Kwanini wengi wa wanaoenda Marekani kutafuta maisha huwa wanarudi hawana kitu na kama vile kisaikolojia hawako sawa?

Kwanini wengi wa wanaoenda Marekani kutafuta maisha huwa wanarudi hawana kitu na kama vile kisaikolojia hawako sawa?

Wengi wanaenda kule wakiwa na matarajio makubwa kumbe si hivyo na maisha kule ni ghali kuanzia kula,kuvaa na kulala na huduma za afya bora hapa kwa huyu Mama wa Vikoba anaenda kukopa kule analeta hela nyumbani japo anazila na wanae.
Mkuu kule si kuna mitumba kuanzia Nguo, Simu, Na vitu vya ndani nasikia kuna sehemu watu wana vipeleka na kuviacha uko.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Kama huna cha maana bongo majuu ni sawa utaishi vizuri japo ndio kazi kazi.

Ila zile unaacha kazi ya ofisini au biashara nzuri bongo na vidigrii vyako unaenda kwa Biden, kazi unazopata ni za unskilled....kulea wazee, kufagia, landscape, kuuza supermarket n.k. Kama hujajiandaa kisaikolojia lazima uweweseke.

Miaka inaenda ukirudi nyumbani uliowaacha wamepiga hatua sana...wewe ni paycheck to paycheck na kule huwezi fungua duka au genge!!!

Mfumo wa kibepari pesa unayoipata yote inaishia kwenye matumizi ndio maana wengi wanarudi na stori, nguo na viatu.

Wanaotoboa ni wale wanakomaa na malengo kwanza kusoma kukr na kufanya kazi za "profession" baada ya kusoma kule. Wakiweza na kuwekeza nyumbani baada ya muda wanarudi mambo poa.
 
Wewe wasema. Nimeandika kwa kushuhudia baadhi ya watu. Sio stori ya kijiweni.

Nakazia tena. ACHANA NA STOTY ZA VIJIWENI. KAMA UNA FURSA ITUMIE HUTONISAHAU MPAKA SIKU UNAENDA KABURINI.

Faida ya kuishi Marekani ni nyingi sana boss.
Ukifeli Maisha Marekani huwezi kufanikiwa popote.( Ila sina maana sehemu zingine huwez kufanikiwa ila Marekani ina nafasi kubwa sana ya wewe kufanikiwa).

ISHI NA MANENO YANGU.
 
Kwani tunaoishi hii nchi yetu pendwa wote tumefanikiwa!?,unaweza kufanikiwa popote pia unaweza usifanikiwe popote ndio maisha yalivyo
 
Marekani mbali mbona hapa hapa Tanzania wapo walioachiwa mali nyingi na hawana kitu..Maisha ni mipango ya mtu wapo wadogo USA walikua wanajitambua toka walipokua SA wapo vizuri sana na wengine wapo UK niliwahi kwenda huko na mwakani tukijaaliwa ntaizunguka Dunia ila kwa wale walioenda wakiamini hiyo ndio Penati yaani nauli imepatikana kwa kuuza Shamba na vijiko huyo Mtu USA au popote kwenye fursa maisha kwake ni rahisi..wapo wadogo Texas,Chicago ni madereva wa Truck wengine wanafanya kazi hospital niliona wapo vizuri kutokana na kiwango wanachobaki nacho kulingana na mapato yao ya mwezi huko bongo wangebaki kuua kingi...
 
Naamini ukijitambua,ukiwa na malengo si haba unaweza ukaambulia chochote kitu ukiwa bado upo huko majuu na hata ukirudi rasmi pia unaweza ukafanya machache.

Na ni kweli inasemekana wapo wanaorudi bila ku-achieve chochote... nafkiri ni swala la kujitambua. Lakini pia maisha kila mtu ana bahati yake.

Naamini hivyo.
 
hata wakifa huko tunachangishwa huku matopeni gharama za kusafirishwa kuletwa huku,na wabongo wa huko wachache wanachanga lakini bado mpunga autoshi mwisho wanaamua wazike huko.
 
hata wakifa huko tunachangishwa huku matopeni gharama za kusafirishwa kuletwa huku,na wabongo wa huko wachache wanachanga lakini bado mpunga autoshi mwisho wanaamua wazike huko.
Ninafkiri huwaga ni ubinafsi tu maana wengi wakishafika huko hubadilika tabia na kuwa kama waliowakuta huko. Wanaamini kila mtu alikuja kimpango wake na chochote kitamkuta ni yeye mwenyewe kimpango wake lakini siamini kama wanashindwaga kuchangishana pesa kusafirisha maiti ya mbongo mwenzao.

Nasikia kuna watu wakifika huko hata kuchangamana na wabongo wenzao hawataki kabisa! Wanaamini hizi fitna zetu za huku na ushamba wetu + majungu, fitna na chuki binasi tunazipelekaga mpaka kule ndo mana huwa wanakwepana sana!
 
Back
Top Bottom