Kwanini watumishi wengi wa 'idara nyeti' ni matapeli na hupenda kujifunua utambulisho wao kwa wauza bia bar

Kwanini watumishi wengi wa 'idara nyeti' ni matapeli na hupenda kujifunua utambulisho wao kwa wauza bia bar

nyboma

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2021
Posts
2,308
Reaction score
7,366
Nimekaa nikajiuliza sana kwanini watumishi wengi wa idara nyeti (wengi mtakuwa mmenisoma na maanisha nini), watu hawa ukiangalia kazi wanayofanya na maisha yao mtaani ni vitu viwili tofouti kabisa maana vijana hawa wamejawa na tamaa hadi kufikia kutapeli watu hovyo mtaani kwa kigezo cha kufanya kazi katika taasisi nyeti hiyo na bila aibu wamekuwa wakionesha vitambulisho vyao hovyo kwenye kumbi za starehe pindi wakilewa.

Swali langu kwa viongozi wa taasisi hii nyeti, Kama mtumishi wa idara hii anaweza kuwatapeli watanzania wenzake, je akikutana na watu wa nchi nyingine ambapo ilitokea akalambishwa dollar je mna uhakika gani mtu huyuhuyu ambaye anaweza kujianika mbele ya wahudumu wa baa kuwa hawezi kuuza siri za nchi kwa thamani ya vipande vya fedha?

Au taasisi hii nyeti inaruhusu watumishi wake kufanya dhuluma kwa watanzania kwa kigezo cha kufanya kazi huko?

Ombi, langu kwa taaisisi hii nyeti wajitahidi kuwaboreshea maisha watumishi wao kuepuka aibu ndogo ndogo kama hizi maana vijana hawa hawa hawakawii kuuza siri za taifa hili kwa maadui kwa kigezo cha maslahi.

Huwa nakutana na vijana kutoka Ubalozi wa kenya, vijana ukikaa nao hata nature ya mazungumzo yao unaona kabisa idara yao ya NIS ilifanya kazi ya ziada ya kuwachuja na kuwa recruited, tofouti na hawa vijana wetu ambao tunawategemea kama taifa wao ni starehe na ulimbukeni usio na faida yoyote kwa taifa.
 
shibela

Unaweza funguka alikutapeli nini na namna ulivyo shughulika nae.
 
Jana Ulirudi Usiku

Huyu alinikuta niko na mke wangu tumekaa mahali akaleta zile za kukonyeza nikamtuma mtu ampe onyo, nilivyoenda enda washroom nikakuta amekuja kwenye meza yangu kumtongoza mke wangu nilimzaba kofi moja zito sana akarise pale ilikuwa nimmalize siku ile sema tu watu waliingilia pale nikaamua kuondoka kwa amani.
 
Tangu lini Pesa Ikatosha mzee, Pride haitalipa Bills zao wacha waingie front kusaka pesa
Kwanini wasitumie pesa wanayopatau kufuga mbuzi wapate japo pesa ila sio kwa mbinu ya utapeli wanayotumia wao na mbaya zaidi wanaenda mbali hadi kutoa vitambulisho vyao je miiko ya kazi inawaruhusu kufanya huu ujinga wanayofanya?
 
Huyu alinikuta niko na mke wangu tumekaa mahali akaleta zile za kukonyeza nikamtuma mtu ampe onyo, nilivyoenda enda washroom nikakuta amekuja kwenye meza yangu kumtongoza mke wangu nilimzaba kofi moja zito sana akarise pale ilikuwa nimmalize siku ile sema tu watu waliingilia pale nikaamua kuondoka kwa amani.
Haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Mkuu maisha ni Ujanja Ujanja hata hawa Viongozi wakubwa wanakutapeli ndio mana unawapa Kura kwenye ballot box
Tofoutisha majukumu ya usalama wa taifa na mtumishi wa wakaida na majukumu yao.
 
Wengi mnao tafuta connection za kuingia uko ndo mna taperiwa
Usifikiri watu wote wanashida na kazi, wao ndio mishahara haiwatoshi wanatoka kuja kukopa mitaani next time tutawashukulia sheria kwa kuwalaza ndani wakose kuripoti huko kazini kwao
 
Back
Top Bottom