 10 na kuku elfu sita.
Hapo ni ndani ya Tanzania
 
Mkuu, labda niseme miongoni mwa mambo yanayomchochea mtu kusafiri ni pamoja na:
1. Shida
Hapo utakuta watu wanaotafuta ajira na makazi, mfano raia wa Somalia, Ethiopia, Libya, Sudan, n.k.

2. Mafanikio.
Hapo, watu wanaosafiri si kwa sababu ya hali ngumu, bali kipato kinawaruhusu.

Sababu za safari zinaweza kuwa masomo, utalii, biashara, n.k.
Nchi zinazoongoza duniani kwa raia wake kusafiri ni hizi hapa
1. Finland
2. USA
3. Sweden
4. Denmark
5. Norway
6. Hong Kong
7. New Zealand
8. Canada
9. Australia
10. France

😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃
Wazungu wamejipendelea? Mbona hakuna hata nchi moja ya Afrika?
Mfano Finland na nchi nyingi za Scandinavian elimu ni bure hadi chuo, kwa hiyo mzazi hata hawazi kuhusu ada ya mtoto. Hapo bongo tunawaza ada tu. Mtu ana watoto 3 hadi wa nne na wote anawalipia ada.

Pia vipato vya walio wengi ni duni ukijumuisha na majukumu mengi ya kusaidia ndugu.
Wenzetu pia hawazai watoto wasioweza kuwatunza, mtu yuko radhi asizae kabisa kuepuka kumtesa mtoto atakayemleta duniani.

Bongo kila mtoto anakuja na riziki yake loh.
 
Kuna jamaa ameelezea vizuri sana humu Chaliifrancisco
Kujazia ni vitu vidogo vidogo kama lugha

Jaribu kufatilia mataifa ambayo atleast wanaongea kingereza hapa africa exposure yao mambo ni mepesi mno kwenda nje

Mtanzania ana asili ya woga na kupenda mazoea akishaona lugha inampa chenga kidogo anakata tamaa
 
Mfano Finland na nchi nyingi za Scandinavian elimu ni bure hadi chuo, kwa hiyo mzazi hata hawazi kuhusu ada ya mtoto. Hapo bongo tunawaza ada tu. Mtu ana watoto 3 hadi wa nne na wote anawalipia ada.

Pia vipato vya walio wengi ni duni ukijumuisha na majukumu mengi ya kusaidia ndugu.
Wenzetu pia hawazai watoto wasioweza kuwatunza, mtu yuko radhi asizae kabisa kuepuka kumtesa mtoto atakayemleta duniani.

Bongo kila mtoto anakuja na riziki yake loh.
😃😃😃
 
Kuna hiki kizazi cha wale tulikuwa vijana miaka ya 80s na 90s kilivuka sana border USA na Europe

Kizazi cha waliokuwa vijana miaka ya 2000 wakaingia sana hapo S.A kizazi cha sasa hivi ni uchawa tu
Kizazi cha kuingia 80 wengi walikula boda kwenda ulaya,mtu anapitia Sudan aitafute Egypt au Algeria, moroco aingie ulaya ile ilikuwa si mchezo...na wengi walikufa na hawakuonekana mpaka leo
Kizazi cha sahvi ambacho tulikitegemea kimekywa cha wakata mauno tu

Ova
 
Back
Top Bottom