Kwanini watanzania wanamlaumu mwalimu Nyerere kwa kukosa elimu?

Kwanini watanzania wanamlaumu mwalimu Nyerere kwa kukosa elimu?

Kmwalimu kufanya kiswahili ndio lugha kuu tanzania alikuwa yupo sawa sana na mfumo mzima wa elimu ulikuwa hauna utata Wowote.

Kiswahili: Niambieni ni nchi ngapi za Afrika viongozi wake wanaweza kuongea kiigereza kwa ufasaha na hivi juzi tu kuna mbunge mmoja wa nertheland alifanya reseach na kupitia nchi kama south Afrika na kenya ambazo ndio zinaonekana watu wanaongea kingereza kizuri bado akakuta watu wengi hawafahamu maneno mengi tu ya kiingereza kwa sababu Lugha ya kiingereza ni "second Language" kwao na alipopita Tanzania alishtuka sana kuona watu wote bungeni wanatumia lugha moja na kila mtu anaweza kujielezea kwa ufasaha na hata asiyesoma anaweza kuelewa. Hivi Nyinyi watu mnataka kuniambia Zambia ambayo Kiingereza ndio lugha ya Taifa watu wote wanaongea kiingereza mpaka kijijini.

Huu ndio ujinga mkubwa wa mwafrika kufikiri kiingereza au kujua kiingereza ndio kuelimika.Wachina,wajapani,wacanada na nchi zote za European Union isipokuwa UK wote wanazungumza lugha zao wenyewe na nchi zote hizo zimeendelea kupita hata hiyo UK, Ndugu zangu kiingereza hakina impact yoyote kwenye maendeleo ya nchi na ukitaka kufahamu hilo mchukue msomi yoyote unayemjua wewe ambaye amekulia Afrika na kusoma Afrika uone kama anaweza kuongea au kujielezea kama Tony Blair anavyoweza kujielezea.Swala la lugha halina msingi wowote na ndio maana hata viongozi wengine wengi tu duniani hawajui hata neno lolote la kiingereza na bado wanashiriki kwenye mikutano ya kimataifa kwa kuongea lugha zao.

Ujamaa: Naona watu hawajui maana ya Ujamaa na wanashindwa hata kujua maana ya Ubepari.Ubepari hauna maana njia kuu za uchumi zimilikiwe na watu binafsi hyo sio kweli kwani ukifatilia kwa karibu zaidi utakuta nchi zote ambazo wanajiita za Kibepari Elimu na Afya pamoja na Usafiri bado zinamilikiwa na serikali mfano Mzuri ni uingereza ambao wao ni wa kwanza kuchampion ubepari lakini kimsingi sio ubepari kamili kwani Elimu,afya ni bure na hata kama unakazi bado serikali wanakulipa fedha, Je ndugu zangu huo ni UBEPARI?

Watanzania inabidii tufikirie kwa makini sana ni nini yule Mzee alivyokuwa anafanya na sio kulaumu pasipo sababu za msingi, wengi wanafikiria Ulaya watu wengi ni matajiri na hakuna masikini, sio kweli hata kidogo kuna watu ulaya hata pakuishi hawapaju"Homeless"

Elimu: NI kweli watu walilazimishwa kubadili dini ili waweze kujiunga na shule za missionari mfano mzuri ni Jaji wetu John Ramadhani na kuna kiongozi wa kani la kianglikani anaitwa Pia John Ramadhani na wengi weni tu.Sasa kama alikuwa hajali watu wake wapate elimu na kuacha mfumo ho je watanzania kweli wangesoma.Nyerer alifanikiwa Mengui sana na hat ahizo University ambazo tanzania tunaza sasa sio kama hawa viongozi wa leo wamezijenga bali ni vilevile vyuo alivyjenga kipindi cha utawala wake na viongozi wa leo kuzibadiisha kuwa university wakiwa walimu ni walewale na majengo ni yale yale mfano Mzumbe,Nyegezi,IFM,vyuo vya Uhasibu Arusha,DSA Mbeya,DSA Mtwara na DSA Dar hebu niambieni mpaka yeye kutoka madarakani kuna vyuo vingapi vipya vimejengwa?

Tanzania ilikuwa inatambulika hata kwenye Michezo leo hii ndio tunasema tumeendelea hakuna mwanamichezo yoyote ambaye anatam,bulika na hata kama yupo ni juhudi zake binafsi na sio program yoyote ya serikali.

Hospitali zilikuwa ni bure na Elimu sasa leo hii kila kitu kulipia ni jinsi gani watoto wa mlalahoi na mshahara kiduchu wataweza kusomesha watoto wao.Kumbukeni wingi wa Vyuo sio ndio watu ndio kuelimika.
 
Mkandara,
Kama ukisoma vizuri maelezo yangu hata nilvyoelewa ya wengine, hayapingani sana na yako. Ila tu tunaangalia upande wa pili wa Mwalimu. On the positive side we have all the qualities as a leader, he made it, and especially at that time when cold war and the law of the jungle (who had to control the resources in Africa) prevailed. Nyerere alikuwa intelligent, Azimio la Arusha and other prints were perfect; but our question is why did he choose that path? He wanted to centralize his power so that he cannot fall. Kama alivosema Joka Kuu hapo juu, maybe hata kufundisha lugha ya Kiswahili ilikuwa ni motive yake kuwa watu wamuelewe au hata kuwadumaza watanzania wasijue mengi.

Hebu twambie kwa mfano, kulikuwa na National service, halafu na Azimio la Musoma; what was the idea here. Nasikia hata kile chuo cha Kivukoni watu walikuwa wanagraduate bila ya certificate (without graduation examinations and diplomas). He did the same thing China did from 1966 - 1976 during cultural revolution. Mao abolished all examinations in all schools in 1966. Examinations only resumed in 1978.

