Kwanini Watanzania wengi hawapendi kucheza na kuwajali wanyama wanaowafuga?

Namba 3 ni very true na ushahidi ninao miaka fulani mbwa wangu alishawahi kuniokoa kwenye issue ya hatari sana kwa kuja kunishtua kwa hali ya kitofauti ambayo sikuizoea kabla.

Pia nimefuga mbuzi na ng'ombe hawa nilicheza nao kiasi hata nilipokuwa nikiingia nyumbani nikifungua geti shingo zote kama wanataka kutoka bandani kunikimbilia mbuzi na ng'ombe wote japo hawakuwa wengi niliwapa majina na walikua wanayajua nikiwaita unaona response burudani kubwa niliipata kwa mbuzi kwa michezo michezo ya kukimbizana pale nikiwa free na kuruka wanavyoruka.

Hadi leo mtu nikiona anapiga mnyama sifurahii kabisa.
 
Duh
Ana hoja, asikilizwe
 
Nchi yetu ingekuwa serious na sheria, watu wengi sana wangefungwa jela kwakuwa ipo,animal welfare act inayosimamia yote aliyoandika mdau ikiwemo chakula na malazi ya wanyama.
 
Mi nawapenda njiwa wangu, nawanunulia choroko na mtama wainjoi, wakiona tu nmebeba container wananifata....siwarushii tu nakaa chini kabisa wanasogea karibu kula.

hao paka mbwa hapana aseee huko sipo sina hobby nao mie
Unafugia mkoa gani hao njiwa?
 
Kuna ile kauli "lete jiwe...lete jiwe"

Binafsi napenda pets, hasa mbwa, ni company nzuri lakini pia ni mlinzi mzuri wa nyumba na master wake pia.
 
Jana tu nlikuwa nmekaa sehemu,ghafla mbws akapita zake,jamaa akaokota bonge la jiwe anataka kumrushia,hadi nikamzuia..Its so sad,na hali hii ni kubwa sana mitaani kwetu. Wanyama hasa mbwa na paka wanateseka sana aisee!
 
Maskini tangu lini akawa na upendo yeye mwenyewe hajipendi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…