Kwanini watu hutazama mieleka licha kujua ni mchezo bandia?

Kuna tofauti ya uongo na mshindi kua pre determined. Mieleka sio kwamba watu hawapigani, wanapigana kweli sema matukio yote yanayofanyika hua yamejadiliwa kabla, nani atampiga nani wapi na mchezo utamaliziwaje. Ofcourse mwanamieleka anaweza kwenda offscript lakini sehemu kubwa ya mchezo unakua umepangwa kwa sababu ni mchezo unaotokana na storyline ama hadithi muendelezo.

Kusema mieleka ni fake sio kweli, watu hupigana kweli, kusema matokeo ya mieleka hua yamepangwa hapo ndip kweli.

Ndio maana inaitwa entertainment, ni mieleka ya burudani.
 
Si bora mieleka, watu wanaangalia movie ambayo wanajua kabisa 100% ni uongo hakuna kitu cha kweli mule na bado wanaangalia na kushangilia kabisa star akishinda [emoji3]
Hiyo ndio maana ya entertainment na art, lengo ni kujifurahisha. Na "ungo" au "ukweli" wa kitu ni mada complex sana na mara nyingi maana yake ni subjective au matokeo tu ya watu ku-label vitu kiuvivu/kiwepesi bila kufikiria kiupana. Mfano michoro ya picha unaweza sema ni "uongo!" Lakini kwanini iwe "uongo"? Kama tafsiri ya neno mchoro ni "kiwakilisha mawazo au chochote" na mawazo ni uhalisia! Ukilinganisha kwamba as long as kitu kina "identification" au "jina" basi tayari kinabeba uhalisia wake wa aina yake sababu tafsiti ya "uongo" ni kitu "kisichokuwepo." Kwa maana, hiyo picha na movie vyote ni "kweli" au "halisia."
 
Hapa umeongea kila kitu.

Mieleka Sio Bandia. /fake .
Ni halisi kabisa sema iko scripted .

Wachezaj Mieleka kuna Kipind wanavunjika kabisa Viungo. Wanatoka damu real kabisa sikuhizi.

Vile vibao vya Kifuan ni Real kabisa na vinauma balaa.

Kwahiyo ni mchezo Halisi ila uko very calculated na wanajaribu kuminimise Risk ili mtu asiumie sana...
by the way wale majamaa wamekomaa balaa.
 
Watu wanaangalia sci-fi movies na wanapenda ije kuwa mieleka? Binafsi niliacha kuangalia mieleka baada ya kugundua ni scripted
 
Makalio pia yamejaa bandia na shingo za vijana wa kiume zinageuka kama feni.
 
Nini chanzo cha ugomvi wa steve austin " stone cold" na Vince Macmahon?
 
Na tamthilia je?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…