Mkandara inawezekana ni kweli huu usingizi wa Wa-Africa wengi unatokana na siasa za "kipumbavu" za Africa. Kwa mfano; ingawa Dunia karibu yote ilitawaliwa, lakini hadi leo ni Africa tu ndiyo haiendelei. Na viongozi wengi (hata Nyerere) wali-preach kuwa kutoendelea kwetu ni kwa sababu ya wazungu. Racism maybe is there, but wengi tunashindwa kufanya wajibu wetu kwa sababu tunadhani kuwa wazungu hawataki tuendelee. Hadi kesho Nyerere alikuwa anaamini kuwa ujamaa ndiyo solution ya matatizo ya dunia, na kuwa Africa iko marginalised in wealth making (which maybe true), but to which extend? Hata kuchimba mfereji au kulima shamba la viazi tunahitaji capital from donors. Nyerere amewahi kuongoza kundi la Nchi ombaoma kwenda Cancun Mexico (Regaan era) kudai chetu, yaani kile walichootuibia zamani (which was well explained); sasa chambua hapa waTanzania wa leo wamedumaa, ukiwambia kitu chocote kile kuhusu kuwajibika wanaona taabu, tumelemaa au tumelemazwa? Mie naona tumelemazwa.

Governance versus Madaraka Mikononi/mikoani (Kiongozi asiwe Mnyampara). Mzee mwezangu, unakumbuka siku zile tunanenda shule, kule Bora Shoes (bata) au National Milling wafanyakazi wanagoma, wanamfungia manager mlango ati kwa kuwaamrisha watu wafanye kazi. Nyerere alikataza watu wasiamrishwe kufanya kazi, ati ni Unyampara. TUkaja kwenye Chama kishike hatamu, na mwanachama aingiaye chamani lazima apewe mafunzo ya kupenda chama na fikra za mwenyekiti. Halafu kila Kampuni lazima iwe na ofisi ya Chama ambacho ndicho chenye nguvu kuliko meneja mkuu.

Tukaja kwenye kufunga maduka etc wtc. Kama alivyosema Prof. A Mushi hapo juu, aliongoza kwa campain za kuhamasisha watu. Tukaja kwenye vita ambayo tulifinance in all phases; kwanza, kuikomboa kagera, kumuondoa Amin, kumuweka lule, kumismika Obote, kumuondoa obote na kumsimika sijui Binaisa etc etc. WanTanzania tulifany yote haya na kukubaliana kutokana na Elimu tuliyokuwa nayo. Kumbuka silbasi yetu yote ilikuwa kisiasa siasa tu. Huwezi kuendelea shule high school kama hukupasi Siasa; you remember?

Then What was the motive? He had his way to make sure that he doesn't loose grip in power.

Kama alivyosema joka Kuu hapo juu, serikali ilibidi icompete na private sector or other institution kujenga mashule yake na hospitali zake. Why he didn't choose this path?

Nodoby hates Nyerere, he is the one who influenced us, he is responsible for our well being or doom today; inawezekana ingawa sisi zote tumesoma, ile elimu haikutusaidia bali imetulaza zaidi, ndiyo maana hatuamki. Kama siyo hiyo system basi inawezekana kuwa we are wrong in our IQs. But Tanzania ya leo inatukumbusha our past and mostly is our education foundation and heritage after independence.

Watu wote wanaendelea kwa nini sisi hatuendelei? Na vile vile nabisha kabisa na mleta hoja kuwa waTanzania wote walio nje ni failure, nafikiri hizo sample zake kazichukua kiholela sana na hata yeye mwenyewe hakutaka kuwaelewa hawa watu aliowauliza. Ndugu mtoa hoja hata wewe inawezekana tofauti kubwa uliyonayo na hao wanaolaumu nyerere kwa elimu ni ndogo sana; what did you accomplish, that should be an issue. Maybe you have a PhD, but did you do your "right thing"? Did you write a book? Did you create employment? we have a series of problems. Remember that education has to liberate your mind, and by such liberation you grab oppoturnities!
 
Mkandara,

..tatizo lako wewe kila hoja unataka kuiangalia kwa Wakristo vs Waislamu. vipi wewe?!

..matokeo ya sera kama ya elimu yanachukua muda mrefu kuonekana.

..kwa mfano mwanafunzi aliyeanza darasa la kwanza kutokana na sera ya Mwalimu Nyerere ya UPE, ali-graduate wakati wa utawala wa Mzee Mwinyi.

..vilevile mwanafunzi aliyesoma ktk mfumo wa double session iliyoanzishwa na Mzee Mwinyi aligraduate wakati wa Mkapa yuko madarakani.

..usipokuwa makini unaweza kutoa sifa/lawama pasipo stahili.

Mkandara said:
Viongozi wote unaowaona leo hii ktk mashirika na serikali ni wanafunzi wa mwalimu na nakuhakikishia kwamba vijana wa leo hawawezi kusimama nao sambamba iwe ktk Elimu dunia au fikra tu.

..umekosea ktk hoja yako hapo juu kwasababu hukuzingatia ni wakati gani unapaswa kupima mafanikio/mapungufu ya sera ya elimu.

..viongozi walioko leo, say wa rika la Kikwete na wenzake, walianza shule about 5 yrs after independence. lakini ukiangalia waalimu waliowafundisha ni wale waliokuwa trained na mkoloni.

..hao vijana unaowabeza kuwa hawana uwezo wamefundishwa na waalimu wa hovyo-hovyo waliotokana na sera hovyo-hovyo za elimu za Mwalimu Nyerere.

..badala ya ku-argue kwa kutumia masuala ya udini-udini, hebu angalia uwezo wa waalimu wa kabla na baada ya sera za Mwalimu za Nyerere. angalia mazingira za kazi za waalimu, na heshima na hadhi ya mwalimu kabla na baada ya sera za Mwalimu Nyerere.vilevile angalia upatikanaji wa vifaa kabla na baada ya sera za Mwalimu Nyerere.

..athari za sera za Mwalimu za elimu hazikuonekana tangu mwanzo kwasababu ya msingi imara uliojengwa kabla yake. lakini muda ulivyokuwa ukiendelea quality ilianza kushuka, na mazingira ya elimu yalianza kuwa mabaya na kuonekana waziwazi.

