Kwanini watumishi wa Mungu hawamuelewi Goodluck Gozbert?

Kwanini watumishi wa Mungu hawamuelewi Goodluck Gozbert?

Simkubali kwa lolote namengi yakusema ila kigugu mizi kimenikata ndaludi
 
aliye kudanganya mavazi sio sifa moja wapo ya utakatatifu ni nan
Mavazi ni utamaduni wa jamii husika sio sula la imani.
Anachokivaa mkristo wa New york kanisani akikivaa mkristo wa Mneya inaweza kuonekana si sahihi.
Si kwasababu ya dini ila kwasababu ya utamaduni wa mahala husika
 
very unfortunately, Mungu anaangalia hata mavazi unayovaa,ndio maana kuna aina ya mavazi anaruhusu, menigne haruhusu, wala msifuatishe namna ya dunia hii.....usiishi kwa kubadilika kadiri dunia inavyotaka bali kadiri Neno la Mungu linavyotaka. usijevaa vibaya, mfano mwanamke kavaa mavazi ya kikahaba akasema Mungu anaangalia moyo sio mavazi, usije kaa pamoja na watu wenye mizaha wanaomdhihaki Mungu, chagua marafiki wa kuwa nao kondoo wa Bwana wanaijua sauti yake na humfuata, hakuna ukristo tofauti na ukristo wa watu wengine, kama kweli unaongozwa na Roho yule yule wa Kristo ambaye na wenzio wanaye lazima mtakuwa na tabia zinazoendana. binafsi huwa simwelewi kuanzia mapozi, nyimbo zake, kutunga nyimbo ya kidunia isiyokuwa ya kimungu, unajua bongoflava ni nyimbo za kishetani/hazihamasishi watu kumtumikia Mungu, zinahamasisha tu uzinzi, ugomvi na takataka za dunia hii, ukiona mtumishi anawatungia watu wa dunia nyimbo jua hana Mungu, anahitaji msaada.
Usipoenda na mitindo ya dunia utashangaza sana.
Kwamba leo hii uvae mavazi yale ya magamba ya miti kwasababu huendi na mitindo ya dunia.
Hayo maandiko unayatafsiri kama gazeti ndugu.
Mavazi yaliyovaliwa miaka 100 iliyopita hayavaliwi leo na ukivaa leo utasahangaza kwasababu dunia imeshayaacha.
Nakumbuka wanawake walipoanza kuvaa suruali miaka ya nyuma ilishangaza sana lakini sasa imezoeleka kwasababu kizazi kilochokua kinashangaa ama kimeondoka ama kimekubaliana.
Suruali unazoshona leo kwa fundi hazikushonwa miaka 70 iliyopita kulikua na mitindo. Pengine watu wa miaka ya 70 hapo mnapendelea mitindo bado ya miaka yenu na mnahisi ndo mitindo ya kiMungu naona ni kushindwa tu kujua mambo kwa ufikiri sahihi.
Ukiona unashangaa sana mambo leo ujue unaishi kwenye dunia ambayo hutakiwi kuwepo au unaiishi jana huku ukisingizia maandiko kwamba yametoa maelekezo tusifanye hivyo.
Unaweza ukawa hata hutumii simu wewe wala TV kwakua wakati wa Kristo havikuwepo.
Wakristo tujitahidi kuwa tunazungumza hoja lasivyo tutakua tunamuaibisha Kristo kwa uprimitive wetu tukiujengea hoja ya kristo
 
...hauwezi kushindana!!ooh kushindana na mwanadamu mwenye kinywa yayaah x2
...vita vya maneno kuna watu ni majemedari, ukisema mshindane mbona mikono utainua,
..kupigwa vita ni kawaida isikusumbuee...
...wewe ni mti wenye matunda zoea mawe,
Lia kidogo nyamaza ili uchungue uishe.....DAAAH DOGO KAWAIMBIA HUU WIMBO.
 
jamaa target yake ni watu wote wenye imani tofauti ndomana hamtaji Yesu pia msanii mwengine ambaye hamtaji yesu kwenye nyimbo zake na anakiki ni Angel Benard. kiukweli wamefanikiwa kwa hili maana comments za nyimbo zao zina watu wa imani tofauti tofauti
Ila maandiko yanasema ukinikana duniani namimi nitakukana mbele ya Baba yangu, ili kumfikia Mungu wakweli lazma tupitie kwa Yesu na hata shetani akisikia mungu hashtuki mapepo pia majini pia lakini ukilitaja jina la Yesu kuna kitu kinatokea ktk Ulimwengu wa roho, so tusipambe dhambi tusitiane moyo kwenye hamna waimbe kweli ili watu wawe huru na dhambi wakombolewe kisawa sawa
 
Bible inasema watu wa Mungu watatambulika kwa matendo yao.
Kama matendo yake hayamtambulishi bas ni tatzo japo kumuhukumu sio kazi yetu ni ya Mungu.

Philips X2560


IMG_20180505_200130_748.jpg
 
jamaa target yake ni watu wote wenye imani tofauti ndomana hamtaji Yesu pia msanii mwengine ambaye hamtaji yesu kwenye nyimbo zake na anakiki ni Angel Benard. kiukweli wamefanikiwa kwa hili maana comments za nyimbo zao zina watu wa imani tofauti tofauti

Angel Benard huwa anamtaja sana Yesu. Sikiliza vzr nyimbo zake
 
Back
Top Bottom