Kwanini watu wa mikoani wanapenda kusalimia salimia?

Kwanini watu wa mikoani wanapenda kusalimia salimia?

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,311
Reaction score
36,056
Amani iwe nanyi wana JF

Niko shamba kwa mitikasi ya hapa na pale, yaani kila mtu anasalimia, kwa siku unasalimiwa zaidi ya mara 200

Mambo ya kijinga sana na ni code za kigoloko sana, unakuta una mawazo yako mtu ana ku-distract halafu cha ajabu hakujui na hiyo salamu haijengi chochote.

Kwa hesabu ya kawaida energy unayotumia kujibu watu 200 ukii-conserve unaweza ukafanya jambo kubwa la msingi.

Tusalimie watu tunaowajua na tuwe tunamaanisha, vinginevyo tunachoshana. Mmesikia nyinyi wapori pori?
 
Hao watu wametoka katika jamii zenye tamaduni zinazoamini kwamba watu wote unaokutana nao kuna uwezekano mkubwa wakawa na undugu na wewe.

Ndiyo maana katika salamu halisi za makabila kama Wasukuma, ukikutana na mzee ukamsalimia, salamu ina sehemu ya kuuliza "Ng'wa nani?". Yani hapo unaulizwa wewe unatokea ukoo/ nyumba gani? Inabidi umtaje babu/bibi yako, na huyo unayemtajia naye ataweka katika mahesabu yake ya majina kama hilo jina analijua.

Pote hapo anatafuta undugu tu, anaamini kuna nafasi kubwa mna undugu fulani hapo.
 
Ni sawa, lakini mambo lazima yaende yakibadilika, wakati ni fedha, gone are those days
 
Ni sawa, lakini mambo lazima yaende yakibadilika, wakati ni fedha, gone are those days
Umenikumbusha mbali sana.

Kuna kipindi nilienda likizo Mwanza, nikakuta kuna vitoto fulani barabarani nikavipita tu. Vitoto vidogo tu, hata siku vi register.

Basi wee, vile vitoto vilimind vibaya sana. Vikawa vinasema Kisukuma kwamba huyu mbona kapita tu kama hajatuona.

Nilishangaa sana, nikaja kugundua siko Dar. Halafu nilishanmgaa kwa sababu nilitegemea wao kwa sababu ni wadogo, kama wana mind kusalimiana sana wangeanza kunisalimia wao.

Nilikuja kugundua kuwa kum recognize mtu pale ni kitu cha muhimu sana.

Ila, unaweza kuvipita vitoto hivi, halafu ukakutana navyo ukaambiwa ni vitoto vya shangazi yako fulani, vinakujua ila wewe huvijui.

Sasa hapo muhimu kusalimiana tu.

Tatizo bora salamu zingekuwa fupi zile kama za Kiswahili "Za saa hizi?" unajibiwa "Salama" unapita.

Msukuma salamu anakusimamisha, ukimaliza kumtajia ukoo wako, anakuuliza na mkeo hajambo, na watoto? Na hapo hapo anaunga stories, kama una haraka unachelewa.
 
Salamu kwa jamii ambazo hazipo westernized na zinaishi kiasili ni kawaida. Hata Dar uswazi ukipita group la watu wamekaa bila kutoa salamu wanamaindi na ukitaka kulijua hilo, kosea njia halafu urudi kuwaomba maelekezo ndio utajua hujui 😁😁

Inshort hii kuishi kijamaa ni kama kuweka assurance kuwa hata stranger anaweza kukupa msaada ukipata tatizo lakini pia, salamu ni alama ya heshima hivyo usipompa mtu bhasi umemdharau au wewe ndio unajisikia
 
Iingie kwenye kstiba mpya, salamu ziwe za ishara, ikishindikana ziwe fupi fupi
Salimia watu wewe.Usilete shobo, utakosa wa kukuzika 🙂 🙂 🙂

Kuna mzee mmoja alikuwa anaona vijana wako maskani, akawaona "wavuta bangi" tu.

Ilamzee mtu wa watu akawa anawapa hi tu akipita.

Siku moja gari yake ikamuharibikia pale pale maskani.

Vijana wakampiga tafu, wakamtengenezea gari (wale wazee hata kufungua bonet hajawahi), wakamsukuma mpaka gari ikawaka.

Kutoka siku hiyo akajifunza sana akisema kuna watu unaweza kuwaona wavuta bangi tu hawana maana, halafu siku moja wakakusaidia sana tu.
 
Salamu kwa jamii ambazo hazipo westernized na zinaishi kiasili ni kawaida. Hata Dar uswazi ukipita group la watu wamekaa bila kutoa salamu wanamaindi na ukitaka kulijua hilo, kosea njia halafu urudi kuwaomba maelekezo ndio utajua hujui 😁😁

Inshort hii kuishi kijamaa ni kama kuweka assurance kuwa hata stranger anaweza kukupa msaada ukipata tatizo lakini pia, salamu ni alama ya heshima hivyo usipompa mtu bhasi umemdharau au wewe ndio unajisikia
Kwa watu mnaofahamiana salamu inaleta maana, kuna genuine concern ya kujua afya ya mtu na hali ya atokako. Mtu usiyemjua ataukimuuliza huu hali gani, akakujibu ni mgonjwa utamsaidia?
 
Salimia watu wewe.Usilete shobo, utakosa wa kukuzika 🙂 🙂 🙂

Kuna mzee mmoja alikuwa anaona vijana wako maskani, akawaona "wavuta bangi" tu...
Una point, ila usitumie salamu kama security au uwekezaji, tuwe genuine, tusalimie kwa kumaanisha, vinginevyo kila mtu na hamsini zake
 
Back
Top Bottom