..nilipoanza shule tulikuwa tukipewa textbooks na madaftari. by the time namaliza shule ilikuwa haina waalimu, haina madawati tunakalia matofali, na haina textbooks.

..MWALIMU ALIKUWA NA NIA NZURI KTK SERA ZAKE ZA ELIMU, LAKINI HAKUWA NA NJIA NZURI ZA UTEKELEZAJI.
 
Uwekezaji ndugu yangu husingewezekana kwenye nchi ambayo ndio kwanza imepata Uhuru na hata hizo sera za uwekezaji wakti huo hazikuwepo kama sasa.Uwekezaji ulikuwa ni ule kama wa Zimbabwe na leo tunaona matatizo yake.Kulikuwa na ulaghai wa hali ya juu na sio uwekezaji kama unavyofikiria na leo hii pia umeona uwekezaji jinsi unavyoaffect nchi yetu, madini yote ambayo yanapatikana Tanzania tunapata asilimia 3% JE huo ndio uwekezaji?Hahahaa

You can be a fool even you go to school
 
Kmwalimu kufanya kiswahili ndio lugha kuu tanzania alikuwa yupo sawa sana na mfumo mzima wa elimu ulikuwa hauna utata Wowote.

Kiswahili: Niambieni ni nchi ngapi za Afrika viongozi wake wanaweza kuongea kiigereza kwa ufasaha na hivi juzi tu kuna mbunge mmoja wa nertheland alifanya reseach na kupitia nchi kama south Afrika na kenya ambazo ndio zinaonekana watu wanaongea kingereza kizuri bado akakuta watu wengi hawafahamu maneno mengi tu ya kiingereza kwa sababu Lugha ya kiingereza ni "second Language" kwao na alipopita Tanzania alishtuka sana kuona watu wote bungeni wanatumia lugha moja na kila mtu anaweza kujielezea kwa ufasaha na hata asiyesoma anaweza kuelewa. Hivi Nyinyi watu mnataka kuniambia Zambia ambayo Kiingereza ndio lugha ya Taifa watu wote wanaongea kiingereza mpaka kijijini.

Huu ndio ujinga mkubwa wa mwafrika kufikiri kiingereza au kujua kiingereza ndio kuelimika.Wachina,wajapani,wacanada na nchi zote za European Union isipokuwa UK wote wanazungumza lugha zao wenyewe na nchi zote hizo zimeendelea kupita hata hiyo UK, Ndugu zangu kiingereza hakina impact yoyote kwenye maendeleo ya nchi na ukitaka kufahamu hilo mchukue msomi yoyote unayemjua wewe ambaye amekulia Afrika na kusoma Afrika uone kama anaweza kuongea au kujielezea kama Tony Blair anavyoweza kujielezea.Swala la lugha halina msingi wowote na ndio maana hata viongozi wengine wengi tu duniani hawajui hata neno lolote la kiingereza na bado wanashiriki kwenye mikutano ya kimataifa kwa kuongea lugha zao.

Ujamaa: Naona watu hawajui maana ya Ujamaa na wanashindwa hata kujua maana ya Ubepari.Ubepari hauna maana njia kuu za uchumi zimilikiwe na watu binafsi hyo sio kweli kwani ukifatilia kwa karibu zaidi utakuta nchi zote ambazo wanajiita za Kibepari Elimu na Afya pamoja na Usafiri bado zinamilikiwa na serikali mfano Mzuri ni uingereza ambao wao ni wa kwanza kuchampion ubepari lakini kimsingi sio ubepari kamili kwani Elimu,afya ni bure na hata kama unakazi bado serikali wanakulipa fedha, Je ndugu zangu huo ni UBEPARI?

Watanzania inabidii tufikirie kwa makini sana ni nini yule Mzee alivyokuwa anafanya na sio kulaumu pasipo sababu za msingi, wengi wanafikiria Ulaya watu wengi ni matajiri na hakuna masikini, sio kweli hata kidogo kuna watu ulaya hata pakuishi hawapaju"Homeless"

Elimu: NI kweli watu walilazimishwa kubadili dini ili waweze kujiunga na shule za missionari mfano mzuri ni Jaji wetu John Ramadhani na kuna kiongozi wa kani la kianglikani anaitwa Pia John Ramadhani na wengi weni tu.Sasa kama alikuwa hajali watu wake wapate elimu na kuacha mfumo ho je watanzania kweli wangesoma.Nyerer alifanikiwa Mengui sana na hat ahizo University ambazo tanzania tunaza sasa sio kama hawa viongozi wa leo wamezijenga bali ni vilevile vyuo alivyjenga kipindi cha utawala wake na viongozi wa leo kuzibadiisha kuwa university wakiwa walimu ni walewale na majengo ni yale yale mfano Mzumbe,Nyegezi,IFM,vyuo vya Uhasibu Arusha,DSA Mbeya,DSA Mtwara na DSA Dar hebu niambieni mpaka yeye kutoka madarakani kuna vyuo vingapi vipya vimejengwa?

Tanzania ilikuwa inatambulika hata kwenye Michezo leo hii ndio tunasema tumeendelea hakuna mwanamichezo yoyote ambaye anatam,bulika na hata kama yupo ni juhudi zake binafsi na sio program yoyote ya serikali.

Hospitali zilikuwa ni bure na Elimu sasa leo hii kila kitu kulipia ni jinsi gani watoto wa mlalahoi na mshahara kiduchu wataweza kusomesha watoto wao.Kumbukeni wingi wa Vyuo sio ndio watu ndio kuelimika.

Dear Popo,
You may be right, hayo yote hamna mtu aliyekubishia, and no adrenaline about Mwalimu. He was an intelligent guy who made the presidency; he influenced our foreign policy on top, he was admired, also I admire him. He was the most influencial president before Mandela in Subsaharan Africa.

