FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Watatokea vipi Rwanda na unasema mipaka ilikuwa haijachorwa?Ni kabila la kikushi lenye asili kutokea Ethiopia, waliingia ardhi ya Rwanda kama wafugaji na baadae wakalitwaa hilo eneo dhidi ya wahutu na watwa. Wabelgiji walipofika waliikuta hali hiyo hiyo na kutokana na physique yao ya urefu, uso mwembamba na pua ndefu, wakawaona wao wapo karibu zaidi na uzungu kuliko wabantu
Hivyo, waliwaweka kuwa superior ethnic group kwa hapo Rwanda na Burundi ndio maana mtusi ni mtu anaejihisi superior sana na huwa hachanganyi damu kirahisi na wabantu kwa kuwaona inferior.
Kuhusu kuingia Tanzania, wameanza hata kabla ya mipaka kuchorwa na mkoloni, ndio maana ukifuatilia mila, mavazi na hata baadhi ya falme za zamani haswa muleba, Ngara na Karagwe utakuta wapo waliotokea Rwanda. Kwa hiyo interaction ya Watusi, wahutu na wahaya si kitu cha leo wala jana
Hiyo route uliyoitaja si ndiyo route waliyokuja nayo wachaga wakaishia Kilimanjaro? kwa hiyo na wachaga ni watusi?