Lengo lilikuwa kufika india na east asia kiujumla.
Chukua atlas hapo utanielewa kwa jinsi gani ingekuwa ni mbali sana kupitia nchi kavu, ukizingatia usafiri ulikuwa ni mgumu, pia njiani kulikuwa na maadui wengi wa kiutawala kutoka falme na nchi zingine.
Proposal hiyo ya Columbus ilikuwa ni kuzunguka kupitia atlantic ili kutokea upande wa pili (hapa ni baada ya watu kuwa na uelewa wa kwamba dunia ni duara).
Tatizo hapa ilikuwa hakuna ajuaye kuwa kuna bara jingine upande huo, hivyo wali-assume wangefika asia ya mashariki moja kwa moja.
Ila ndo hivyo, baada ya muda mrefu wa safari, wakatia nanga katika bara wasiolijua (america).
Waliwakuta wenyeji, i.e. wahindi wekundu wakawaua kibao. Kiufupi ni kwamba wakatwaa ni kwao. Baada ya feedback kurudi ulaya, na mataifa mengine yakafuata. Hivyo america ikawa ni territory ya watu weupe.
Additionally, kwa nini east asia? - ni kwa sababu kulikuwa na biashara 'iliyochangamka' zaidi ukizingatia kulikuwa falme/mataifa tajiri, civilized yenye maendeleo.
Cha kukumbuka tu, ni kwamba origin ya watu weupe kiujumla ni ulaya. Huko kwingine ni kwa sababu walivamia tu.
Hivyo, kama afrika ilivyofanywa, ndivyo amerika ilifanywa hivyo hivyo.
Nchi za asia ilishindikana kwa sababu tayari wenyeji walikuwa na maendeleo yao binafsi including silaha.
Lakini, bado waliziweza nchi kadhaa kuzitawala, ingawa mwisho wa siku walipinduliwa tena.
Hii ndio maana asia wanajiamini na tamaduni zao.
Kwa hiyo, simply, Amerika ilipatikana by accident. Lakini mwisho wa siku walifanya scrambling na patition kama Afrika.
Sent from my TECNO-W3LTE using
JamiiForums mobile app