Ok, tunataka kuelewa kwa nini hao watu ambao umewauliza wewe wote wanamlaumu Nyerere kwa elimu walizonazo na kuwa hawakupata oppotunities, you sould not igonre their ideas because you only think that, and because you have been succesful. Uliowauiza ni wengi, na kama wewe ni msomi (as i think from your comments above); haikutishi kuona segment kubwa kama hiyo ya pupulation inalaumu kuwa elimu opportunities haizikuwepo? Mie ningekuw wewe ningechambua hili suala. Inaogopesha.

Therefore hapa tunaungana ku-study a Cuase which made this Effect, then is there any solution. Mkandara kashasema anaogopa Tanzania inakwenda wapi. Ok wewe umekazana na ku-tuconvince at tuangalie yale mazuri aliyoyafanya na tuwalaumu hao vijana kwa kumlaumu Nyerere. We are coming from different backgrounds. Kwa hiyo take this issue as a National issue, wote lazima tuishi nchi hii hii, au wewe ushaamua kuwa hawa jamaa wanaolaumu Nyerere have to go to hell? There are many issues here.

Let us study other alternatives; kwa nini Nyerere ingwa alikuwa such intelligent, kwa nini hakuchukua easier route? Ni kweli shule kwa wakati ule zilikuwa hazitoshi; nakumbuka nilipongia kidato cha kwanya Tanzania zima ilikpasisha vijana 10,000 - 15,000, what is the number. Unajua leo Tanzania kuna Engineers wangapi? I bet if we have 3000. How many doctors we have? Sasa nyie mnaobisha hilo la vijana mko wapi? Tumetumia pesa nyingi hata kuwakomboa wengine. Nyerere alikataa religious institutes kuwekeza elimu only for special permits; what was the motive?
 
Uwekezaji ndugu yangu husingewezekana kwenye nchi ambayo ndio kwanza imepata Uhuru na hata hizo sera za uwekezaji wakti huo hazikuwepo kama sasa.Uwekezaji ulikuwa ni ule kama wa Zimbabwe na leo tunaona matatizo yake.Kulikuwa na ulaghai wa hali ya juu na sio uwekezaji kama unavyofikiria na leo hii pia umeona uwekezaji jinsi unavyoaffect nchi yetu, madini yote ambayo yanapatikana Tanzania tunapata asilimia 3% JE huo ndio uwekezaji?Hahahaa

You can be a fool even you go to school

Popo unaongelea era ipi mwenzangu? Nyerere aliondoa uwekezaji. Alitaifisha investment zote, na kuwaita hao wote mabepari. Kule kwetu Isimani alitaifisha hata mashamba ya wenyeji ambao walikuwa wanalima mahindi na ku-export. Fikiria walikuwa wanatosheleza chakula cha WaTanzania, na ku-export; are you there? Akataifisha mashamba ya Katani, Tumbaku yote hayo. Au unaongelea investment ipi tena? Investment ipo tangu kale. Unamsikiaga mtu mmoja anaitwa Mwamwindi? Aliambiwa lile shamba aliache ili liwe la kijiji; yaani shamba lilimwalo na mtu mmoja kwa kuwaajiri watu 200 litaifishwe na kupewa hao watu mia mbili. Badala ya hao watu miambili kupewa mapori wayafyeke na kucompete na huyo mtu mmoja.

Nenda kule Kilimanjaro same story, Ok he was doing for the well being of the country, is that true? That was what our education was telling us. But why he didn't choose another path? Competition? Simply he wanted to consolidate his grip on power!
 
Ila mnasahau kuwa wazazi waliruhusiwa kuanzisha shule za sekondari katika maeneo yao swali linabaki walilitekelezaje hilo. Mbona kilimanjaro walijenga, njombe walijenga shule za wanging'ombe, mtwango, N.K., Mfundi walijenga shule kibao hata mbozi walijenga angalau shule mbili Tunduma na Mbozi sekondari, maeneo mengi tu yaliruhusiwa kujenga. Tulikuwa wapi kutumia fursa hiyo? Pia serikari nayo ilijitahidi kujenga shule pia. Kwenye ujamaa shule hazikuruhusiwa kubagua watu kwa sababu tu ya kipato au imani kitu ambacho shule za makanisa zilikuwa zinafanya. Hivyo Nyerere hakuruhusu makanisa kujenga shule za kibiashara bali zile zilizohusiana na kuwaandaa watu wao kiimani kama seminary na ndio maana hakuzitaifisha. Kama mnakumbuka shule zilizotaifishwa ni za watu binafsi na za makanisa ambazo zilikuwa zinaendesshwa kibiashara. Je tuliitumia hiyo fursa ya kuanzisha shule katika maeneo yetu au tulibweteka tukawa tunasubiri atufanyie kila kitu?
 
Interested Observer,

..inaelekea hao jamaa waliohojiwa na Mheshimiwa Popo ni matokeo ya sera na mfumo wa elimu ya Mwalimu Nyerere.

..kwangu mimi hicho ni kigezo tosha kwamba mfumo wa elimu, au elimu waliyoipata/waliyopewa hao vijana inawalakini.
 
Kitu kingine ambacho tunashindwa kukilink ni utawala wa Mwinyi na kuyumba kwa elimu. Wakati wa Mwinyi ndio changes za kielimu zilipofanyika bila kuangalia madhara yake. Somo la sayansi ndio lilipata pigo kubwa, rejea kuanza kwa mitihani ya alternative to practicals, selikari iliacha kununua vitabu na madawa ya maabara. Ikawa ni furaha kwa kwenye nazo maana wakawa na uwezo wa kusoma shle binafsi na kwa maskini ikawa ni msiba maana ikawa ndio mwisho wa kupata elimu bora kwenye shule za selikari. Nakumbuka walimu waliotufundisha miaka ya mwishoni mwa miaka ya Themanini walikuwa wamebobea kwenye masomo yao, mpaka tukawa tunatamani kuwa walimu. Ukienda maabara, unafundishwa na kuelewa somo bila matatizo, lakini toka miaka ya tisini hiyo fursa imebaki kwa wanafunzi wanaosoma shule za private na sio private njaa.

