Kwanini watoto wa kike hasa Gen Z wazito kuanzisha salamu?

Mambo vipi wakuu?

Kuna sehemu bhana nilikuwa napata breakfast asubuhi hii mara pah wakaja wasichana wawili kwenye meza niliyokaa wakaa wakanilia buyu hawakutoa ata salamu na mi nikapiga kimya maana hauwezi salimia mtu aliyekukuta itakuwa maajabu, baada ya dk 10 wakaibuka wengine wawili nao wakapiga buyu hawa wote wanafahamiana wana matshirt ya benki yenye brand color ya kijani ni wale vijana wa direct sales.

Siwalaumu maana kutoa salamu kwa mtu uwa sio lazima ila kwangu uwa naona haijakaa sawa kuna vitu vingi mtu unaweza kosa kisa salamu tu na hizi tabia wanazo sana watoto wa kike wa Tanzania yaani wanaona jukumu la kuanzisha salamu ni wanaume ata wakikuta na hii usikute imesababishwa na wanaume wengi walivyowazoesha hii ni shida sana.
Mkuu misingi ya malezi imebadilika kabisa. Zamani mtoto alikuwa ni wa jamii na kila mmoja aliwajibika kulea. Sasa kila mtu anakufa lwake na mtoto wake. Ukikutana na mtoto akakusalimia, unashangaa!

Ijumaa nikiwa natoka kazini, nilipishana na katoto kanatoka shule kanasoma darasa la 5. Alinisalimia kwa "anwani"; "shikamoo mama" nikaitikia kwa furaha kwa kweli kisha akaitikia na kumaliza "pole". Sio siri nilifurahi na kushangaa, ikabidi nikahoji kidogo. Ndipo nikagundua wazazi wake hakika wamemlea vyema.
 
kutoa salamu umemkuta mtu sehemu inachosha ila mkipata shida mnaanza kutusumbua na kusalimia watu hamsalimii,fursa nyingi uletwa na mahusiano mazuri na salamu ni sehemu ya mahusiano mazuri tofauti na wewe unavyoitafsiri,
We unawaza tu kupata shida uko kwenye ubongo wako,
Okay sawa, mtu akipata shida kama hajakusalimia usimsaidie ondoka
 
Mambo vipi wakuu?

Kuna sehemu bhana nilikuwa napata breakfast asubuhi hii mara pah wakaja wasichana wawili kwenye meza niliyokaa wakaa wakanilia buyu hawakutoa ata salamu na mi nikapiga kimya maana hauwezi salimia mtu aliyekukuta itakuwa maajabu, baada ya dk 10 wakaibuka wengine wawili nao wakapiga buyu hawa wote wanafahamiana wana matshirt ya benki yenye brand color ya kijani ni wale vijana wa direct sales.

Siwalaumu maana kutoa salamu kwa mtu uwa sio lazima ila kwangu uwa naona haijakaa sawa kuna vitu vingi mtu unaweza kosa kisa salamu tu na hizi tabia wanazo sana watoto wa kike wa Tanzania yaani wanaona jukumu la kuanzisha salamu ni wanaume ata wakikuta na hii usikute imesababishwa na wanaume wengi walivyowazoesha hii ni shida sana.
Salamu za nini .... watu mlio kuwa mnatumishwa salamu hadi chooni mashuleni mna shida sana ....utasalimia watu wangapi kwa siku ...salamu ziwe kwa nyakati na mambo muhimu tu
 
kutoa salamu umemkuta mtu sehemu inachosha ila mkipata shida mnaanza kutusumbua na kusalimia watu hamsalimii,fursa nyingi uletwa na mahusiano mazuri na salamu ni sehemu ya mahusiano mazuri tofauti na wewe unavyoitafsiri,
Nani huyo ambaye akipata shida anaanza kukusumbua 2026 hii?
Wewe sema tu uko entitled na unapenda kusalimiwa, inakufanya ujisikie vizuri. Haya mengine ni visingizio tu
 
Mkuu misingi ya malezi imebadilika kabisa. Zamani mtoto alikuwa ni wa jamii na kila mmoja aliwajibika kulea. Sasa kila mtu anakufa lwake na mtoto wake. Ukikutana na mtoto akakusalimia, unashangaa!

Ijumaa nikiwa natoka kazini, nilipishana na katoto kanatoka shule kanasoma darasa la 5. Alinisalimia kwa "anwani"; "shikamoo mama" nikaitikia kwa furaha kwa kweli kisha akaitikia na kumaliza "pole". Sio siri nilifurahi na kushangaa, ikabidi nikahoji kidogo. Ndipo nikagundua wazazi wake hakika wamemlea vyema.
Natoa sana shikamoo.

Kwenye 10 zinajibiwa 4. Kwenye hizo 4 moja ndo inajibiwa kwa bashasha.

Nimeshakata tamaa.

Sasa ninasalimia pale tu ambapo ninahitaji kuzungumza na mtu.

Sema huu utamaduni ni wa kipumbavu sana sijui utaishaje.
 
watu wanachanganya mi nazungumzia ile mtu mmekutana kabisa face to face na mtu sehemu yoyote maofisini,migahawani nk kusalimiana ni ustaarabu na uungwana wa watanzania ,wanajifanya kuleta ubishi ila wameelewa nachomaanisha
 
Sasa kwanini watu wengine wasipoambiwa Shikamoo wananuna?
iyo sasa shida ,kwa mtu aliyekuzidi sana umri unatakiwa umpe tu shikamoo yake ndo utamaduni wa kitanzania ata wazungu wanatamaduni zao shida wabongo ujuaji tunadanganyana sana. wazungu wenyewe tamaduni zao kibao hawajaziacha
 
Natoa sana shikamoo.

Kwenye 10 zinajibiwa 4. Kwenye hizo 4 moja ndo inajibiwa kwa bashasha.
Wazee hawataki shikamoo, unawazeesha🤣🤣
Nimeshakata tamaa.

Sasa ninasalimia pale tu ambapo ninahitaji kuzungumza na mtu.

Sema huu utamaduni ni wa kipumbavu sana sijui utaishaje.
Kusalimiana sidhani kama ni utamaduni mbaya.
 
watu wanachanganya mi nazungumzia ile mtu mmekutana kabisa face to face na mtu sehemu yoyote maofisini,migahawani nk kusalimiana ni ustaarabu na uungwana wa watanzania ,wanajifanya kuleta ubishi ila wameelewa nachomaanisha
Salamu tofauti na "Shikamoo" hata wewe unaweza kuanzisha. Hizi hazina haja ya Gen Z kuanza. Changamka, si unataka salamu. Uwe unaanzisha. La sivyo kila mtu ataendelea na mambo yake maana sikuhizi watu wana mambo mengi kichwani
 
Back
Top Bottom