Bodi ya ligi lazima ijiuzulu kwasababu zifuatazo.
1. Ndani yao alikosekana mtu wa kunusa hatari za kijamii, kimpira, kiuchumi, na za kiusalama zitakazoambatana na kuahirisha mchezo ule. Kiongozi hana busara, akili ya kusimamia mpira na amani ya nchi. Kwake yeye ilikuwa liwalo na liwe haichezwi.
2. Waliarishisha mechi kwasababu ambazo ni nyepesi ambazo hazina tabia ya kuahirisha mpira kote duniani.
3. Waliahirisha mechi bila kutumia kanuni za ligi husika.
4. Waliahirisha ligi bila kushirikiana na mamlaka za kijinai kama polisi, takukuru na serikali ili kupata maoni yao.
5. Kuna malalamiko mengi dhidi yao kuhusu uendeshaji mbaya wa ligi. Kuna timu zinanyang'anywa wachezaji wao wenye mikataba halali kwa baraka za TFF.
6. Kutokana na uendeshaji mbaya ziko timu kwenye ligi ambazo zinaweza kushuka daraja kutokana uamuzi mbaya viwanjani na ratiba mbaya ya mechi zao. Timu nyingine zinacheza kwenye jua Kali na nyinge kwenye baridi Kali, nyingine zinapangiwa ratiba ngumu nyingine ratiba nyepesi, nyingine zinapewa penati nyingi zingine zinanyimwa penati zao makusudi na nyingine zinanyimwa hata magoli yao halali.
7. Timu nyingi hazina Imani na Bodi ya ligi/TFF. Kama waziri akizishirikisha timu zote za ligi na kuzihoji ni uhakika 98% ya timu zitasema hazina Imani na usimamizi na uendeshaji wa ligi yao.
Kucheza mpira chini ya uongozi ambao huna imani nao ni balaa. Wajiuzulu.
1.Hoja Yako ya kwanza bodi ya ligi ilihairisha mchezo kwa kufata maelezo ya Afisa Usalama wa mchezo ambaye kitaaluma ni askari polisi mwenye cheo Cha ISP bwana Hashim Abdallah ambaye aliona Yale yalio fanyika siku Moja kuelekea mchezo huo.
Kwenye barua ya bodi ya ligi Paragraph ya mwisho kabisa barua imesema ilipokea ripoti ya afisa usalama ambaye alionyesha Kuna mambo yanayo hitaji uchunguzi zaidi,hivyo bodi ligi walihairisha mchezo huo.
2.Umesema wamehairisha kwa hoja nyepesi ambazo hazipo duniani kote.
Duniani kote Kuna Sheria 17 ambazo Zina tungwa na IFAB ambazo FIFA Wana zitumia nankuzipeleka kwa mashrikisho yote duniani ikiwemo TFF.
Naomba utambue ukiondoa sheria 17 ambazo Zina fuatwa na mashirikisho yote mwanachama wa Fifa, tambua Kila shirikisho Lina KANUNI zake za kuendesha ligi Yao.
Kwaiyo kanuni za Tanzania za ligi zina weza zisifanane na ligi nyingine.
Mfano: Kanuni ya Hat trick ya Ujerumanj haifanani na mashrikisho mengi duniani.
Ujerumani hat trick ina hesabiwa baada ya magoli yote matatu kufungwa ndani ya kipindi kimoja cha mchezo.
Ukifunga goli Moja kipindi Cha kwanza alafu ukafunga magoli mawili kipindi Cha pili Ujerumani sio Hat Trick lakini kwenye nchi zingine Ina hesabika.
BODI YA LIGI imeharisha mchezo kwa kufata ripoti ya afisa usalama hivyo hoja ya msingi ni usalama.
3.Una sema hawakufata kanuni je umesoma barua ya bodi ya ligi ?
Paragraph ya mwisho bodi imesema imetumia kanuni ya 34....nenda kasoma ujielimishe kwanza.
4.Una sema walihairisha mchezobbila kishauriana na mamlaka nyingine ikiwemo polisi.
Nadhani una onyesha jinsi usivyo fahamu taratibu za mchezo wa Mpira wa miguu.
Iko hivi kabla ya mechi yoyote duniani iwe ya Fifa, CAF, UEFA au hizi za TFF na bodi ya ligi, mamlaka ya uendeshaji Ina teua waamuzi, GC ambaye ni kratibu wa mchezo, Kamishna wa mchezo huyu ndio mmiliki wa mchezo huo na ndio mwenye sauti ya mwisho juu ya mchezo husika, Afisa Usalama huyu ana Toka ndani ya jeshi la polisi ili kuja kushauri mambo yote ya usalama na kusimamia usalama akiwa mwajiliwa wa muda wa shirikisho husika.
Kwa Nini Shirikisho Lina takiwa kuteua afisa Usalama kutoka jeshi la polisi ? Jibu ni kwamba Polisi na mamlaka zingine hasitakiwi kuingilia Mpira wa mguu kimaamuzi !!! Hivyo Afisa Usalama anae teuliwa ana hesabika ni mwajiriwa wa muda wa TFF au Caf au UEFA hivyo Afisa huyu ndio ana toa ripoti ya kiusalama !!!
Bodi ya ligi ili pokea ripoti ya Afisa Usalama ambaye ndio mwenye dhamana ya usalama na kubainisha mambo kadhaa ya kiusalama.
Kimsingi bodi ya ligi ili imeshirikiana vyema kabisa na jeshi la polisi kupitia Afisa usalama.
5-6-7 hoja zako ugeweka na mifano kuliko hisia zako binafsi ili uwe mjadala wa wazi.