Hivyo kuanza kulaumu inabidi ufanye assessment ya hali ya juu sana
 
Mwalimu Augustine Moshi,
Mkuu wewe utamlaumu mwalimu kwa sababu ya imani yako ya dini.. Ni sawa na Kaburu tu kwangu maanake sisi waislaam kabla ya shule hizi hazijachukuliwa tulilazimishwa kubadilisha dini, wengine tulibadili majina tu ili tupate elimu ya Msingi..Na mimi ni ushahidi tosha wa madai nayoyaweka..
Na kama unabisha nakuomba nambie jina la Muislaam hata mmoja aliyekuwa akisoma shule hizo bila kutengwa kutokana na dini yake sasa hawa walikuwa na tofauti gani na Kaburu!

Mkandara,
Nakubaliana na wewe kwenye suala la Nyerere kutaifisha shule ili watanzania wote wasome hata wale ambao siyo wa madhehebu ya zile shule. Lakini kuhusu kulaumu kwamba shule zilifanya watu wabadili dini, Mkuu wangu hiyo ndiyo ilikuwa njia ya kueneza dini. Waislam nao walikuwa na njia zao za kulazimisha watu waingie kwenye dini zao, kwa mfano wengine wazazi wetu waliingia kwenye uislamu ili wapate kuoa mama zetu. Bila kuwa muislamu hupati mke ilikuwa hivyo.

Kwa hiyo, kwa Nyerere (hapo lazima tumpe sifa zake) hakuwa mtu wa chini hivyo kuangalia wangapi wanalazimishwa kubadili dini, ila kwake suala lilikuwa Watanzania wangapi watasoma. Na alishapata kusema kwamba yeye ni Mtanzania kwanza kabla ya kuwa mkatoliki hivyo angetokea mtu mwingine na kumshawishi angeweza kubadili dini lakini siyo utanzania wake.
 
Interested Observer,
Mkuu napenda sana unavyo Observe issue hii na la msingi umezungmza kitu cha maana sana..
Bila shaka maelezo yangu yaliyotangulia yalitazama mawazo ya mw. Augustine Moshi na sio kutazama sababu ambazo hata mimi namlaumu mwalimu ktk Elimu..
Kifupi ni kwamba kila unayemfahamu analaumu elimu yetu kutokana na uchache wa nafasi za shule..kama sikosei only 7% ya wanafunzi wa shule za msingi ndio waliweza kwenda mbele kabla ya Uhuru hadi majuzi ktk utawala wa Mkapa..Na hesabu hiyo ilizidi kushuka kila unapopanda juu hadi kufikia asilimia 2 au 3 ya wanafunzi wanaomaliza chuo kikuu..Hii ni aibu kubwa sana kwetu sote pamoja na kwamba tunafikiri sisi wajanja wa kufika..
Watoto waliweza kwenda shule ya msingi alijitahiudi sana kuweza kufikia asilimia 98 lakini hakutayarisha shule za sekondary kulingana na ongezeko hilo.. Kwa hiyo hata kaa alichukua cshule zile au kutochumua bado hesabu ya wanafunzi kuingia kidato cha kwanza ingekuwa ndogo na lawama hizi zingeendelea kuwepo...
Kwa uhakika Hili ni tatizo la nchi zote za Kiafrika, pengine niseme ni tatizo la viongozi wote wa Kiafrika kushindwa kutazama vipaumbele vya nchi zao kulingana na mazingira waliyoyakuta ili kuleta mabadiliko..
Kwa wananchi hakuna vitu muhimu kama - Elimu, Afya, haki ya kumiliki Ardhi na Chakula..Vitu hivi ni vya mwisho ktk mtazamo mzima wa viongozi wa nchi za Kiafrika iwe Nyerere, Mandela au Kwame Nkurumah isipokuwa watu kama Ghadaffi, Idd Amin, Makaburu, Waisrael na washenzi wengine wote ambao kwa hakika hujali sana kuwaendeleza watu wao kulingana na mazingira wanayokabiriwa..Na itaendelea hadi kesho kwani hata Kikwete anajenga mashule bila kuwa na sababu ya ujenzi huo (adui) zaidi ya kufikia malengo ya hesabu (Quantity)..hivyo shule zinazidi kuongezeka lakini umuhimu wa shule na mazingira yetu bado ni tata kwani watu wanaenda shule ili wapate kuzungumza kiingereza zaidi ya kuelimika..

Pengine ni uhakika wa kujua kwamba hawapendwi wana maadui ambao wako tayari kuwakandamiza hivyo elimu, Afya na Ardhi na Chakula ni misingi ya ngome ya uhai wao sawa na jeshi lilipo vitani...Na nchi kama Tanzania kutokuwepa na Uadui, hali mbaya ya kutopendwa na makabila au Mataifa mengine kumetufanya kuviweka vitu hivyo nje ya vipaumbele ambavyo tumevifuata toka Nyerere hadi leo hii..

Hadi kesho binafsi nitaendelea kumlaumu Nyerere kwa kutoipa Elimu umuhimu wa kuongeza hesabu ya shule za Secondary, College na University, kiasi kwamba hata hesabu ya walimu wenyewe ilizidi kupungua kila mwaka. Wengi wa wanafunzi waliomaliza darasa la saba walilazimika kuingia shule za Private na wengine kwenda soma Uganda wakati fedha nyingi zilitumika dhidi ya Makaburu, adui tuliyemuona sisi..na kutangaza sana Ujamaa kwa sababu Ubepari pia alikuwa ni Adui wetu ktk itikadi hiyo ya kukopesha..
Lakini pamoja na lawama zote hiuzi ni muhimu sana pia tukumbuke kuwa dunia nzima iligubikwa na kawa hili la siasa za Mrengo.. Sisi wenyewe tulikuwa na uadui mkubwa na Kenya, Malawi na hata Uganda kwa sababu tu walikuwa na mrengo tofauti na sisi, tena basi naweza kusema EAC ilivunjika kwa sababu ya hizi imani za kisiasa. Kenya walituona Wajamaa na sisi tuliwaona Mabepari hivyo hapakuwepo na imani yoyote kati yetu..Tulitumia zaidi itikadi za kufikirika kama walivyotufungia hao Wachina na Wamarekani tukaamini kuwa kuna mmoja wao anayesema ukweli.. Kibaya ni kwamba leo hii Marekani na China wako karibu zaidi kibiashara kuliko hata Uingereza...wakati sisi adui wetu imekuwa vyama upunzani baina yetu sisi wenyewe na tunatumia mabillioni kujitenganisha lakini sio ktk ujenzi wa elimu bora nchini..

