Kwanini watumishi wa Mungu hawamuelewi Goodluck Gozbert?

Binadamu anaweza kukuhukumu kwa monekano. Bila kujali Imani yako ikoje. Monekano sio Imani
Imani pasipo matendo basi imekufa. Kama mtu anaamini pombe ni haramu basi asiinywe, au anaamini nguruwe ni haramu basi asiile nyama yake.

Kile unachokiamini kinapaswa kijionyeshe kwenye maisha yako ya kila siku. Hivyo muonekano wako ni kielelezo cha kile unachokiamini moyoni mwako.
 

Siku zingine unaandika hekima kweli..safi sana
 
Waafrika tumezivamia dini (za nje) na tutakufa hatuzijui.

Lengo la nyimbo za dini ni kusifu na kuabudu sasa fikirini yeye anafanya wapi kisha mtajua analenga nin hasa.

Utakuta mtu anamponda eti ajataja jina la Yesu alafu mtu huyo huyo utankuta anazisifu Zaburi. Mtu akisema Zaburi ziliandikwa wakati Yesu ajaja duniani basi na sharyi aziache maan ni outdated.

Eti Sharo?, kwan mlitaka awe mchafu mchafu wakati dini znasema mwili wako ni hekalu la Bwana!.

Narudia tutakufa hatuijui hizi dini.
 
Hajawahi hata nyimbo moja kutaja jina la YESU
Sikuwahi kumsikiliza, nadhani hajaingia kwenye circles zangu za muziki. Ila sasa nitatafuta nyimbo zake mbili tatu nisikilize ili nipate kufahamu ni kwa nini mtu ambaye nyimbo zake zote hazihusishi jina wala matendo ya Yesu bado anasadikiwa kuimba "muziki wa injili". Anaimba INJILI ya nani sasa?
 
Kwa hiyo mtu aliyeamua asitaje kabisa jina la Yesu huyo anaimba muziki wa injili? La hasha! Yawezekana anaimba muziki wenye ujumbe mzuri sana, apewe credit zake kwa hilo. Kwani muziki mzuri lazima uwe wa injili? Kwa nini iwe lazima kumuunganisha na injili ambayo kimsingi haiongelei kabisa? Injili ni ya Yesu Kristo. Kama katika nimbo zake ZOTE hajalitaja jina la Yesu lazima tujiulize kwa nini.
 
Mi namkubali Angel Benard ndo msanii wa injili wa kisasa ,jina la Yesu analitaja bila woga na dini zote wanasikiliza na kutazama nyimbo zake. Huyo mwingine ni Kaoge alijificha katika ukristo.

Gospel waachie watu wa Mbeya, wanaimba kwa hisia na madaha mpaka rahaaaa
 
Haya

Ujana haubagui.[emoji53][emoji53]
 
Mkuu huyu jamaa mimi huwa simwelewi pamoja na wenzake wa dini kama kina rose muhando.Raha ya nyimbo za dini usikilize kina Buluzuga, Bulyunkulu hawa waliimba na kuchukua baadhi ya vifungu kwenye biblia na kuelezea ila hawa wengine huwa siwaelewe
 
Mkuu huyu jamaa mimi huwa simwelewi pamoja na wenzake wa dini kama kina rose muhando.Raha ya nyimbo za dini usikilize kina Buluzuga, Bulyunkulu hawa waliimba na kuchukua baadhi ya vifungu kwenye biblia na kuelezea ila hawa wengine huwa siwaelewe
Hiyo zamani sasa MKUU
 
Wapo wengi tu paul clement,jessica bm,mercy masika,joel lwaga
 
Huyu jamaa mi mwenyewe sometime huwa ananimix

Kupima mkojo na uchochezi wapi na wapi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…