Kwanini Watanzania wengi hawapendi kucheza na kuwajali wanyama wanaowafuga?

Hapana kwa hilo ninakupinga, wenzetu majuu wapo ambao waliochoka mbaya lakini kwenye suala la wanyama huwa wanajali kiasi cha kumuona ni mwanafamilia, mtu anaweza akawa kachoka mbaya lakini hawezi kuuza mbwa ama paka wake, binafsi mbwa ama paka wangu hata ulete milioni 5 siwezi kuzichukua nafsi itanisuta kwa usaliti.
Nina uhakika huwanunulii/kuwapikia chakula maalum, huwapi chanjo, huwapeleki kupimwa mara kwa mara, huwalipii mafunzo maalum, huwapi dawa za kuua wadudu kwasababu kipato ni changamoto.
 
Wengine akiona mbwa, paka, kunguru yeye ni kuokota jiwe na kumbonda hata bila sababu yoyote ya msingi.

Yaani basi tu, tena ikiwa usiku ndo kabisaa anaweza hata kumkimbiza ampige mawe na akizidiwa anamuua kabisa hata bila sababu za msingi.

Binafsi hata wadudu kama hawanidhuru nawaacha tu waishi. Mdudu ninaemuua ni mbu na nzi, hawa kwakweli wanakera na hii mikoa ya joto hawaepukiki kwa sisi wakata ufuta.
 
Mkuu nipe faida ya kumwandalia mazingira mazuri ya kimchinja mbuzi au kuku?
Mimi ni mfugaji lkn kwenye kuchinja naogopa sana na nawaonea huruma sana Huwa najitajid sana kukwepa. Hivo sioni mantiki ya kuandaa mazingira mazuri ya kuua kiumbe mwenzio

Kuhusu kupeti peti mbwa na paka u esahau kitu kimoja
Hapa ni bongo sio Paris Wala London mzee. Ni hayo tu ukiihitaji yaendelee tutaendelea
 
Unachosema ni sahihi yani mtu anakutana na mbwa barabarani anaokota jiwe anamtwanga nalo bila hata sababu ya msingi, nafikiri pia malezi yana play role kubwa hapa.... nafikiri ifike wakati zitungwe sheria zitakazoadhibu watu wenye tabia kama hizi, wanyama nao wana haki.
 
Sawa ni bongo, kwanini ufuge kiumbe ambacho umedhamiria kukitesa? Sawa jamii zetu za kiafrica huwa tunafuga mbwa kwa ajili ya ulinzi, hivyo kumuweka bandani ni sawa kwa sababu mbwa akizoeana na wageni anakosa ukali, ila pia kumhifadhi mbwa ndani ya nyumba ya kuishi kunahitaji usafi wa hali ya juu kwa mfugaji kwa kumzingatia huyo mbwa, ila kama umeamua kumfuga bandani basi hakikisha mazingira ni safi, pia mpe mlo mzuri, mtibu pale panapohitajika.....tukija kwa paka, paka anapenda kukaa karibu na binadamu ndio maana mara nyingi utamkuta yupo karibu na mfugaji wake au amelala kwenye sofa au yupo mazingira ya ndani, na pia paka ni wasafi huwa hawajisaidii hovyo hovyo pahala pasipotakiwa....kwanini paka huyu umtese kwa kumfukuza nje mara zote wakati umeamua kumfuga mwenyewe?
 
Tanzania wanyama tunaoishi nao wanateseka sana kwakweli, ni kama vile waliumbwa na shetani wakati tumeumbwa nao na Muumba wetu alietupa mamlaka tumsaidie kuwatunza, Watanzania tunasali sana na kuomba dua ila ya nini hivi vyote kama hatupo tayari kuukubali uumbaji wa viumbe vingine vilivyoumbwa na Baba wa mbinguni / Allah?

Ni mwaka unaisha sasa paka wako hujawahi hata kumpa zawadi ya samaki mzima.

Ni mwaka unaisha sasa mbwa wako hujawahi kwenda buchani umnunulie kilo ya nyama umchomee ama umchemshie.

Mbuzi ama kuku umemnunua wa kumchinja, yafaa umtendee haki walau kwenye safari yake ya mwisho umuandali malazi safi, chakula na maji viwepo, kisha kesho yake umchinje, si sawa apigwe na mvua ama upepo wa el nino, chakula umbanie na maji anywe kwenye vyombo vichafu kisha kwa unafki eti umuombe Mungu kabla ya kumchinja.

Paka ama mbwa kakuzoea hujawahi hata kukaa nae sehemu kumpeti peti, akija unamwambia tokaa, yupo kwao tayari aende wapi?