Yes, Nyerere alifanya makosa mengi tu lakini sio hili la kuchukua shule za misheni ambazo kulingana na wakati ule shule hizi zilikuwa shanga za kuwavuta watu ktk imani hiyo ya dini...It was wrong na wasingeweza kubadilika.. sasa fikirieni Tanzania hii ingekuwa na only 2 percent ya Waislaam waliosoma wakati wana represent 1/3 ya population ya nchi.. Kungekalika kweli!..
 
Interested Observer,

..inaelekea hao jamaa waliohojiwa na Mheshimiwa Popo ni matokeo ya sera na mfumo wa elimu ya Mwalimu Nyerere.

..kwangu mimi hicho ni kigezo tosha kwamba mfumo wa elimu, au elimu waliyoipata/waliyopewa hao vijana inawalakini.

Unaacha scenario nyingine kuwa mtu mwenyewe anaweza kuwa chanzo cha tatizo na isiwe mfumo. Ila kwa kujifariji wanasingizia mfumo. Mfano mtu aliyefeli hata katika mfumo ambao ni efficient, pamoja na kuwa alikuwa hana uwezo au alikuwa hajibidiishi atasingizia kuwa ilikuwa bahati mbaya. Pia msisahau kuwa sio kila mtu anatakiwa awe na degree ndio aendeshe maisha, milango ya maisha ipo mingi sana kama mmoja ukifungwa jaribu mwingine. Nakumbuka kuna mzee mmoja hakuchaguliwa kwenda sekondari lakini alikubari kwenda mafunzo ya ualimu grade C. Kwa vile alikuwa na nia ya kujiendeleza, leo hii ni professor. Hakukaa na kulaumu mfumo bali alitafuta njia ya kuboresha maisha yake.

So sometimes people themselves are part of problems for not doing something to solve the problem facing them
 
Ndugu pia tusisahau kuwa elimu mahali popote ni pyramid, wengi chini, wachache juu. hata tungejenga Vyuo vikuu nchi zima hizo degree tutakuwa tunatoa tuu bila kuangalia uwezo, mbona tumejenga sekondari kila kata lakini tumesikia kuwa kuna shule zimefungwa kwa sababu yakukosa wanafunzi wenye sifa. Wanafunzi katika kata husika waliofaulu hawakufikia hata robo ili kujaza darasa. Hata kama ni raslimali za kuendesha shule mnazo ndio za kuchezea kuendesha shule yenye wanafunzi watano?
 
Nilisahau kitu kikingine, katika wakati huu kuna wazazi walikuwa wanawaambia watoto wao wajifelishe ili wazazi wasilipe sh. 20,000 ya ada. mara nyingine watoto wenyewe wanajifelisha ili waoe au waolewe. Kama watu wanaujinga wa namna hiyo wakati huu, je wakati wa Nyerere ujinga ulikuwaje? watu si walichapwa viboko ili wahudhurie shule? Ujinga wote huu uliokuwepo watu wanasahau na wanaishia kumlaumu Mwalumu.
 
Popo said:
Kiswahili: Niambieni ni nchi ngapi za Afrika viongozi wake wanaweza kuongea kiigereza kwa ufasaha na hivi juzi tu kuna mbunge mmoja wa nertheland alifanya reseach na kupitia nchi kama south Afrika na kenya ambazo ndio zinaonekana watu wanaongea kingereza kizuri bado akakuta watu wengi hawafahamu maneno mengi tu ya kiingereza kwa sababu Lugha ya kiingereza ni "second Language" kwao na alipopita Tanzania alishtuka sana kuona watu wote bungeni wanatumia lugha moja na kila mtu anaweza kujielezea kwa ufasaha na hata asiyesoma anaweza kuelewa. Hivi Nyinyi watu mnataka kuniambia Zambia ambayo Kiingereza ndio lugha ya Taifa watu wote wanaongea kiingereza mpaka kijijini.

Huu ndio ujinga mkubwa wa mwafrika kufikiri kiingereza au kujua kiingereza ndio kuelimika.Wachina,wajapani,wacanada na nchi zote za European Union isipokuwa UK wote wanazungumza lugha zao wenyewe na nchi zote hizo zimeendelea kupita hata hiyo UK, Ndugu zangu kiingereza hakina impact yoyote kwenye maendeleo ya nchi na ukitaka kufahamu hilo mchukue msomi yoyote unayemjua wewe ambaye amekulia Afrika na kusoma Afrika uone kama anaweza kuongea au kujielezea kama Tony Blair anavyoweza kujielezea.Swala la lugha halina msingi wowote na ndio maana hata viongozi wengine wengi tu duniani hawajui hata neno lolote la kiingereza na bado wanashiriki kwenye mikutano ya kimataifa kwa kuongea lugha zao.

Watanzania inabidii tufikirie kwa makini sana ni nini yule Mzee alivyokuwa anafanya na sio kulaumu pasipo sababu za msingi, wengi wanafikiria Ulaya watu wengi ni matajiri na hakuna masikini, sio kweli hata kidogo kuna watu ulaya hata pakuishi hawapaju"Homeless"

Tanzania ilikuwa inatambulika hata kwenye Michezo leo hii ndio tunasema tumeendelea hakuna mwanamichezo yoyote ambaye anatam,bulika na hata kama yupo ni juhudi zake binafsi na sio program yoyote ya serikali.

