sijui kama watumishi wa Mungu wanamuhukumu au la, ila mimi nikiwa kama mkristo kwa kweli huyu kaka hata simuelewi na nyimbo zake huwa sijui nizeweke kwenye kundi gani, kiasi kwamba nilishaamua kuachana nazo, mimi huwa sipendi kusikiliza album nzima ya mtu kwahiyo mara nyingi huwa nachagua nyimbo za watu tofauti tofauti nnazozipenda natengeneza mix naweka sehemu moja ndo nasikiliza, kama ni gospel basi nategeneze mix ya waimba injili tofauti tofauti ndo nasikiliza, ila nyimbo za huyu kijana nimeshindwa kabisa niziweke wapi, mana kwenye gospel hazikai na kwenye bongo fleva hazikai. Kuna neno linasema Wanyama wanaofanana huenda pamoja na Ndege wanaofanana huruka pamoja, Ila wenzako wamekukataa kwasababu ya tofauti yako, ndo yanayomtokea gosbert, achague kama anataka kuwa moto au baridi, mkristo bila kumtajia jina la Yesu hajakuelewa bado, mana Kutaja jina la Mungu hata bongo fleva au taarabu wana litaja sana tu kwenye nyimbo zao.