kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Bodi ya ligi lazima ijiuzulu kwasababu zifuatazo.
1. Ndani yao alikosekana mtu wa kunusa hatari za kijamii, kimpira, kiuchumi, na za kiusalama zitakazoambatana na kuahirisha mchezo ule. Kiongozi hana busara, akili ya kusimamia mpira na amani ya nchi. Kwake yeye ilikuwa liwalo na liwe haichezwi.
2. Waliarishisha mechi kwasababu ambazo ni nyepesi ambazo hazina tabia ya kuahirisha mpira kote duniani.
3. Waliahirisha mechi bila kutumia kanuni za ligi husika.
4. Waliahirisha ligi bila kushirikiana na mamlaka za kijinai kama polisi, takukuru na serikali ili kupata maoni yao.
5. Kuna malalamiko mengi dhidi yao kuhusu uendeshaji mbaya wa ligi. Kuna timu zinanyang'anywa wachezaji wao wenye mikataba halali kwa baraka za TFF.
6. Kutokana na uendeshaji mbaya ziko timu kwenye ligi ambazo zinaweza kushuka daraja kutokana uamuzi mbaya viwanjani na ratiba mbaya ya mechi zao. Timu nyingine zinacheza kwenye jua Kali na nyinge kwenye baridi Kali, nyingine zinapangiwa ratiba ngumu nyingine ratiba nyepesi, nyingine zinapewa penati nyingi zingine zinanyimwa penati zao makusudi na nyingine zinanyimwa hata magoli yao halali.
7. Timu nyingi hazina Imani na Bodi ya ligi/TFF. Kama waziri akizishirikisha timu zote za ligi na kuzihoji ni uhakika 98% ya timu zitasema hazina Imani na usimamizi na uendeshaji wa ligi yao.
Kucheza mpira chini ya uongozi ambao huna imani nao ni balaa. Wajiuzulu.