Hospitali zilikuwa ni bure na Elimu sasa leo hii kila kitu kulipia ni jinsi gani watoto wa mlalahoi na mshahara kiduchu wataweza kusomesha watoto wao.Kumbukeni wingi wa Vyuo sio ndio watu ndio kuelimika.

Popo,

..huyo mtaalamu wako ungemuuliza kuhusu uwezo wa wa-Tanzania ktk lugha ya Kiingereza.

..inavyoelekea alipokuwa Kenya na SA alichunguza uwezo kwa wananchi wa nchi hizo ktk kuzungumza Kiingereza.

..lakini alipofika Tanzania akaachana na Kiingereza, akaanza kuchunguza uwezo wetu ktk kuzungumza Kiswahili.

..labda utueleze kama kiwango cha wa-Tanzania ktk kujieleza kwa Kiingereza kimeongezeka au kupungua tangu Mwalimu aingie madarakani. halafu tueleze sababu za ongezeka/mapungufu uliyoyaona.

..tunachanganya madawa kutumia lugha mbili ktk mfumo wetu wa elimu. zaidi kuchelewesha kuwafundisha wanafunzi Kiingereza, na kuanguka kwa viwango vya taaluma vya waalimu wetu wa Kiingereza, kunadumaza mfumo mzima wa elimu yetu.

..ni nani alisema "KIINGEREZA NDIYO 'KISWAHILI' CHA DUNIA?" sasa tuizingatie kauli hiyo. tunapokuwa wenyewe ndani ya Tanzania we feel like we doing just fine. problems arise when we have to interact with outside world.

Popo said:
Elimu: NI kweli watu walilazimishwa kubadili dini ili waweze kujiunga na shule za missionari mfano mzuri ni Jaji wetu John Ramadhani na kuna kiongozi wa kani la kianglikani anaitwa Pia John Ramadhani na wengi weni tu.Sasa kama alikuwa hajali watu wake wapate elimu na kuacha mfumo ho je watanzania kweli wangesoma.Nyerer alifanikiwa Mengui sana na hat ahizo University ambazo tanzania tunaza sasa sio kama hawa viongozi wa leo wamezijenga bali ni vilevile vyuo alivyjenga kipindi cha utawala wake na viongozi wa leo kuzibadiisha kuwa university wakiwa walimu ni walewale na majengo ni yale yale mfano Mzumbe,Nyegezi,IFM,vyuo vya Uhasibu Arusha,DSA Mbeya,DSA Mtwara na DSA Dar hebu niambieni mpaka yeye kutoka madarakani kuna vyuo vingapi vipya vimejengwa?

..wako waliolazimishwa kuingia Ukristo ili kupata elimu, lakini pia wako Waislamu ambao walisomea shule za misheni bila kulazimika kubadili dini zao.

..Uislamu na Ukristo ni imani za kuletewa tu. hakuna mwenye ushahidi kwamba hao waliokuwa Waislamu wakalazimishwa kuwa Wakristo, waliacha imani za mababu zao na kuingia Uislamu kwa hiari yao.

Popo said:
Tanzania ilikuwa inatambulika hata kwenye Michezo leo hii ndio tunasema tumeendelea hakuna mwanamichezo yoyote ambaye anatam,bulika na hata kama yupo ni juhudi zake binafsi na sio program yoyote ya serikali.

Hospitali zilikuwa ni bure na Elimu sasa leo hii kila kitu kulipia ni jinsi gani watoto wa mlalahoi na mshahara kiduchu wataweza kusomesha watoto wao.Kumbukeni wingi wa Vyuo sio ndio watu ndio kuelimika.

..sidhani kama ushindi wa kina Filbert Bayi,Suleiman Nyambui,Gidamis Shahanga, Nzael Kyomo,etc tunaweza kuulinganisha na jinsi Wakenya au Waethiopia wanavyo-dominate mbio ndefu sasa.

..kwa mtizamo wangu Bayi na wenzake walishinda kwa kutegemea vipaji vyao vya kuzaliwa kuliko program na mikakati wa sera ya michezo za wakati ule.

..kwenye mpira wa miguu tulifika fainali za Kombe la mataifa ya Afrika mara moja tu --1981. Kenya wana rekodi ya kushinda kombe la challenge, tena wakati wa utawala wa Mwalimu, mara nyingi kuliko Tanzania. katika mashindano ya vilabu ya Afrika tulikuwa hatuwezi kuvuka raundi ya pili.

..ukiritimba wa habari ndiyo unaowafanya wa-Tanzania waamini kwamba walikuwa zaidi ya nchi nyingine wakati ule. soka letu lilikuwa chini kuliko hata la nchi ya Zaire iliyoongozwa na mwendawazimu Mobutu Sese Seko.

..ELIMU HAIKUWA BURE, ILILIPIWA KUTOKANA NA KODI WALIZOKATWA WANANCHI, MIKOPO NA MISAADA TOKA NJE.
 
Last edited:
" I was in Washington last year. At the World Bank the first question they asked me was `how did you fail?' I responded that we took over a country with 85 per cent of its adult population illiterate. The British ruled us for 43 years. When they left, there were 2 trained engineers and 12 doctors. This is the country we inherited. When I stepped down there was 91-per-cent literacy and nearly every child was in school. We trained thousands of engineers and doctors and teachers. In 1988 Tanzania's per-capita income was $280. Now, in 1998, it is $140. So I asked the World Bank people what went wrong. Because for the last ten years Tanzania has been signing on the dotted line and doing everything the IMF and the World Bank wanted. Enrolment in school has plummeted to 63 per cent and conditions in health and other social services have deteriorated. I asked them again: `what went wrong?' These people just sat there looking at me. Then they asked what could they do? I told them have some humility. Humility - they are so arrogant!" - Mwalimu Nyerere, 1998
 
Elimu ya bure ya kujifunza kusoma na kuandika.

Ingekuwa bora kusomesha watu wachache vizuri kuliko kusomesha watu wengi roborobo.

