Kwanini Watanzania wengi hufukuza ama kupiga wanyama bila sababu?

Kwanini Watanzania wengi hufukuza ama kupiga wanyama bila sababu?

Aisee hatari sana na nina uhakika hata hapa Tanzania mapolisi wengi ni vichaa ila ndiyo hivyo tena hawajijuwi

Wengi ni laana na uporaji wa mali za masikini na wengine msongo wa mawazo unachangia
Hawana maisha mazuri na kwa kuwa wanachukiwa inakuwa vigumu kujichanganya na watu wa kawaida
 
Kero ya paka ni kwamba huwa anaajiona yeye ndio anakumiliki wewe, vile anavyoona unamlisha, unamshika shika, n.k anaona yeye ndie bosi wako, yani inafikia kipindi kama siku mnapika samaki na yeye mmempa dagaa, hatakula hizo dagaa [emoji23] atasubiria samaki hao mnaowaunga ama kuwakaanga. [emoji23][emoji23][emoji23] ubaya wa paka mwengine ni kwamba mda wowote anaweza kuondoka hapo kwenu anarudi baada ya miezi ana mimba [emoji23][emoji23]

Kwa mbwa tayari huwa anajua wewe ndie master / mmiliki wake, inakuwa rahisi hata kufundishika, ila sasa wabongo wengi wanatesa mbwa wao.
Mimba tena, mi nafukuzia mbali
 
Kuna wale paka wanaofugwa na kurandaranda kwenye pub au migahawa ya uswahilini. Kila wakiona mteja kapewa huduma ya chakula nao usogea miguni wakivizia wadondoshewe chakula. Uwa najiuliza kama hao paka ni wa wamiliki wa hizo pub au migahawa ambao wapo pale kwa lengo la kukubiliana na panya kwa nini wasiwe wanawaandalia hata makombo ya chakula kilichobakizwa na wateja kwa kuwawekea sehemu yao maalumu ili wasiwe wanawabugudhi wateja kwa kuwazongazonga miguuni? Maana mteja kula chakula huku kamkaushia paka anaemzongazonga huku akilia nako kunamletea aibu mbele ya wateja wengine na akisema ampe sehemu ya chakula alichohudumiwa kama ni kidogo basi yeye anaweza asishibe.
Mi huwa namaliza nyama zote afu namtupia mfupa tupu
 
Hatuna hela za kujikimu,stress tulizonazo tunahamishia kwa wanyama.
 
Umenikumbusha miaka ya utotoni jirani yetu karudi shamba saa tisa mchana huku kabeba samaki wake wa kukaanga ili wapike ugali wa mchana baada ya kazi ngumu ya shamba. Baada ya kuingia nyumbani kwake na vijana wake na kuweka samaki mezani jikoni ili mapishi yaanze huko nje ikatokea tafrani (ugomvi) majirani zake wanapigana baada ya kuitana wachawi, jamaa na vijana wake wakakimbilia ugomvi huko nje. Baada ya ugomvi kwisha na yeye kurudi ndani akakuta paka ndiyo anamalizia kutafuna samaki wa mwisho. Kwa hamaki jamaa na vijana wake wakafunga milango na kufanikiwa kumkamata yule paka. Adhabu waliompa ni kumwagiwa mafuta ya taa na kumuwasha moto!! Basi paka akachomoka huku anawaka moto mbio akapanda ukutani nyumba ya jirani ya nyasi, na mara nyumba yote ikaanza kuungua moto na mwishowe kuteketea yote na mahindi yaliyokuwepo darini.. [emoji23] [emoji23]
Waliwezana
 
Mi mbwa na paka sitaki waona karibu ni kuwawinda tu. Kuna mbwa niliwahi mpiga tofali hatanisahau

Ukienda India utashangaa sana Yaani kuna mbwa wengi unaweza sema wako idadi moja na hawapigwi
Wanaishi na wanyama wote in harmony
Ndege wanakuja mpaka karibu yako ukiwa garden

Nimependa wanavyoishi nao
 
Hebu chukulia mfano yanayoendelea Ukraine, mtu unamkuta anaenda kutafuta hifadhi pamoja na mnyama wake, leo hii sitashangaa hapa kwetu mtu akihamia hata mtaa wa nne basi atamtelekeza mbwa wake.

kuwatesa wanyama ni kumtemea mate usoni Mwenyezi Mungu alieumba viumbe vyote,

kuna hizi tabia mbaya sana zimezoeleka na watanzania wengi kwa wanyama 👇👇

-unakuta tu mtaani mbwa anajipitia zake, mtu anaanza kumrushia mawe.

-nyumbani kwako unafuga paka, ukimualika mgeni anaanza kumfukuza sshh tokaa!! aende wapi sasa wakati hapo ni kwao ?

-Mtu kavimbiwa nyama, zile zilizobaki ambazo hata hajazila anaenda kutupa badala ya kumpa hata mbwa au paka wanaeishi nae

-kuku yupo bize anatafuta chakula, mara mtu anaanza kumkimbiza tu bila sababu.

-Mbuzi ameletwa kwajili ya nyama ya sherehe, usiku umefika anaachwa ukutani, yani mtu hata hajali kama kuna baridi, mvua, mbuzi angalau apumzike vizuri siku yake ya mwisho, n.k.

-usiombe kukutana na mtu anatumia ng'ombe kulima, yani hizo stiki huyo ng'ombe anazokula na matusi juu ni balaa.

-Dume limempanda jike, mtu anaanza kuwarusha mawe.

-mbuzi analia meee meee kwavile ndivyo alivyoumbwa, mtu anachukia anaenda kumpiga.

-Punda anabebeshwa mizigo mizito yani hata kutembea inakuwa shida lakini mtu wala hajali.

-Mbwa kila usiku anakulinda wewe, familia yako na mali ila kibanda chake hakijasafishwa mwaka mzima kimejaa viroboto, chakula chake ni makombo kila siku, yani mtu hajiongezi hata kumpa nyama mara moja kama shukrani ya ulinzi

Ila sisi tuliokulia kwenye ufugaji, ngombe, kondoo, mbwa, mbuzi ni sehemu ya familia. Tena unawaita kwa majina yao.
 
Kunguru mpumbavu lazma nimtie kitofa😅 ananyea gari langu makusudi kabisa
Kuna kipindi alinyeaga bakuli la supu ,,nimetoka kitaa kuchukua supu napita chini ya waya za umeme akaachia kitu.........hawa ndege wana tabia za kihunihuni tu kama wakazi wengine wa hili jiji
 
Back
Top Bottom