Kwanini wateja wanatumia “mna” na “wingi” wanapoulizia bidhaa? Ni saikolojia au mazoea ya lugha?

Maana yake anajua mpo wewe na Boss wako, hata kama hamuoni😃
Kama wewe ndio boss mwenyewe basi vumilia tu
 
Mkuu, hapa lazima turudi katika ngeli za nomino. Jawabu lako liko kwenye ngeli ya PA-MU-KU.

PA- Huonesha mahali maalumu.
Mfano, hapa ni pazuri sana.
Pale panafaa kukaliwa.

KU- Huonesha mahali Kwa ujumla/eneo lisilo maalumu sana.
Mfano, huko shuleni Kuna chakula?
Kule barabarani ni kizuri.

Mu- Huonesha ndani ya kitu.
Mfano, humu ndani mna baridi sana.
Mule ndani muna wanafunzi.
Humu ndani (dukani) mnauza kalamu?

Hivyo, si kosa mteja kuja hapo dukani kwako na kutumia 'mna' ilimradi kile anachokiulizia Kiko ndani ya duka.
 
Wateja wameshachukulia kuwa wafanyabiashara wengi wana misukule isiyoonekana dukani,ndio maana wanatumia wingi hata kama muuzaji ni mmoja,muache ushirikina kwenye biashara manina
 
Kuna case kama hiyo uliozungumzia na kuna ile anapiga simu, hamjawahi kuonana wala hamfahamiani na bado atatumia wingi
Yes, ni lugha nzuri na sahihi. Hata wenye maduka mara nyingi huwa wanatumia wingi kujibu mteja..... Kwenye uongozi pia. Kiongozi mnyenyekevu siku zote hutumia wingi anapozungumzia mambo yanayohusisha serikali yake. Tutahakikisha....... na siyo nitahakikisha..... NB: kuna wakati maalum anaweza kutumia ''mimi''....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…