Sijui kwa nini serikali haikuamuru wananchi kujenga shule za secondari ili kuongezea nguvu juu ya zile za makanisa na vyama vya ushirika na nyinginezo?

Kutaifisha shule ulikuwa ni uhuni mkubwa uliokwenda kinyume na historia ya elimu duniani.

Kufuta somo la Kiingereza katika kufundisha nalo lilikuwa ni pigo kubwa katika kutoa elimu ya maana.
Vitabu vingi vyenye maarifa hata yale ya kiwango cha darasa la 7 havipo katika lugha ya kiswahili.
Lugha siyo elimu, lakini kufundisha katika lugha isiyojitosheleza kimsamiati ni sawa na kushindwa kabla ya kuanza.
 
This is very interesiting,

Title ya Mada "Kwanini Watanzania wanamlaumu Mwalimu Nyerere kwa kukosa Elimu"

....ukiisoma article ilivyoandikwa na mtoa mada utaona kuwa "Kumlaumu Mwl Nyerere ni UNAFIKI wa aina fulani.....hakuna aliyejibu maswali ya msingi ya mtoa mada ili kujustify lawama towards Mwl Nyerere.

Vivyohivyo na hapa JF watu wanashindwa kuleta justification za kutoa "same" lawama towards Mwl Nyerere.....simply because HAKUNA.........especially kwenye hii mada so far

Kuna maswaliya ujiuliza kutokana na mada
1. Je Mwl Nyerere alifanya juhudi ili wananchi wake wapate elimu?...Jibu ni absolutely YES.....hata hao wanompinga hapa JF watakubaliana nami...vinginevyo nitawaita WANAFIKI...pengine waniambie hawajui juhudi za Mwl.

2.Je, watu kukosa elimu wakati wa kipindi chake Mwl Nyerere.....je anastahili lawama......This can only be debated with facts.

3. Je ni kweli Mwl Nyerere alikataza uanzishwaji wa shule Binafsi kama ilivyodaiwa hapa........?....the answer is NO

4.Je Mwl Nyerere "kuchukua" (still debatable) mashule ya mission kulisababisha watu kukosa elimu? in addition kama kweli nia yake ilikuwa kuua juhudi za mission WHY aliacha shule zingine za mission ziendelee?........Jamani tuache ku-concoct propaganda kuwa eti Mwl "alinyang'anya na kukataza" shule za watu binafsi....naombeni muongee facts na si majungu.........
MWALIMU JKN HAKUKATAZA SHULE BINAFSI..........ILA ALIKATAZA UBAGUZI NA ALIAGIZA SHULE ZOTE ZA KIDINI (MISSION) KUKUBALI WANAFUNZI WOTE BILA KUANGALIA DINI ZAO WALA RANGI ZAO.......

Lugha ya Kiswahili
Again........Ni vyema tukapata/establish facts za kwa nini Mwl alihamasisha sana hii lugha mashuleni..............na siyo kusema tu ooohh Mwl alitufanya tusijue kiingereza....thats very vague argument......

Mkuu Bob Mkandara,
Tuko pamoja Mkuu.....unajua binafsi ya mtu ni kitu cha ajabu sana.......watu wanasahau!!............yes Mwl alikuwa na mapungufu yake.....lakini tuwe honesty..at least when looking at ourselves..........dah
 
andindile said:
Unaacha scenario nyingine kuwa mtu mwenyewe anaweza kuwa chanzo cha tatizo na isiwe mfumo. Ila kwa kujifariji wanasingizia mfumo. Mfano mtu aliyefeli hata katika mfumo ambao ni efficient, pamoja na kuwa alikuwa hana uwezo au alikuwa hajibidiishi atasingizia kuwa ilikuwa bahati mbaya. Pia msisahau kuwa sio kila mtu anatakiwa awe na degree ndio aendeshe maisha, milango ya maisha ipo mingi sana kama mmoja ukifungwa jaribu mwingine. Nakumbuka kuna mzee mmoja hakuchaguliwa kwenda sekondari lakini alikubari kwenda mafunzo ya ualimu grade C. Kwa vile alikuwa na nia ya kujiendeleza, leo hii ni professor. Hakukaa na kulaumu mfumo bali alitafuta njia ya kuboresha maisha yake.

So sometimes people themselves are part of problems for not doing something to solve the problem facing them

..off course kuna wakati tatizo ni la mwanafunzi.

..lakini tatizo likiwa kubwa zaidi, na ukaona idadi kubwa ya wanafunzi wanafeli, basi watu lazima wahoji mfumo uliopo.

..mfano: wanafunzi wengi sasa hivi hawaimudu lugha ya Kiingereza. je, tatizo ni wanafunzi au mfumo wetu wa ufundishaji lugha hii?
 
Ogah said:
4.Je Mwl Nyerere "kuchukua" (still debatable) mashule ya mission kulisababisha watu kukosa elimu? in addition kama kweli nia yake ilikuwa kuua juhudi za mission WHY aliacha shule zingine za mission ziendelee?........Jamani tuache ku-concoct propaganda kuwa eti Mwl "alinyang'anya na kukataza" shule za watu binafsi....naombeni muongee facts na si majungu.........
MWALIMU JKN HAKUKATAZA SHULE BINAFSI..........ILA ALIKATAZA UBAGUZI NA ALIAGIZA SHULE ZOTE ZA KIDINI (MISSION) KUKUBALI WANAFUNZI WOTE BILA KUANGALIA DINI ZAO WALA RANGI ZAO....

Ogah,

..hivi ilikuwa haiwezekani kukataza huo ubaguzi bila kutaifisha hizo shule?

..yaani unataifisha shule ya Kanisa, halafu unawaambia wajenge nyingine?

..binafsi nasikitishwa na the fact kwamba Mwalimu alitaifisha shule zikiwa na hali nzuri. by the time anaondoka madarakani shule alizotaifisha zilikuwa ktk hali mbaya sana.
 
Back
Top Bottom