Kama huna cha maana bongo majuu ni sawa utaishi vizuri japo ndio kazi kazi.
Ila zile unaacha kazi ya ofisini au biashara nzuri bongo na vidigrii vyako unaenda kwa Biden, kazi unazopata ni za unskilled....kulea wazee, kufagia, landscape, kuuza supermarket n.k. Kama hujajiandaa kisaikolojia lazima uweweseke.
Miaka inaenda ukirudi nyumbani uliowaacha wamepiga hatua sana...wewe ni paycheck to paycheck na kule huwezi fungua duka au genge!!!
Mfumo wa kibepari pesa unayoipata yote inaishia kwenye matumizi ndio maana wengi wanarudi na stori, nguo na viatu.
Wanaotoboa ni wale wanakomaa na malengo kwanza kusoma kukr na kufanya kazi za "profession" baada ya kusoma kule. Wakiweza na kuwekeza nyumbani baada ya muda wanarudi mambo poa.