Kwanini watumishi wa Mungu hawamuelewi Goodluck Gozbert?

Kwanini watumishi wa Mungu hawamuelewi Goodluck Gozbert?

Mkuu huyu ni muimbaji wa nyimbo za dini na dini siyo injili pekee ni zaidi ya hapo ndio mana nkatolea mfano wa zaburi ambayo pia siyo injili.
Nakubaliana na wewe kuwa dini si injili peke yake, maana kuna dini ambazo msingi wake haujajengwa kwenye injili. Lakini dini isiyoitambua injili hiyo si dini ya kikristo, maana huwezi kumtenganisha Yesu Kristo na Injili yake.

Kwa misingi hiyo sijakataa kuwa yeye anaimba nyimbo za dini...sawa. Lakini dini hiyo si ya Kikristo. Tukubaliane hapo.
 
Kwa sababu wengi wana wivu. Wakiimba injili wanakata mauno ila mtu akikata kiuno hicho hicho kwenye bongo flava wanaleta unafiki.
 
Ni kweli kwamba hajawahi litaja jina la Yesu..!?

Hii kwangu mpya...
 
images
 
sijui kama watumishi wa Mungu wanamuhukumu au la, ila mimi nikiwa kama mkristo kwa kweli huyu kaka hata simuelewi na nyimbo zake huwa sijui nizeweke kwenye kundi gani, kiasi kwamba nilishaamua kuachana nazo, mimi huwa sipendi kusikiliza album nzima ya mtu kwahiyo mara nyingi huwa nachagua nyimbo za watu tofauti tofauti nnazozipenda natengeneza mix naweka sehemu moja ndo nasikiliza, kama ni gospel basi nategeneze mix ya waimba injili tofauti tofauti ndo nasikiliza, ila nyimbo za huyu kijana nimeshindwa kabisa niziweke wapi, mana kwenye gospel hazikai na kwenye bongo fleva hazikai. Kuna neno linasema Wanyama wanaofanana huenda pamoja na Ndege wanaofanana huruka pamoja, Ila wenzako wamekukataa kwasababu ya tofauti yako, ndo yanayomtokea gosbert, achague kama anataka kuwa moto au baridi, mkristo bila kumtajia jina la Yesu hajakuelewa bado, mana Kutaja jina la Mungu hata bongo fleva au taarabu wana litaja sana tu kwenye nyimbo zao.
Kwani nyimbo za gospel zikoje?.je hebu niambie kipindi cha nyuma kabla ya yesu kristo kuja duniani waliokuepo walikua hawaimbi nyimbo za kumtukuza Mungu?
 
Uyo dogo kajitaidi sana kufanya mapinduzi kwenye nyimbo zakumtukuza Mungu.Nyimbo nyingi tunazoita za injili huo mtindo ni watu walioubuni kwaiyo kama kuna mtu kajitokeza kufanya maboresho kwa namna alivyoona mimi sidhani kama ni kosa.Mambo mengine tumekariri tu bila kujua dunia imetoka mbali na kumekua na mabadiliko kila zama zinapofika.Nyimbo yoyote yenye mahudhui yakutukuza Mungu ni nyimbo ya dini ndo maana kabla ata ya yesu kristo kuja watu walikua wanaimba tena kwa namna mbalimbali kuliko hizi tunazoimba leo.Kwaiyo hao watumishi wamwache uyo dogo afanye kile anachoona chafaa kwa Mungu wake na maisha yake maana uimbaji ni ajira pia.mengine tumwachie Mungu mwenyewe.
 
Nakubaliana na wewe kuwa dini si injili peke yake, maana kuna dini ambazo msingi wake haujajengwa kwenye injili. Lakini dini isiyoitambua injili hiyo si dini ya kikristo, maana huwezi kumtenganisha Yesu Kristo na Injili yake.

Kwa misingi hiyo sijakataa kuwa yeye anaimba nyimbo za dini...sawa. Lakini dini hiyo si ya Kikristo. Tukubaliane hapo.

Haya mkuu na zile amri 10 za Mungu tuziache mana siyo ukristo ule. Ukristo amri ni moja tu upendo
 
huyu ni miongoni mwa wajanja wajanja wanaotumia gospel music kma kichaka cha kufanikisha mambo yao nyimbo zake zina maudhui ya kijanja tu, injiri sio kwa ajili ya kupata pesa ila pesa itakuja kma baraka lkn huyu na Flora mbasha ni wajasiriliamali .
 
Back
Top Bottom