Kwanini watu wanataka Bodi ya ligi wajiuzulu ili dabi iruduwe?

Kwanini watu wanataka Bodi ya ligi wajiuzulu ili dabi iruduwe?

Hoja ya sababu za kiusalama haina mashiko kwakuwa ilitolewa siku moja kabla ya mchezo kitu ambacho inakinzana na kanuni ambayo ilipaswa waainishe siku ya mchezo kulikuwa na tishio gani la kiusalama ambalo vyombo vya usalama waliona hakuna namna nyingne tofauti na kughairisha mchezo.
NB: KAMA UNAONGEA KWA DHATI YA MOYO WAKO BILA UPENDELEO WOWOTE LAZIMA JIBU LITAKUWA MCHEZO ULIGHAIRISHWA KWAKUWA SIMBA WALIGOMEA
Andika hapa kanuni hiyo ambayo imekinzana na kanuni ya 34 ambayo bodi ya ligi wameitumia kuahirisha mchezo huo.Yani una andika maneno matupu bila kanuni daaah alafu una sema kanuni imevunjwa.PLZ USIJADILI KAMA HAUJUI KANUNI AU HAUJA WAHI KUSOMA HIZO ZA LIGI.
 
Hakuna kanuni itatungwa na shirikisho la nchi yoyote ambayo itapingana na zile za FIFA. FIFA inataka mpira uchezwe na maswala yanayoweza kuahirisha mechi yameorodheshwa, kuzuiwa kucheza mazoezi kwenye uwanja sio miongoni mwake. Nchi nzima na vitengo vyake vyote vilijiandaa kikamilifu kudumisha usalama wakati na baada ya mechi. Ni Nani kasema usalama hautakuwepo siku ya mechi, kwasababu gani? Ni aina ipi ya uvunjivu wa amani ulitarajiwa; kuvuja viti? maandamano? Kupigana? au aina ipi ya usalama ingekosekana?!Je, huyo afisa wa usalama imeitoa wapi taarifa ya uvunjivu wa usalama siku ya mechi;; IGP, FFU, usalama wa taifa, Muliro, au CDF?
Hii nchi Ina watu wajuaji sana, daaah Yani umeandika pumba ambazo hata hata wewe siku ukipata uelewa utajicheka sana.
 
Kuhairisha mchezo ilipaswa kuwa tukio la mwisho Kabisa tena baada ya kujiridhisha kwa kushirikisha vyombo vya usalama tena kwa mchezo mkubwa kama ule ilipaswa kiongozi mkubwa wa usalama auelezee umma nini kilitokea na hatua gani walichukua tofauti na hvyo ni vile tuu bodi ya ligi walilazimika kuhairisha mchezo kwakuwa tuu simba waligoma mana ata barua yao ya kuhairisha mechi walisema wamekaa kikao baada ya kupokea barua ya simba hilo linatosha kabisa kujua kuwa maamuzi yao yalisabishwa na simba kugomea mchezo
Kanuni za mpira zinaruhusu timu kupokwa points 3 hata baada ya mechi kuchezwa. Busara ya Bodi ya ligi/TFF wangeacha mechi ichezwe wakati wakiendelea na uchunguzi wao wa rushwa na usalama. Ni usalama gani huo ambao jeshi la polisi na vyombo vingine vya ulinzi lingeshindwa kuudhibiti? kama issue usalama ingekuwa so serious bodi ya ligi wangeweza pia kuruhusu mechi ichezwe bila mashabiki ili kupunguza vitendo vya usalama. Bodi ya ligi na TFF ni wahuni wa kupindukia; CAS ndio suluhisho kwenye hili. Siku za mwizi ni 40, arobaini ya janjajanja za Karia imetimia; amekanyaga mpira unaopeleka oxygen kwake mwenye na TFF.
 
Back
Top Bottom