Kwanini watu wa vijijini na masikini sana huwa na sura na maumbile mabaya tofauti na wa mjini au matajiri?

Hii mikoa ndio inazalisha sehemu kubwa ya nafaka Tanzania. Kinachokosekana ni ni Milo mchanganyiko yenye lishe kamili. Mtu anakula ugali mwaka mzima!
 
Tembelea vijijini Moshi,nenda tanga vijijini,nenda singida vijijini ,nenda kondoa Kwa warangi ,nenda kaone karatu Vijijini tembelea vijini vya ,babati manyara utakuja kugundua Uzi wako ni WA kipumbavu Tu Vijijini kuna watu wazuri kama mjini au kwako mawigi,lotion na mavazi ndio uzuri.
 
Lishe na kazi ngumu,kijijin mtu anashindia makande na mlenda,mjini ni mwendo wa pizaa kiepe ,huku wakila kiyoyozi.

Kimsingi watu wa kijini na wa mjini wanatofauti kubwa ki mwonekano.
Kama ni lishe mbona vijijini ni kitu cha kawaida kuwakuta wazee miaka 80>90 na kuendekelea wakiwa wazima afya Tele na wanafanya shughuli zao za kila siku.
Ingali wazee wa hapa mjini(penye lishe) wenye umri huo huo hawawezi kufanya task km mzee wa kijijini?
 
Hii ipo hata kwenye dini, kuna wazee wa dini fulani wana sura mbaya zilizokakamaa tofauti na wazee wa dini nyingine. Ila wanawake wa dini yenye wazee wenye sura mbaya ni wazuri hasa wanapokuwa kwenye mavazi yao utawapenda sana kwa wanavyoonekana usoni wamejikwatua kwa urembo wa kuvutia
 
bora mkoa wa pwani haupo hata mmoja ungekuwepo ungesikia ....ooh tatizo shule oooh wavivu kulima 😁😀
 
Ni kwa sababu ya Kazi ngumu na kukosa vitakasa mwili kama sabuni na mafuta. Kazi ngumu na jua kali vina zeesha mwili.

Watu wa vijijini jua lote la siku linaishia kwenye mwili, hawapati virutubisho vya ngozi, lishe duni, n.k.
Mwili unahitaji matunzo, kuogeshwa na sabuni, kupakwa mafuta, kukingwa na jua.

Lakini pia watu wa mjini hasa wanawake wana vitu bandia vingi kwenye miili yao. Nywele bandia, uso bandia ulio kandikwa angel face, kope bandia, wanja n.k.

Mwisho ni mavazi, mavazi pia yanafanya mtu apendeze, watu wa vijijini hawana mavazi mazuri, mavazi yame fubaa n.k.
 
kwa taarifa yako hao ndio wanaoishi miaka mingi.
 
Lishe na kazi ngumu,kijijin mtu anashindia makande na mlenda,mjini ni mwendo wa pizaa kiepe ,huku wakila kiyoyozi.

Kimsingi watu wa kijini na wa mjini wanatofauti kubwa ki mwonekano.
Vijijini hawajui kupanga diet, vyakula vyao ni wanga % 99, kukuta wanakula Mayai, maziwa, Samaki, Nyama na matunda ni ngumu, vijiji vingi wanakula asubuhi Uji, mchana ugali na mboga za majani usiku ugali tena, Asubuhi uji mchana ugali usiku ugali, kula nyama mpaka mnyama afe

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Matajiri hawana mawazo ya namna ya kupata kile wanachohitaji (Stress zinazeesha).Wanalala pazuri.
Mjini hakuna uchawi. Wewe fikiria mtu anakosa usingizi usiku kucha anapambana na wachawi (kelele za paka, bundi, panya nk,) atapendeza lini? Na ujue usingizi ni tiba
 
Huyo wa masaki mvizie asubui akiwa katoka kulala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…