Moisemusajiografii
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 43,960
- 77,533
Na hao wageni walibeba vyakula,ndege(kuku,bata)na masurufu mengine kupeleka waendapo.Zamani chakula hakikuwa cha kununua.. Sehemu kubwa kilitoka kwenye mashamba na bustani za familia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na hao wageni walibeba vyakula,ndege(kuku,bata)na masurufu mengine kupeleka waendapo.Zamani chakula hakikuwa cha kununua.. Sehemu kubwa kilitoka kwenye mashamba na bustani za familia
Hahaha ukoloni nadhani ndio njia nzuri ya kuendesha familia kubwa, mzee wangu alikua mtata sana, chumba chake cha kulala zilikua fimbo zimeshakatwa zimekauka zinasubiri mtu ajichanganye.
- Maisha yalikuwa rahisi.
- Wazee walikuwa watata kinoma. Moto akihitimu la Saba tu, kesho yake anasepa mjini kukwepa amri na maelekezo magumu ya baba. Mama akizingua, mnavurugwa nyumba nzima na kutawanyika kama sisimizi.
Mkuu,Nimefikiria sana mpaka nimekosea majibu, tulizaliwa watoto saba nyumbani, na ndugu waliokuja kuishi nyumbani kipindi tunakua wanafika 6, hao waliosomeshwa na mzee, japo wengine walikua wanakuja na kuondoka, mabinti wengine walikua wanakuja kujifunza cherehani na kuondoka, na sio kwamba mzee alikua na maisha mazuri hapana ya kawaida tu wala hakua mtumishi wa serikali, japo ndugu kutoka kijijini walikua hawakatiki pale nyumbani kiukweli tulikua na familia kubwa yenye upendo, mpaka sasa mzee ameshazeeka na tumeshakua watu wazima, lakini bado ndugu wapo huko nyumbani pamoja na wajukuu kutoka sehemu mbalimbali.
Nikipiga mahesabu yangu na nina watoto wawili wako primary lakini maisha yananiendesha, yaani nawaza hapa wakiongezeka ndugu wengine nitaweza kuiendesha hii familia? Sasahivi vijana wengi wanavipato lakini ni ngumu sana kumsomesha ndugu yake ukiachana na ndugu wadamu, lakini mtoto wa baba mkubwa sijui mama mkubwa upendo haupo kabisa.
Hapa nawaza wazazi walikua na upendo sana au walikua na uwezo? Au maisha yalikua cheap miaka hiyo?
Chakula bure unamaanisha nini mkuuHadi saivi wanaishi nao lakini ni vijijini, mjini huwezi kukaa na watu wengi kwasababu chakula ni gharama, lakini kijijini hasa usukumani chakula ni bure na wanapeana hadi nafaka bure kabisa
Ukishajaa hofu ya maisha huku unajidai unapenda ibada unapaswa kuitwa mnafiki mwenye AA+Watu wa zamani waliamini katika Mungu.
Watu wa sasa hawaamini katika Mungu, wamejawa na hofu ya maisha ingawa watu wa sasa ni wapenda ibada sana.
Sisi tumezaliwa mjini, hao ndugu walikua wanatoka kijijini kuja kujitafuta mjini, maana mzee alitangulia kuingia mjini.Mjini 'maisha ya kupima'...utasikia, "kapime unga robo"; kapime mkaa kopo moja"; kapime sukari kibaba". Ndugu yangu mmoja alisikia hayo akaondoka mwenyewe, kasema hajazoea maisha ya kupima!!! 😀😀
Sikuhz chakula tu ni almost 50% ya kipatoZamani chakula hakikuwa cha kununua.. Sehemu kubwa kilitoka kwenye mashamba na bustani za familia
Ni roho za kishetani zimewashika watuUkishajaa hofu ya maisha huku unajidai unapenda ibada unapaswa kuitwa mnafiki mwenye AA+
Kweli, pesa inatawanyika, enzi hizo hakuna umeme, kwa hiyo gharama za vifurushi hakuna, maji tunaamka asubuhi nyumba nzima kwenda kuchota maili 2Siku hizi maisha yamekua ghali,na Pesa imekua na matumizi mengi,zamani maisha kula tu,but now kipato kidogo utalipa Kodi,,umeme,maji,mlinzi,taka,King'amuzi,airtime, internet,usafiri,..shule Hadi za kata michango daily, unaweza kuchukua watoto wadada ukae nao??na nyumba za kupanga now hawawezi kukupangisha ujaze watoto watano chumba kimoja,kipato Cha kupanga nyumba nzima unacho??
Sultan sayyid said 😅 mpaka aka shift his capital from mascat to Zanzibar..zamani kuna mfumo wa kijamaa ambao ulikuwa unafavor sana udugu,pesa enzi za ujamaa haikuwa na thamani hivyo ilisababisha mpaka vyakula kupatikana bei cheee,...idadi ya watu haikuwa kubwa rasilimali zilikuwepo za kutosha baharini,nchi kavu n,k
hivi aliyegundua nazi ni chakula ni nani?
ujamaa vs ubepari -population increaseCha ajabu sasa hivi MTU unakaa peke yako na bado kuna siku unapiga pasi ndefu.
Mimi hapo nachojua uhaba wa chakula umekuwa tatizo sana kwa familia nyingi hivyo mtu kuishi na ndugu zake na awapatie mahitaji yote muhimu sio jambo jepesi.
Ila kiimani ukiwa na uwezo kiasi ni vizuri kuwasapoti ndugu zako na kuishi nao kuna karma utazivuna.
Bure yaani hawanunui wanachotaChakula bure unamaanisha nini mkuu