Asilimia kubwa watakao kupinga humu ni wale waliokulia vijijini na uswazi..Profesa J mwenyewe amewahi imba kuhusu binti alie mtoa Sichimbi na kumpeleka mjini.
Mjini shule.
Watu wa vijiji hawana acces ya vyakula tofauti vinavyorutubisha mwili. Vipo vijiji vichache angalau.
Binafsi nimejiingiza kwenye kazi za watu wa vijijini, aisee nikikaa shamba mwezi hakuna mafuta yanakubali ngozi.
Nahisi kupigwa mionzi ya jua nayo inachangia sana, mfano trafic polisi hupigwa na jua sana na kuwa ngozi nyeusi sijui kama mmeliona hilo.
Vijijini watu huoga matope mda mwingi kuliko wa mjini, tope hufubaza ngozi.
Mizigo mizito, yaani watu wa vijijini hudumaa kwa kubeba mizigo mizito mara kwa mara kuanzia utotoni wakati mjini wanatumia usafiri.
Kazi ngimu, kutokana na kazi ngumu wanapoteza sehemu kubwa ya nishati wakati mjini mfano wanawake hio nishati hugrika mafuts na huifadhiwa kwenyr makalio.Makalio asilimia kubwa ni mafuta.
Kutembea mwenfo mrefu aisee hao watu wanatembea japo boda xipo ila wabahiri sana.
Kuuza vyakula vizuri na kubaki na makapi au masalia, mfano unyakyusani huchuja maziwa mazuri na kuyasafirisha mijini na wao kunywa makapi wanayaita 'Masulu"
Kulewa.Aisee kuna vijiji wanalewa mpaka wanasahau kula kuoga na kufanya kazi.