Brojust
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 349
- 1,024
Wadau habari ya Jioni,
kwani ugali una shida gani, mimi
nilijua ni hapa tu jamiiforum kumbe hata majumbani kwa watu.
Mimi ni mzanaki wa pale Kyabakari mbona kule kwetu tunakula ule ugali wa mtama na tupo fresh tu.
Tena ukila ugali wa mchanganyiko wa udaga na mtama alafu mboga yako ikawa kuku wa kienyeji jogoo ukalipika chuku chuku mbona tunakuwa tupo strong tu, kimwili na kiakili.
Watanzania tuachane na mambo ya kuzungu, Kama unapenda ugali basi dondosha comment yako kwa aina ya ugali unaopikwa kwenye kabila lako.
Nawasilisha;