MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Wakuu kama kichwa cha habari kinavyojieleza naomba tujadili hili.
Binafsi nimekulia kwenye mkoa wa kitalii ambapo nimeshuhudia vijana wengi wakienda ughaibuni kutafuta maisha.. Arusha na Ulaya zina uhusiano mzuri. Vijana kwenye utalii hupata fursa za kwenda huko. Pia wanamichezo kupitia riadha huenda nchi za Ulaya na America. Hata mimi mwenyewe nilikuwa na ndoto za kwenda huko ila shule ikanibana.
Katika watu ninaowafahamu walioenda Marekani ni kwamba wengi wao huwa wanarudi hawana kitu na pia ni kama kisaikolojia hawako sawa. Kuna siku tulikuwa kwenye sherehe akaja jamaa mmoja kavaa tshirt na jeans anaonekana kama vile afya imetetereka nikaambiwa huyo kaja likizo from the USA. Pia hapa mtandaoni kuna mtu maarufu sana aliishi marekani miaka mingi ila mienendo yake baada ya kurudi unaona kama kuna kitu kinamtesa akilini. Nina mifano mingi ya watu maarufu na wasio maarufu walioenda Marekani na kurudi hawako sawa.
Huu ni mtazamo wangu binafsi. Pia niseme kuna ambao walienda wakafanikiwa sana.