Kwanini wazazi wengi wa kiislamu hasa wa kike hawataki watoto zao kuolewa mke pili

Kwanini wazazi wengi wa kiislamu hasa wa kike hawataki watoto zao kuolewa mke pili

Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2022
Posts
1,215
Reaction score
3,035
Wakati wa mwezi mtukufu wa ramadhan unakaribia vijana wanavuta jiko na wengine wanaongeza mke wa pili,tatu mpaka wa nne kama dini inavyoruhusu.

Kuna tukio limetokea juzi mama wa binti ni muislam Safi tu na mumewe ni shekh mkubwa Ila mama wa binti amekataa mtoto wake kuolewa mke wa pili,

Je hii ni haki muislam unakataa mtoto wako kuolewa mke wa pili kama dini inavyoruhusu.

Naomba kuwasilisha
 
Kuhusu mamamke kukataa haipaswi kukataa sio mke wa pili bali hata kukataa mke wa kwanza.

Ila mtoto anayeolewa anayo haki ya kukataa kwasababu ndoa ya wake wawili inaruhusiwa kidini ila sio lazima just Kama kuolewa mke wa kwanza inaruhusiwa ila sio lazima kwamba bwana akija tu ukubali.
 
Vita, husda, chuki, migongano kwenye familia hasa ya mwanaume...

Japo ni kheir kuolewa mke wa pili kuliko kuwa mchepuko wa mtu
 
Hivi unadhan kuolewa mke wa pili ni raha ni vitaaa muraaa ,mke mwenzio vita ,ukwen vita
Hapo sasa,
Mzazi gan atakubali binti yake mdogo akaingie kwenye majukumu mazito ya uke wenza hapo bado arogwe ashindwe kuzaa
 
Kuwa mzazi ni changamoto tosha
Huwezi kujua labda karidhiki na huyo mme baada ya kuuulizia tabia na hulka zake

Sasa kama ni mtu wa kuoa mwezi mmoja na ukiisha anarudi bar unataka mzazi akubali tu

Wapo wanaoona mwezi wa Ramadhani tu wanaanza kuuabudu kama Mungu tena wanauogopa hasa
Miezi 11 humuoni msikitini ila mwezi ukiandama tu unamuona na kanzu sasa Mama akikataa kosa liko wapi?
 
Ukewenza mgumu Tena upate mume kisirani 😀😀
 
Ila mama wa binti amekataa mtoto wake asiolewe mke wa pili

Wanawake wameumbwa na wivu mkuu
Unaambiwa hata hao wake wa mitume walikuwa wanaoneana wivu , kukataa ni moja ya wivu wa mwanamke kutaka kuwa pekee Kwa mme wake , sio kitu cha hajabu.
 
Back
Top Bottom