Kwanini wazee wa zamani waliweza kuishi na ndugu wengi nyumbani, lakini kizazi hiki ni ngumu kuishi na ndugu?

  • Maisha yalikuwa rahisi.
  • Wazee walikuwa watata kinoma. Moto akihitimu la Saba tu, kesho yake anasepa mjini kukwepa amri na maelekezo magumu ya baba. Mama akizingua, mnavurugwa nyumba nzima na kutawanyika kama sisimizi.
Hahaha ukoloni nadhani ndio njia nzuri ya kuendesha familia kubwa, mzee wangu alikua mtata sana, chumba chake cha kulala zilikua fimbo zimeshakatwa zimekauka zinasubiri mtu ajichanganye.
 
Zamani ndugu walikuwa wazalendo kwenye familia wanazobebwa.
Siku hizi wengi wamejaa majungu, uchonganishi, lawama, us itch na hata ukicheza wanavunja nyumba.

Siku hizi pia wasimamizi wa familia hawakai nyumbani muda mwingi kama baba na mama wako bize wote. Hapo Lazima kandugu kavimbe na kuleta usumbufu.
 
Mkuu,
Nyumbani kwetu palikua hapakauki wageni..

Mimi nilikuaga naleta washikaji na marafiki tuna kula na kukaa Sana
home na wanapata huduma zotee

NB.
Mjini hakuna SHAMBA na Ile communion mode of production (ujamaa ulio changamka) yaan mtu Hana pressure na maisha Ila Sasa Maisha ya town kizungumkuti...
 
zamani kuna mfumo wa kijamaa ambao ulikuwa unafavor sana udugu,pesa enzi za ujamaa haikuwa na thamani hivyo ilisababisha mpaka vyakula kupatikana bei cheee,...idadi ya watu haikuwa kubwa rasilimali zilikuwepo za kutosha baharini,nchi kavu n,k


hivi aliyegundua nazi ni chakula ni nani?
 
Siku hizi maisha yamekua ghali,na Pesa imekua na matumizi mengi,zamani maisha kula tu,but now kipato kidogo utalipa Kodi,,umeme,maji,mlinzi,taka,King'amuzi,airtime, internet,usafiri,..shule Hadi za kata michango daily, unaweza kuchukua watoto wadada ukae nao??na nyumba za kupanga now hawawezi kukupangisha ujaze watoto watano chumba kimoja,kipato Cha kupanga nyumba nzima unacho??
 
Mjini 'maisha ya kupima'...utasikia, "kapime unga robo"; kapime mkaa kopo moja"; kapime sukari kibaba". Ndugu yangu mmoja alisikia hayo akaondoka mwenyewe, kasema hajazoea maisha ya kupima!!! 😀😀
Sisi tumezaliwa mjini, hao ndugu walikua wanatoka kijijini kuja kujitafuta mjini, maana mzee alitangulia kuingia mjini.
 
Zamani chakula hakikuwa cha kununua.. Sehemu kubwa kilitoka kwenye mashamba na bustani za familia
Sikuhz chakula tu ni almost 50% ya kipato

Na watu wameacha kula mihogo, viazi, mahindi nk...

Mm nakumbuka nyumbani ilikua asbh viazi au mihogo, mchana ugali na mboga za majani ambazo ni za kuchuma tu nyuma ya nyumba, usiku kama sio ugali tena basi ni wali maharage kama ni msimu wa mchele. Haya muite ndg yako leo kwako umlishe hvo kama hutoishia kulaumiwa tu
 
Kweli, pesa inatawanyika, enzi hizo hakuna umeme, kwa hiyo gharama za vifurushi hakuna, maji tunaamka asubuhi nyumba nzima kwenda kuchota maili 2
 
Sultan sayyid said 😅 mpaka aka shift his capital from mascat to Zanzibar..

Alienda ku Establish coconut 🥥 & clove plantations hapo Zanzibar maana zilikua na soko Sana in Arabs countries & far east
 
Cha ajabu sasa hivi MTU unakaa peke yako na bado kuna siku unapiga pasi ndefu.


Mimi hapo nachojua uhaba wa chakula umekuwa tatizo sana kwa familia nyingi hivyo mtu kuishi na ndugu zake na awapatie mahitaji yote muhimu sio jambo jepesi.



Ila kiimani ukiwa na uwezo kiasi ni vizuri kuwasapoti ndugu zako na kuishi nao kuna karma utazivuna.
 
ujamaa vs ubepari -population increase
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…