Kwanini watumishi wa Umma waliokatazwa na sheria kujihusisha na siasa wanavaa nguo za vyama vya siasa?

Kwanini watumishi wa Umma waliokatazwa na sheria kujihusisha na siasa wanavaa nguo za vyama vya siasa?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Wapo watumishi wa mahakama, tume, vyombo vya dola na taasisi nyingine wamekatazwa na sheria kwa kipindi chote Cha utumishi wasijihusishe na siasa lakini aidha kwa kujua au kutokujua leo wanavaa nguo za vyama, wanaposti picha kwenye mitandao wakiwa na nguo za chama Cha siasa na kuandika katika magroup wakiunga mkono siasa.

Je,kwa kuwa mamlaka zao za nidhamu zimeshindwa kuwawajibisha , hakuna namna uchunguzi binafsi unaweza ukafanyika na kuwasilisha ushahidi mahakamani? Haya Ni Mambo yanayokwaza nafsi za watu ambayo mtu akikwazikwa anaweza akapandwa hasira akavunja amani ya eneo flani la nchi.

Hawa tunaowaona kwenye status zao wameweka maneno au picha wakiwa na nguo za chama tuwafanyeje? Kwanini wadharau sheria za nchi na wasiadhibiwe? Kila mwenye chama akivaa nguo za chama chake shughuli za serikali zitaenda?
 
Back
Top Bottom