Mbwa wako kakuzoea hujawahi hata kucheza nae michezo ya kukimbizana ama mpira

Mbwa yumo kwenye banda kila siku, hujawai kutembea nae hata siku moja jioni

Waafrika ni viumbe waajabu sana[emoji28][emoji28]
 
Mkuu hakuna mfugaji anaetesa mbwa wake sema mlichokisema ndo hakipo Kwa maisha ya watanzania wengi kweli kabisa uchomoe Hela ukanunue samaki mzima Kwa ajiri ya paka au mbwa maisha hayo hatuna Mimi ni mfugaji kabisa na kuku mbuzi nk lakini hata tukichinja mbuzi siwezi chukua kilo nzima nimpe mbwa never! Yeye kama ni mkali akawinde huko Kuna wanyama kibao Hadi ngendere nitamchomea vzr tu ale ashibe lkn si kununua nyama na kumpeti peti huo muda Sina mkuu paka awinde panya awezavyo Kuna panya kibao zinakula mazao yetu halafu nitoe hela ninunue samaki hapana kwakweli hayo ni maisha yenu ya mjina unafuga tu Kwa ajiri ya kumwangalia majuzi tu nimeambia watu waue paka alikuwa anakula vifaranga pamoja na kwamba anakunywa maziwa panya wapo lkn anaona awinde vifaranga wangu wa kuku.
 
Kasema hata kuku ukitaka kumchinja kamnunulie chakula kizuri, mtandikie kitanda kizuri halafu kesho yake ndo umchinje.
[emoji23][emoji23][emoji23] eti ukiandalie mazingira mazuri ya kukiua nadhani jamaa huyu sio mfugaji ila anafurahisha ukumbi tu asee. Mgeni kaja chapu jion huo muda wa kuandaa utoke wapi[emoji38][emoji38]
 
Unachosema ni sahihi yani mtu anakutana na mbwa barabarani anaokota jiwe anamtwanga nalo bila hata sababu ya msingi, nafikiri pia malezi yana play role kubwa hapa.... nafikiri ifike wakati zitungwe sheria zitakazoadhibu watu wenye tabia kama hizi, wanyama nao wana haki.
Mbwa njiani anafanyaje? Manake huyo mbwa ni mzurulaji sharti apigwe ikiwezenzekana auawe tu vipi akiuma Watoto? Matukio mangapai ya mbwa wenye kichaa mtaani hujeruhi watu? Sema Sheria itungwe Kwa mfugaji wa huyo mbwa kuwa akimuachaniza aajibishwe lkn kumpiga mbwa mzurulaji ni Haki yake ya kikatiba kabisaaa
 
Wengine akiona mbwa, paka, kunguru yeye ni kuokota jiwe na kumbonda hata bila sababu yoyote ya msingi.

Yaani basi tu, tena ikiwa usiku ndo kabisaa anaweza hata kumkimbiza ampige mawe na akizidiwa anamuua kabisa hata bila sababu za msingi.

Binafsi hata wadudu kama hawanidhuru nawaacha tu waishi. Mdudu ninaemuua ni mbu na nzi, hawa kwakweli wanakera na hii mikoa ya joto hawaepukiki kwa sisi wakata ufuta.
Mkuu zingatia Hilo mbwa na paka wanafugiwa barabarani? Kumpiga mbwa mzurulaji ni namna fln ya kujihami asije kukujeruhi
 
Tanzania wanyama tunaoishi nao wanateseka sana kwakweli, ni kama vile waliumbwa na shetani wakati tumeumbwa nao na Muumba wetu alietupa mamlaka tumsaidie kuwatunza, Watanzania tunasali sana na kuomba dua ila ya nini hivi vyote kama hatupo tayari kuukubali uumbaji wa viumbe vingine vilivyoumbwa na Baba wa mbinguni / Allah?

Ni mwaka unaisha sasa paka wako hujawahi hata kumpa zawadi ya samaki mzima.

Ni mwaka unaisha sasa mbwa wako hujawahi kwenda buchani umnunulie kilo ya nyama umchomee ama umchemshie.

Mbuzi ama kuku umemnunua wa kumchinja, yafaa umtendee haki walau kwenye safari yake ya mwisho umuandali malazi safi, chakula na maji viwepo, kisha kesho yake umchinje, si sawa apigwe na mvua ama upepo wa el nino, chakula umbanie na maji anywe kwenye vyombo vichafu kisha kwa unafki eti umuombe Mungu kabla ya kumchinja.

Paka ama mbwa kakuzoea hujawahi hata kukaa nae sehemu kumpeti peti, akija unamwambia tokaa, yupo kwao tayari aende wapi?

Mbwa wako kakuzoea hujawahi hata kucheza nae michezo ya kukimbizana ama mpira

Mbwa yumo kwenye banda kila siku, hujawai kutembea nae hata siku moja jioni
KWA HII TREAD NZURI INABIDI SASA NIANZE KUWAPENDA SANA WAMNYAMA KAMA UNAVYO WAPENDA WEWE
 
Back
Top Bottom