Habari wana JF
Kuna kitu nimekuwa nikikiona mara kwa mara kwa wateja wanakuja kuulizia bidhaa dukani.
Mteja baada ya salamu anauliza kwa kutumia wingi, hata kama anahitaji kitu kimoja tu.
Mfano:
•Hivi mna pump za Pedrollo?
•Mna taa za Tronic?
•Mna pipes za PVC?
•Mna switches za umeme?
•Mna tiles za rangi hii?
•Mna tank za maji?
•Mna rangi za kupaka ukuta?
•Mna mashine za welding?
•Mna vifaa vya plumbing?
•Mna solar panels?
•Mna CCTV cameras?
•Mna extension cables?
Lakini kiuhalisia, mara nyingi anahitaji kitu kimoja tu.
Pia kuna kitu kingine cha kuvutia zaidi 👇🏻
Karibu wateja wote hutumia neno “mna” badala ya “una”
Mfano:
•Mna pump?
•Badala ya kusema: Una pump?
Swali linakuja:
👉 Huyu mteja ana uhakika gani kwamba hili duka ni la watu wengi (partnership) na sio mtu mmoja tu ndo mmiliki (single entity)
Au kwanini automatic anachagua kutumia “mna”?
Je inaweza kuwa:
•Ni lugha ya heshima (formal tone)?
•Ana-assume biashara ina team hata kama ni mtu mmoja?
•Ni njia ya kuonyesha seriousness ya manunuzi?
•Au ni mazoea tu ya mawasiliano ya kibiashara?
Kwa upande wangu naona hii ina reflect psychology ya mteja + communication habits ambazo wengi hatuzifikirii kwa undani.
👉 Ninyi mnaonaje? Wale wanaopokea simu kila siku, mme-notice hili?
Karibuni tushare uzoefu na mawazo 👇🏻